Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini kimeonesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara inayounganisha maeneo ya Ilomba na Machinjioni, chini ya mradi wa TACTIC awamu ya kwanza.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi huo, Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Afrey Nsomba, alisema mradi huo ni ushahidi tosha wa dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha miundombinu na kuinua huduma kwa wananchi wa jiji la Mbeya.
Ziara hiyo iliambatana na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali waliokwenda kujionea kazi inavyoendelea kufanyika.
Barabara hiyo, ambayo inaendelea kujengwa na kampuni ya ujenzi ya Chongqing International Construction Corporation (CICO), inagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.384,588,000 na inalenga kurahisisha shughuli za usafiri na uchumi kwa wakazi wa Ilomba, Machinjioni na maeneo jirani.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamesema kuwa wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa hasa msimu wa mvua, lakini sasa wana matumaini makubwa pindi ujenzi utakapokamilika.
“Nyakati za mvua magari hayapiti kabisa, lakini sasa tunafurahia mabadiliko yanayoletwa na mradi huu,” alisema mmoja wa wakazi wa Machinjioni.
Mradi wa TACTIC ni miongoni mwa mikakati ya serikali ya kuendeleza miundombinu ya barabara katika maeneo ya mijini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi.