Uchaguzi 2020 CCM, michanganyo hii mwisho mtachanganyikiwa kabisa na kupoteana

Mshana Jr tofautusha Kati ya "VIONGOZI WA DINI NA VIONGOZI WA KIROHO"
wale malofa tunaowaona ni viongozi wa dini yaani kazi Yao kuongoza maisha Yao na matumbo Yao Ila viongozi wa KIROHO ni wale wanaoongoza mioyo ya watu ili waurithi ufalme wa MUNGU.... viongozi wa dini ni hao akina gwajima,Mzee Wa upako,nabii Tito,bakwata na katoliki
[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1534][emoji1534][emoji1548][emoji1548][emoji1548]
 
KUDOS
Hiki kilichoitwa jana KONGAMANO LA AMANI, badala ya kujikusanya pale kwenye ukumbi wa gharama na kula vinono kwenye AC, walitakiwa wakusanyike sehemu kama uwanja wa taifa na kufanya ibada ya kuliombea Taifa na watu wake wote. Kuombea:

  • Amani ya Taifa
  • Mshikamano
  • Upendo
  • Umoja
  • Msamaha na kusameheana
  • Ustawi wa Taifa na watu wake n.k, n.k
[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Usijaribu kumchanganya Mungu na shetani ..hizi ni falme mbili kinzani..japo ufalme wa Mungu ni mkubwa kuliko ufalme wa shetani. Kuna namna ya kuenenda na shetani na kuna namna ya kuenenda na Mungu; hupaswi kuzichanganya hizi falme mbili kwenye jambo moja.
Kwa ccm ambao wameamua rasmi kushikamana na 'yule aliye kinyume na Mungu' wala sio la kushangaa matendo yao.
Yanayofanyika yanaakisi kabisa kuwa yana msaada wa 'yule mwovu' kwani wenye hofu ya mUngu hawawezi kabisa kufanya haya!
 
Sikumbuki kama nilimsikia hata mmoja akilitamka neno HAKI
 
Mungu si mwanasiasa bali wanasiasa wana miungu. Shetani si mwanasiasa bali wanasiasa wana vishetani vyao.

Siasa ni imani lakini siasa sio dini. Siasa ina wafuasi na dini pia ina wafuasi, lakini si lazima mfuasi wa dini awe mfuasi wa siasa na kinyume chake.

Ni muhimu think tank ya CCM ielimishwe sasa kwakuwa ikizidisha hii michanganyo mwisho itachanganyikiwa, na ikichanganyikiwa inaweza kufanya mambo bila ufahamu kamili. Sijui ni hofu ama ni nini, lakini dalili zinaonesha wazi CCM imejawa hofu.

Hofu huleta woga
Hofu huondoa ujasiri
Hofu huleta taharuki
Hofu huondoa ufahamu

Kila jambo ni mchakato na kila mchakato una formula zake, wabobezi wa kemia wanalijua hili vema. Ukikosea formula huwezi kupata matokeo tarajiwa.

Usijaribu kumchanganya Mungu na shetani ..hizi ni falme mbili kinzani..japo ufalme wa Mungu ni mkubwa kuliko ufalme wa shetani. Kuna namna ya kuenenda na shetani na kuna namna ya kuenenda na Mungu; hupaswi kuzichanganya hizi falme mbili kwenye jambo moja.

Ndani ya wiki moja CCM imezichanganya falme mbili, matokeo yamekuwa hasi. Lilianza kitu kinachoitwa 'tamasha la wasanii' wasiopungua 200, wote tulishuhudia ufalme wa giza ulivyosujudiwa pale. Shetani alipewa airtime ya kutosha kabisa.

Siku chache baadae likaja kitu kinaitwa 'kongamano la amani' wahusika walikuwa ni viongozi wa dini mbalimbali walionona kweli kweli, wakajaribu kuusimika ufalme wa Mungu pale.

Mwaka uliopita lilijitokeza kundi la watu mia moja taslimu waliojiita waganga wa kienyeji mashuhuri Tanzania, wakatoa onyo na kupiga mikwara yao.

Think tank ama kitengo cha propaganda, kilitakiwa kufanya nini ili kisiharibu taswira ya chama mbele ya wananchi?

Wale watu mia moja taslimu hawakupaswa kupewa jina la WAGANGA WA KIENYEJI, walau basi wangeitwa wazee wa mila. Lakini je, ni kweli kabisa uganga wa kienyeji unafanya kazi kwa jinsi ile? Jibu ni HAPANA. Kwahiyo basi kule kulikuwa ndiyo mwanzo wa kuchanganyikiwa.

Hiki kilichokuja kuitwa TAMASHA LA WASANII kingetakiwa kufanya nini?

