CCM msipumbazike na kula, kunywa na kushiba hata mkalewa msioone hatari iliyoko mbele yenu

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Nimetoa mada "Rais Samia Suluhu Hassan, alama ya mwisho ya anguko la utawala wa siasa za CCM Tanzania...."

Wengi hawajanielewa na kusema it's a delusional....

Dunia hii ina historia pevu sana inayoweza kutufundisha na kutujuza tulikotoka. Tunaweza kutumia matukio yaliyopita (historia) ili kutuelekeza yatupasayo kufanya sasa.....

Tanzania ni sehemu muhimu ya dunia hii. Haiwezi kujitenga na historia ya dunia ya kale, ya Jana, ya juzi na ya sasa....

CCM ni chama kinachotawala Tanzania tangu Uhuru wa Tanganyika 1961 na tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964....

Hawa watu mpaka sasa wanachojua wao ni kitu kimoja tu kwa sasa....

"....Kwa kuwa TUNAKULA na KUNYWA na KUSHIBA hadi kusaza, basi ni nani awezaye kuwa juu yetu....?"

Kunywa, kula na kushiba hadi kusaza kumeshawalevya. Hawaioni hatari iliyoko mbele yao. Hawauoni mwisho wao unaowatazama kwa macho makali na angavu....

Dunia ya kale ya kina Luthu, Nuhu, Nebukadneza, Dario, Alexabder The Great (Roman Empire) inaweza kutupa somo zuri sana....

Na the Latest ni dunia ya kina Adolf Hitler, Benito Mussolini, Iddi Amin Dada, Daniel Arap Moi (KANU) Kenya, Kenneth Kaunda (UNIP) Zambia and so forth inaweza kuwapa somo nzuri CCM, watawala wa sasa katika Tanzania yetu....

Lakini ni heri yetu kwa kuwa kula na kunywa na kushiba na na kusaza na kisha kulewa, kumewapumbaza na kuua fikra za ufahamu zao....

Kula na kunywa kumewapumbaza kiasi cha kila sauti inayosikika masikio mwao inaonekana kuwa ni upuuzi na kelele zisizo na maana....

Wamejisahau na kutojua kuwa wamepewa dhamana na Mungu muumba kutawala watu wake kwa HAKI....

Hata Roman empire iliyooanguka kwa kishindo kikuu, walikuwa kama walivyo watawala hawa wa Leo...

Walikuwa wakila na kunywa huku mauti na anguko la dola yao kuu iliyotawala ulimwengu wote liliwanyemelea kimya kimya bila wao kujua....

Hawakujali sauti yoyote ya kukosoa wala ya maonyo kwa sababu walisema, "sauti za chura kwenye dimbwi la maji hazimzuii ng'ombe kunywa maji hayo....."

Walikuwa wakila na kunywa na kulewa ,na mwisho wao uliwakuta bila taarifa ktk starehe zao na mpaka leo hawaelewi nini kilitokea....

Hata hivyo, ni bora mwisho huo wa CCM ukaja haraka na mapema. Na huo unakuja. Nasi tunasema na uje sasa...AMEN.
 
CCM ndio chama kilichofanikisha mafanikio na maendeleo yote tuliyonayo kiuchumi, kisiasa na hata kijamii

Pamoja na mapungufu yaliyopo CCM imejenga msingi imara sana wa Taifa hili. Imejenga msingi wa umoja, upendo, amani kwa njia ambayo ni ngumu sana kwa nchi nyingine.

Miaka 60 ya uhuru Tanzania hakuna ugomvi wala vita ya wenyewe kwa wenyewe kwenye udini wala ukabila, na wala kwa jinsia; kwa maana hiyo kwa yoyote mwenye nia ya kulisambaratisha taifa letu njia yoyote ni ngumu sana.

Tunapokua tunawakosoa tusisahau kwamba hata huu uwezo wa kukosoa wametujengea wao
 
Upinzani ulipofeli 2015 tu!! Sjui tena itachukua miongo mingapi
Tunapanga mengi, tunategemea mengi, kwa wakati tunaoutaka lakini Mungu hakosei, hata ombi unalofikiria kuwa halijamfikia, lipo katika himaya yake.

