Nimetoa mada "Rais Samia Suluhu Hassan, alama ya mwisho ya anguko la utawala wa siasa za CCM Tanzania"
Wengi hawajanielewa na kusema it's a delusional.
Dunia hii ina historia pevu sana inayoweza kutufundisha na kutujuza tulikotoka. Tunaweza kutumia matukio yaliyopita (historia) ili kutuelekeza yatupasayo kufanya sasa.
Tanzania ni sehemu muhimu ya dunia hii. Haiwezi kujitenga na historia ya dunia ya kale, ya juzi na ya sasa.
CCM ni chama kinachotawala Tanzania tangu Uhuru wa Tanganyika 1961 na tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Hawa watu wanachojua wao ni hiki kitu kimoja tu kwa sasa.
Kwa kuwa TUNAKULA na KUNYWA na KUSHIBA, nani awezaye kuwa juu yetu?
Kunywa, kula na kushiba hadi kusaza kumeshawalevya. Hawaioni hatari iliyoko mbele yao. Hawauoni mwisho wao unaowatazama kwa macho makali.
Dunia ya kale ya kina Luthu, Nuhu, Nebukadneza, Dario, Alexabder The Great (Roman Empire).
Na the Latest ni dunia ya kina Adolf Hitler, Benito Mussolini, Iddi Amin Dada, Daniel Arap Moi (KANU) Kenya, Kenneth Kaunda (UNIP) Zambia and so forth inaweza kuwapa somo nzuri CCM, watawala wa sasa katika Tanzania yetu.
Kula na kunywa na kushiba na kisha kulewa, kumepumbaza na kuua fikra za ufahamu zao.
Kula na kunywa kunapumbaza kiasi cha kila sauti inayosikika kuwa ni upuuzi.
Hata Roman empire iliyooanguka kwa kishindo kikuu, walikuwa kama ninyi. Walikuwa wakila na kunywa huku mauti ikiwanyemelea kimya kimya.
Hawakujali sauti yoyote ya kukosoa wala ya maonyo kwa sababu walisema, "sauti za chura kwenye dimbwi la maji hazimzuii ng'ombe kunywa maji hayo"
Walikuwa wakila na kunywa na kulewa ,na mwisho wao ulivyowakuta bila taarifa ktk starehe zao.
Hata hivyo, ni bora mwisho huo wa CCM ukaja haraka na mapema. Na huo unakuja!