Ili kuonesha UTU na kujali pamoja na nyimbo zao zile wangetawanywa na kwenda kutoa huduma za kijamii kwa wahitaji na wasiojiweza, wangetawanywa kwenye mahospitali, nyumba za watoto yatima na zile za kulelea wazee wasiojiweza. Ssehemu ya pesa iliyotumika kuwalipa wasanii ingetumika kuwahudumia hawa wahitaji.

Hiki kilichoitwa jana KONGAMANO LA AMANI, badala ya kujikusanya pale kwenye ukumbi wa gharama na kula vinono kwenye AC, walitakiwa wakusanyike sehemu kama uwanja wa taifa na kufanya ibada ya kuliombea Taifa na watu wake wote. Kuombea:
  • Amani ya Taifa
  • Mshikamano
  • Upendo
  • Umoja
  • Msamaha na kusameheana
  • Ustawi wa Taifa na watu wake n.k, n.k
Hivi inaleta picha gani kwa wagonjwa wenye uhitaji mkubwa wa vifaa tiba na madawa pale Hospital ya Temeke wakiwa hawajapewa kwa serikali kukosa pesa lakini wakati huohuo chama chenye serikali kikifanya ufujaji mkubwa wa pesa kwa vijana wahuni, barobaro na 'wavuta bhangi' wasiojitambua waliolipwa malipo wasiyostahili?

Hivi inaleta picha gani kwa wagonjwa waliolala pale Ocean rd na Muhimbili wakidaiwa pesa za matibabu ambazo hawana uwezo nazo wanakufa wanajiona huku viongozi wao wa kidini kwa sura zilizong'aa na nyuso zilizonona wakikaribishwa kwenye hafla ya kusifu na kuabudu? Badala ya kupendwa ndio kwanza wataanza kutengeneza chuki.

Chama kilifadhili kusanyiko la waganga wa kienyeji 100
Chama kikafadhili tamasha la wasanii 200
Chama kimefadhili kongamano la amani Tanzania la viongozi wa dini- sina idadi yao
Ni jambo jema kwakuwa chama kina miradi mbalimbali, lakini je, hayo ndio matumizi sahihi ya mapato?

Think tank
ya CCM inapaswa kujitafakari upya. Maamuzi ya kukurupuka kwa ajili ya hofu yanaweza kuliweka taifa kwenye mtanziko mkubwa.
Umelitumia vibaya neno 'think tank'
Hapa bongoland hakuna mtu au kukundi kinachostahili sifa hiyo.
 
Think tank ya CCM inapaswa kujitafakari upya. Maamuzi ya kukurupuka kwa ajili ya hofu yanaweza kuliweka taifa kwenye mtanziko mkubwa.
Safi kabisa ndugu yangu naunga mkono hoja , ila sikio la kufa halisikii dawa .
 
Umelitumia vibaya neno 'think tank'
Hapa bongoland hakuna mtu au kukundi kinachostahili sifa hiyo.
Dah brother tusijishushe kiasi hiki tafadhali tusijidharau kwa kiwango cha kutia aibu
 
Mkuu kwa Wakristo wanaijua hiyo. Unaitwa Utwala wako Umefitinika na umegawanyika . Huyo ni Nebuchadnezzar utawala wa Babiloni alivyopewa ujumbe baada ya kuanza kuabudu miungu. Ipo kwenye kitabu cha DANIELI 5:25. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI

Tabia na mwenendo wa Magufuli ni kama Nebuchadnezzar kabisa. Na tayari amefitinika kwa namna alivyowatenga waliompigania kupata Uraia mwaka 2015
Nadhani mkuu unakosea kwa kusema waliompigania kupata Urais, unamaanisha walifanya hivyo kwa ajili ya nafsi na matombo yao sasa wamekosa wanalalamika. Kwa hiyo kila anayeshindania nafasi fulani ya uongozi inabidi awabebe wale wote waliokuwa nao kwenye kampeni hata kama hawatoshi ktk nafasi walizonazo?
 
Mshana umewai kuona wapi kwenye kundi la viongozi wa dini kuna ASKOFU Malasusa, ASKOFU Sothteness alafu Kuna SHEIKH sharif majini???

Umewai ona wapi huo mchanganyiko wa viongozi wa dini?????

Tunaposema CCM wamechanganyikiwa na Lissu mjue wamechanganyikiwa kweli!!!!

Ndani Ya Kamati Za Amani...
 
[emoji23][emoji23][emoji23] kwamba askofu na mganga wa kienyeji wanakaa pamoja??? Kweli CCM subirini maziko tu!!
Usiwafokee basi..subiri watoke ndani walikojifungia kimya
JamiiForums497226166.jpg
 
Back
Top Bottom