Yeye hakawii wala hakosea, huyajibu maombi kwa wakati ufaao na kwa namna ifaayo maana hekima ya Mungu siyo ya mwanadamu.

Mliomba utawala wa Tanzania ubadilike. Wapo waliotaka utawala wa marehemu Magufuli ubadilike kutoka kuwa utawala dhalimu uwe utawala wa heri. Wapo walioomba CCM ianguke kwenye uchaguzi ili Serikali ibadilike, iingie Serikali ya cha cha upinzani. Wapo walioomba, ikiwezekana Magufuli asiteuliwe na chama chake kuwa mgombea wa Urais. Wapo walioomba tupate utawala mzuri, bila ya kujali ni wa chama gani. Sina uhakika kama wapo waliomwombea kifo mtawala. Lakini kipa aliyeomba, alitaka maombi yake yatimizwe mara moja. Wapo waliotarajia maombi yao yajibiwe wakati wa uchaguzi wa 2020. Baada ya uchaguzi, wengi waliinamisha vichwa chini wakiamini maombi yao hayakumfikia Mungu.

Kwa wakati usiotegemewa na mwanadaku lakini muda ulio sahihi kwa kipimo cha Mungu, mtawala amebadilika, serikali imebadilika. Chama ni kile kile, kiongozi ni mwingine, kutoka upande mwingine, dini tofauti, jinsia tofauti, hulka na malezi tofauti.

Hiyo ndiyo hekima ya Mungu. Baadhi wangependa labda angekuwa TL, wengine Membe n.k. lakini haijawa. Kwa nini haijawa, hakuna ajuaye. Wapo watakaofurahia kuwa bado ni CCM, wapo waliochukia kwa kuwa bado ni CCM, lakini Mungu anayeipenda Tanzania, ndiye anayejua ni namna gani nchi ipite, ifike kunakotakiwa bila ya majonzi makubwa.

Kuweni wenye imani, mabadiliko mazuri na yaliyo mema , yatakuja kwa wakati ulio wake.
 
Nimetoa mada "Rais Samia Suluhu Hassan, alama ya mwisho ya anguko la utawala wa siasa za CCM Tanzania"

Wengi hawajanielewa na kusema it's a delusional.

Dunia hii ina historia pevu sana inayoweza kutufundisha na kutujuza tulikotoka. Tunaweza kutumia matukio yaliyopita (historia) ili kutuelekeza yatupasayo kufanya sasa.

Tanzania ni sehemu muhimu ya dunia hii. Haiwezi kujitenga na historia ya dunia ya kale, ya juzi na ya sasa.

CCM ni chama kinachotawala Tanzania tangu Uhuru wa Tanganyika 1961 na tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Hawa watu wanachojua wao ni hiki kitu kimoja tu kwa sasa.

Kwa kuwa TUNAKULA na KUNYWA na KUSHIBA, nani awezaye kuwa juu yetu?

Kunywa, kula na kushiba hadi kusaza kumeshawalevya. Hawaioni hatari iliyoko mbele yao. Hawauoni mwisho wao unaowatazama kwa macho makali.

Dunia ya kale ya kina Luthu, Nuhu, Nebukadneza, Dario, Alexabder The Great (Roman Empire).

Na the Latest ni dunia ya kina Adolf Hitler, Benito Mussolini, Iddi Amin Dada, Daniel Arap Moi (KANU) Kenya, Kenneth Kaunda (UNIP) Zambia and so forth inaweza kuwapa somo nzuri CCM, watawala wa sasa katika Tanzania yetu.

Kula na kunywa na kushiba na kisha kulewa, kumepumbaza na kuua fikra za ufahamu zao.

Kula na kunywa kunapumbaza kiasi cha kila sauti inayosikika kuwa ni upuuzi.

Hata Roman empire iliyooanguka kwa kishindo kikuu, walikuwa kama ninyi. Walikuwa wakila na kunywa huku mauti ikiwanyemelea kimya kimya.

