LGE2024 CCM: Lazima mkubali mambo yanabadilika na humuwezi kuwadanyanya watu siku zote

LGE2024 CCM: Lazima mkubali mambo yanabadilika na humuwezi kuwadanyanya watu siku zote

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Demokrasia ipo kama kivuli tu,kiukweli hakuna demokrasia nchini wala hakuna mfumo wa vyama vingi vya siasa,kuna hawa tuliowachoka wanaojiona wao ndo wao
 
Uchaguzi ungekuwa huru wangechapika vibaya mno
Unajua mwisho wao utakuwa wapi? Hatakapo ruhusu tu wagombea wengi wa vyama ya upinzani watu wanapiga kura kwa hasira ndo wanatapoteana na hawataamini kinachotokea!
Muda wa kubadilika ni sasa!
 
Unajua mwisho wao utakuwa wapi? Hatakapo ruhusu tu wagombea wengi wa vyama ya upinzani watu wanapiga kura kwa hasira ndo wanatapoteana na hawataamini kinachotokea!
Muda wa kubadilika ni sasa!
Wameshagundua wamechokwa wameogopa kuaibika
 
Wameshagundua wamechokwa wameogopa kuaibika
Uongo siku zote haudumu maana giza haliwezi kuushinda mwanga!
CCM haina zaidi ya miaka 10 ijayo kwa mfumo huu wanao enda nao hawatoboi hata wafanye figisu kiasi gani watafeli tu!
 
Muda utaongea
IMG-20241127-WA0124.jpg
IMG-20241127-WA0123.jpg
ndo maana figisu ni nyingi
 
napenda sana kuona hivi nchi nzima jamani, hongereni huko
 
CCM ni chama kikubwa chenye historia kubwa ndani ya nchi na nje ya nchi lakini nashauri yafatayo!

CCM kwenye chaguzi kuanzia 2019 imekuwana na woga kushindana na vyama vingine na kupelekea watu wengi kuona zoezi la uchaguzi halina maana

CCM itambue kizazi kinabadilika na kusema kweli watu wengi wanataka mabadiliko yatayotoka ndani ya CCM au ndani ya upinzani kwa maana ya watu kuchoka kuwa chini ya chama kimoja na hiyo ni hulka ya binadamu kwa asili!

CCM kujiandaa kwa miaka ijayo kwa maana wahenga wanasema huwezi kuwadanganya watu muda wote,Nasema hayo kwa maana haitawezekana miaka yote kuwa na uchaguzi wa namna hii na mapungufu yake kwa maana sio asili ya mambo!

CCM inapaswa kutoogopa kabisa ushindani kwa sababu hata nchi zilizoendelea vyama hutawala kwa sera nzuri zinazokubalika na wananchi si kwa kufanya figisu au ujanja ujanja wa kisingizio cha watu kukosea kujaza fomu. Kuogopa uchaguzi ni ishara ya chama kuchoka na kuongeza chuki katika jamii.

CCM itambue viongozi wengi wanaopita bila kupingwa kwa maana ya kukosa wapinzani hawawezi kukijenga chama katika jamii kwa maana viongozi watokanao na uchaguzi kama huo huwa sio chaguo la wananchi.

CCM ina faida kubwa moja ina mtaji wa vipaji vingi vya uongozi na wachama wengi katika vijana,watu wa makamo na wazee.Kitu hichi kinaifanya CCM kuwa ni chama imara ila kinapungukiwa na viongozi shupavu wa kushindani.

CCM itambue ushindani halali ndo pekee utaifanya CCM kuwa imara na sivinginevyo maana ushindani huleta ushindi halali na kuheshimika na jamii!

CCM ikumbuke kabla ya 2015 wanachama walikuwa wanaogopa kutembea wakiwa wamevaa nguo za kijana kwa maana zomea zomea ilikuwa nyingi sana.

CCM hamjachelewa kuruhusu Ushindani kwa maana ushindani katoka uongozi ni kama damu katika mwili bila ushindani kinachofata ni mauti!

Niwatakie pole wote waliopata changamoto katika kipindi hiki cha uchaguzi!

Mungu awabarikini nyote!

View: https://youtu.be/doU05kVEoz0?si=Q8-XtN2cXCOHqHHs

Ndugu zangu nchi hii sasa tumebakia na kete mbili zilizo kuu ili tuondokane na vitisho na uongozi wa kidhalimu wa CCM chini ya SAMIA Suluhu Hassan ,kete ya kwanza ni ss wananchi kuamua kuandamana nchi nzima non stop kujitetea wenyewe dhidi ya mateso ya kutekwa na kuuawa kwa ndugu zetu mbalimbali.Kete ya pili ni JESHI la WANANCHI wa TANZANIA kama linavyofahamika kuchukua mamlaka kwa niaba ya wananchi kama kweli jeshi hili ni lao na liko kwa ajili ya wananchi.Mauaji yanayoendelea sasa naamin ni zaidi ya awamu zote zilizowahi kupita kuongoza Taifa hili.Kete hz mbili yoyote inaweza kuanza bila kusubiri nyingine kwa lengo la kuponya Taifa.Anayeshabikia watu kutekwa ,kuteswa na kuuawa ni kwa sababu hana upendo na uzalendo kwa watanzania wenzake.Majeshi ya wananchi kama ya Burkina faso,Mali na kwingineko yalipoona siasa chafu zinazonuka kama mavi zikiendeshwa ndani ya nchi zao majeshi hayo yaliingilia Kati ya kuwafurusha wanasiasa washenzi na wapumbavu wasio na Akili wanaohujumu nchi zao.JESHI letu linasemwa na kusifiwa kuwa lina weledi,nidhamu na maadili ya hali ya juu kabisa,Sasa SWALI la msingi linawezaje kuwa na sifa zote hizo Alafu linavumilia wananchi wake wakiteseka,je sifa hizi kea jeshi letu ni za kweli?.Kama nchi ni lazm tuache usanii na tujitafakari kwa kina na mapana.
 
Chaguzi tu za ndani ya chama zinaamuliwa na 'mapanga'.

Mshkaji wangu ni kampeni manager wa kata ameambiwa chama kikishindwa wanachokua pilipili, na CHADEMA walikaba kwenye kampeni hazijawahi tokea. Akisikia 'Peoples' Power" anaweweseka, anawasha pikipiki huyo ...
 
Hadi aibu.

Ndo maana walisisitiza sn kujiandikisha.Mimi sijagusa geti kutoka nje leo ila najua nimepigishwa kura maana nilijiandikisha nikijua uchaguzi utakuwa huru.
Nilipoona wanaenguliwa wa upinzani kwa speed kubwa nikasema siendi kujisumbua
 
CCM ipo sana; ipo kwa muongo kama 4 hivi.
Itaondolewa na ugumu wa maisha kipindi hicho hakutakuwa na fursa za uchawa na kubeba mikoba ya waandamizi, ardhi inayofaa kwa kilimo itakuwa hafifu sana na gharama za kilimo kubwa hivyo vijana wengi kushindwa kulima, hakutakuwa na fursa za umachinga (kila kijana atakuwa machinga), ....
 
Hahaha kikubwa tupate watu sahihi kwa mfumo sahihi sio ujanja ujanja!
Sio rahisi ccm kubadilika. Na kwa bahati mbaya hakuna mwanaccm anakubaliana na ukweli huu ndio maana tunashuhudia chaguzi za kipuuzi mno. Ccm nawafananisha na watu wanaoogopa kupima ukwimi, kuliko waujue ukweli ni bora wakae bila kujua liwalo na liwe. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataleya mabadiliko ya kweli nchi hii.
 
Back
Top Bottom