Hawakujali sauti yoyote ya kukosoa wala ya maonyo kwa sababu walisema, "sauti za chura kwenye dimbwi la maji hazimzuii ng'ombe kunywa maji hayo"

Walikuwa wakila na kunywa na kulewa ,na mwisho wao ulivyowakuta bila taarifa ktk starehe zao.

Hata hivyo, ni bora mwisho huo wa CCM ukaja haraka na mapema. Na huo unakuja!
Unaandika Kama mtu wa kiroho Sana,naanza kuogopa.
 
Warumi 13: 1-7​

Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.

Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu.

Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.

Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu.

Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala.

Walipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.
 
Uzi wa pili wa ramli kutoka kwa The Palm Tree.
Yes, ni wa pili kwa Leo...

Mimi sio mtoa mada sana ktk jukwaa hili. Ila ni mmoja Wa wachangiaji wazuri kwenye mada za wengine...

Lakini juzi, jana na leo nimepata msukumo Mkubwa wa kuandika kuhusu haya...

Ni mawazo na maoni yangu tu. Hayashurutishwi mtu kusoma na kuyakubali...

Ruksa kwa mtu yeyote kuweza kuyapinga kwa namna yoyote ile hata kama ni kutukanwa...
 
CCM ndio chama kilichofanikisha mafanikio na maendeleo yote tuliyonayo kiuchumi, kisiasa na hata kijamii

Pamoja na mapungufu yaliyopo CCM imejenga msingi imara sana wa Taifa hili. Imejenga msingi wa umoja, upendo, amani kwa njia ambayo ni ngumu sana kwa nchi nyingine.

Miaka 60 ya uhuru Tanzania hakuna ugomvi wala vita ya wenyewe kwa wenyewe kwenye udini wala ukabila, na wala kwa jinsia; kwa maana hiyo kwa yoyote mwenye nia ya kulisambaratisha taifa letu njia yoyote ni ngumu sana.

Tunapokua tunawakosoa tusisahau kwamba hata huu uwezo wa kukosoa wametujengea wao
Ninyi ndio wanufaika wa keki ya Taifa. Ongereni ila siku yenu yaja.
 
Warumi 13: 1-7​

Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.

Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu.

Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.

Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu.

Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala.

Walipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.
Biblia ipo kwenye msingi wa upendo na haki.
Mamlaka hutoka kwa Mungu, i.e iliyopatikana kwa njia halali, inayotenda haki.
Ni sawa na kutumia hela haramu kama sadaka, kisa tu Mungu amesema kupitia Biblia nijaribuni kwa zaka na dhabihu.
Note : Sikuwa na mpango wa kuchangia ktk post hii
 
Umekua nani wewe uanze kutengua maandiko!? Au unataka kumwambia Mungu hiyo serikali unayoichukia ipo madarakani sababu yeye alishindwa kuizuia isiwepo??

Umeambiwa..... "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu."

Wewe umeshaambiwa TII ni KUTII tuu bila shurti😆😆
 
Ninyi ndio wanufaika wa keki ya Taifa. Ongereni ila siku yenu yaja.

Siku yetu ikija hatuna shida..... tutaendelea kutii mamlaka bila shurti

Maana tumeambiwa..... "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu."
 
CCM ndio chama kilichofanikisha mafanikio na maendeleo yote tuliyonayo kiuchumi, kisiasa na hata kijamii

Pamoja na mapungufu yaliyopo CCM imejenga msingi imara sana wa Taifa hili. Imejenga msingi wa umoja, upendo, amani kwa njia ambayo ni ngumu sana kwa nchi nyingine.

Miaka 60 ya uhuru Tanzania hakuna ugomvi wala vita ya wenyewe kwa wenyewe kwenye udini wala ukabila, na wala kwa jinsia; kwa maana hiyo kwa yoyote mwenye nia ya kulisambaratisha taifa letu njia yoyote ni ngumu sana.

Tunapokua tunawakosoa tusisahau kwamba hata huu uwezo wa kukosoa wametujengea wao
Unasema CCM "Imejenga msingi wa umoja, upendo, amani", lakini unasahau kuwa ndio CCM hiyo hiyo iliyoendekeza siasa za kibaguzi?
 
Umekua nani wewe uanze kutengua maandiko!? Au unataka kumwambia Mungu hiyo serikali unayoichukia ipo madarakani sababu yeye alishindwa kuizuia isiwepo??

Umeambiwa..... "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu."

Wewe umeshaambiwa TII ni KUTII tuu bila shurti😆😆
Duuh, huyaelewi maandiko. Umejipotosha mwenyewe na unataka kupotosha wengine...

Naomba nikurejeshe kwenye mstari, usiendelee kupotea. Nitatumia mfano mmoja ktk Biblia kuelezea hili...

Unamfahamu mtu mmoja anaitwa Daniel..? Stori hii inapatikana katika Biblia > [SOMA: Daniel 6: 1 - 25]

Ni mfano wa mtu boldly mmoja anaitwa Daniel aliyekataa kutii AMRI halali toka kwenye MAMLAKA HALALI YA KISERIKALI YA KIBINADAMU ya mfalme (Rais) Dario wa Umedi na Uajemi iliyotaka kila mtu aabudu sanamu ya dhahabu ya kuchongwa ña yeye mfalme (Rais) badala ya kumwabudu Mungu Yehova wa kweli...

Amri ilisema anayekataa kutii amri hiyo angepata adhabu ya kifo cha kutupwa kwenye shimo la simba wala watu ili aliwe na afe...

Kwa sisi hapa tunaweza kusema angepotezwa, kuteswa, kupigwa risasi ufe kabisa kama Tundu Lissu na adhabu zingine zifananazo na hizo...

SASA TUJIFUNZE NINI KWA MFANO HUU vs HOJA KILA MTU KUTII MAMLAKA HALALI KWA KUWA KILA MAMLAKA IMEWEKWA NA MUNGU...?

å Biblia inaposema "kutii mamlaka halali kwa sababu kila mamlaka yatoka kwa Mungu.." haina maana unayoielewa wewe. Unapotea ndugu yangu. Unamsaidia shetani kutimiza ajenda zake ovu dhidi ya binadamu...!

å Siyo kila mamlaka za kiserikali za kibinadamu zinatoka kwa Mungu. Mamlaka zingine ni totally zinatoka kuzimu kwa shetani zikiwatumia watu wenye miili ya kibinadamu kutawala wanadamu...!

å Biblia inasema "...mtawatambua kwa matendo yao..." na pia Biblia hiyo hiyo inasema ".....hamuwezi kushindwa kuzitambua hila (mikakati) yake..." anayotumia kuwalaghai binadamu ili atimize hila (motives) zake bila binadamu kutambua kama ulivyo wewe ulivyopotoka na kutaka kupotosha wengine...!

å Mathalani, lazima uelewe kuwa Mungu ni wa UWAZI, HAKI na UPENDO...

å Mungu hawezi kuweka serikali madarakani kupitia uchaguzi usio wa HAKI na WAZI unaoambatana na mauaji na kuumiza watu..

å Mtu yeyote atakuwa mjinga na mpumbavu sana kama atatii kila kitu atakiwacho kukifanya na mtawala wa serikali ya namna hii...

å Ni lazima tuwe kama Daniel. Ni lazima tuwe kama Tundu Lissu. Inashangaza na bahati mbaya sana kuwa baadhi ya watu huwa hawamuelewagi Tundu Lissu anapokataa na kuwapinga waziwazi watawala. Kama ilivyokuwa kwa Daniel, ndivyo ilivyotokea na inavyoendelea kutokea kwa watu wengi ktk serikali nyingi za kidunia na hapa Tanzania akiwemo Tundu Lissu kuhukumiwa adhabu ya kifo bila kupitia mahakamani..!

å Biblia inasema "...watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa........." [Hosea: 4:6]. Maarifa yanayosemwa hapa ni NENO LA MUNGU. Yaani kutoisikia na kuilewa SAUTI YA MUNGU. Binadamu kukataa kuongozwa na Mungu ktk maisha yao. Wanaongozwa na tamaa za miili yao, tamaa ya madaraka, tamaa ya mali nk ambayo provider wake ni "ulimwengu..." ambao unatawaliwa na Ibilisi...

Najua utasema au kupinga kuhusu Daniel kwa hoja ya ".....aaah, hiyo ilikuwa ni kuabudu sanamu ambayo hata mimi (wewe) ungekataa...!"

Ukiuliza nitakujibu vizuri tu Kibiblia maana kumbe kweli utakuwa huyajui maandiko ndiyo maana unapotea unnecessarily...!

Karibu

Unaandika Kama mtu wa kiroho Sana,naanza kuogopa.
Sio "kama" bali divyo nilivyo ndugu Niza Doyi...!

Yesu Kristo ndiye Bwana na mwokozi wangu. Nitatumia jukwaa hili kusema yaliyo ya Mungu. Nitawakemea, kuwakosoa na kuwaonya watawala na wote wanaopumbazwa na kupotosha nao kwa lugha kali kwa kadiri ya kuongozwa na Roho mtakatifu...

Niwieni radhi kwa andiko refu kidogo, lakini imenipasa kutoa maelezo marefu kidogo...
 
Nimetoa mada "Rais Samia Suluhu Hassan, alama ya mwisho ya anguko la utawala wa siasa za CCM Tanzania"

Wengi hawajanielewa na kusema it's a delusional.

Dunia hii ina historia pevu sana inayoweza kutufundisha na kutujuza tulikotoka. Tunaweza kutumia matukio yaliyopita (historia) ili kutuelekeza yatupasayo kufanya sasa.

Tanzania ni sehemu muhimu ya dunia hii. Haiwezi kujitenga na historia ya dunia ya kale, ya juzi na ya sasa.

CCM ni chama kinachotawala Tanzania tangu Uhuru wa Tanganyika 1961 na tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Hawa watu wanachojua wao ni hiki kitu kimoja tu kwa sasa.

Kwa kuwa TUNAKULA na KUNYWA na KUSHIBA, nani awezaye kuwa juu yetu?

Kunywa, kula na kushiba hadi kusaza kumeshawalevya. Hawaioni hatari iliyoko mbele yao. Hawauoni mwisho wao unaowatazama kwa macho makali.

Dunia ya kale ya kina Luthu, Nuhu, Nebukadneza, Dario, Alexabder The Great (Roman Empire).

Na the Latest ni dunia ya kina Adolf Hitler, Benito Mussolini, Iddi Amin Dada, Daniel Arap Moi (KANU) Kenya, Kenneth Kaunda (UNIP) Zambia and so forth inaweza kuwapa somo nzuri CCM, watawala wa sasa katika Tanzania yetu.

Kula na kunywa na kushiba na kisha kulewa, kumepumbaza na kuua fikra za ufahamu zao.

Kula na kunywa kunapumbaza kiasi cha kila sauti inayosikika kuwa ni upuuzi.

Hata Roman empire iliyooanguka kwa kishindo kikuu, walikuwa kama ninyi. Walikuwa wakila na kunywa huku mauti ikiwanyemelea kimya kimya.

Hawakujali sauti yoyote ya kukosoa wala ya maonyo kwa sababu walisema, "sauti za chura kwenye dimbwi la maji hazimzuii ng'ombe kunywa maji hayo"

Walikuwa wakila na kunywa na kulewa ,na mwisho wao ulivyowakuta bila taarifa ktk starehe zao.

Hata hivyo, ni bora mwisho huo wa CCM ukaja haraka na mapema. Na huo unakuja!
wakivimbiwa tu wanajiona mjini wameshamaliza kila kiti yaani
 
CCM itaachia madaraka kwa amri kutoka kwa wahisani hasa Benki ya Dunia kama tulivyolazimishwa vyama vingi!!Mimi nawashauri waandae vyama mbadala vilivyokomaa na kukua ili wafanye Demokrasia ya kutengeneza kuliko ya kulazimishwa na Raia au vikundi vya kigaidi vitakavyomilikiwa na mataifa tajiri Duniani kama Marekani n.k!!!
 
Back
Top Bottom