CCM msipumbazike na kula, kunywa na kushiba hata mkalewa msioone hatari iliyoko mbele yenu

CCM msipumbazike na kula, kunywa na kushiba hata mkalewa msioone hatari iliyoko mbele yenu

Nimetoa mada "Rais Samia Suluhu Hassan, alama ya mwisho ya anguko la utawala wa siasa za CCM Tanzania"

Wengi hawajanielewa na kusema it's a delusional.

Dunia hii ina historia pevu sana inayoweza kutufundisha na kutujuza tulikotoka. Tunaweza kutumia matukio yaliyopita (historia) ili kutuelekeza yatupasayo kufanya sasa.

Tanzania ni sehemu muhimu ya dunia hii. Haiwezi kujitenga na historia ya dunia ya kale, ya juzi na ya sasa.

CCM ni chama kinachotawala Tanzania tangu Uhuru wa Tanganyika 1961 na tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Hawa watu wanachojua wao ni hiki kitu kimoja tu kwa sasa.

Kwa kuwa TUNAKULA na KUNYWA na KUSHIBA, nani awezaye kuwa juu yetu?

Kunywa, kula na kushiba hadi kusaza kumeshawalevya. Hawaioni hatari iliyoko mbele yao. Hawauoni mwisho wao unaowatazama kwa macho makali.

Dunia ya kale ya kina Luthu, Nuhu, Nebukadneza, Dario, Alexabder The Great (Roman Empire).

Na the Latest ni dunia ya kina Adolf Hitler, Benito Mussolini, Iddi Amin Dada, Daniel Arap Moi (KANU) Kenya, Kenneth Kaunda (UNIP) Zambia and so forth inaweza kuwapa somo nzuri CCM, watawala wa sasa katika Tanzania yetu.

Kula na kunywa na kushiba na kisha kulewa, kumepumbaza na kuua fikra za ufahamu zao.

Kula na kunywa kunapumbaza kiasi cha kila sauti inayosikika kuwa ni upuuzi.

Hata Roman empire iliyooanguka kwa kishindo kikuu, walikuwa kama ninyi. Walikuwa wakila na kunywa huku mauti ikiwanyemelea kimya kimya.

Hawakujali sauti yoyote ya kukosoa wala ya maonyo kwa sababu walisema, "sauti za chura kwenye dimbwi la maji hazimzuii ng'ombe kunywa maji hayo"

Walikuwa wakila na kunywa na kulewa ,na mwisho wao ulivyowakuta bila taarifa ktk starehe zao.

Hata hivyo, ni bora mwisho huo wa CCM ukaja haraka na mapema. Na huo unakuja!
Eeeee BWANA, huo mwisho na uje, Na uje BWANA, Amen
 
Umekua nani wewe uanze kutengua maandiko!? Au unataka kumwambia Mungu hiyo serikali unayoichukia ipo madarakani sababu yeye alishindwa kuizuia isiwepo??

Umeambiwa..... "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu."

Wewe umeshaambiwa TII ni KUTII tuu bila shurti😆😆
Kwa hiyo kulifanyika makosa kupinga serikali ya Idi Amin, Uganda, na ya makaburu wa Africa Kusini? Na vipi serikali za wakoloni waliotutawala, tulifanya makosa kuwatimua?
 
Siku yetu ikija hatuna shida..... tutaendelea kutii mamlaka bila shurti

Maana tumeambiwa..... "Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu."
Acha ujinga. Hivi kwa mfano kina Kigwa, Majaliwa nao wamewekwa na Mungu?
 
Acha kupotosha hoja! Sijamkataa Rais Samia, bali tatizo langu lipo kwenye uhalali wa ushindi uliowezesha CCM kuunda serikali , hapa ndipo msingi wa uhalali au uatili wa serikali!

Hivi hamjiulizi Inakuaje mnashindwa kupata suluhu ya mnachokiita tatizo kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
Hivi nyie mko sawa kweli!? Sioni kama mnaweza kutatua hata kero moja ya wananchi... Maana naona mnademka na kulialia kama toto tuu
 
Acha ujinga. Hivi kwa mfano kina Kigwa, Majaliwa nao wamewekwa na Mungu?
Kabla sijakujibu jiulize kwanini wewe unastahili sanaaaaa hukuwekwa pale kwa majaliwa 🤣🤣🤣🤣
 
Kwa hiyo kulifanyika makosa kupinga serikali ya Idi Amin, Uganda, na ya makaburu wa Africa Kusini? Na vipi serikali za wakoloni waliotutawala, tulifanya makosa kuwatimua?

Jifunze kanuni za kulinganisha vitu, huwezi kufananisha vitu visivyofanana
 
CCM ndio chama kilichofanikisha mafanikio na maendeleo yote tuliyonayo kiuchumi, kisiasa na hata kijamii

Pamoja na mapungufu yaliyopo CCM imejenga msingi imara sana wa Taifa hili. Imejenga msingi wa umoja, upendo, amani kwa njia ambayo ni ngumu sana kwa nchi nyingine.

Miaka 60 ya uhuru Tanzania hakuna ugomvi wala vita ya wenyewe kwa wenyewe kwenye udini wala ukabila, na wala kwa jinsia; kwa maana hiyo kwa yoyote mwenye nia ya kulisambaratisha taifa letu njia yoyote ni ngumu sana.

Tunapokua tunawakosoa tusisahau kwamba hata huu uwezo wa kukosoa wametujengea wao
Hakika hakika!
 
Kabla sijakujibu jiulize kwanini wewe unastahili sanaaaaa hukuwekwa pale kwa majaliwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwa sababu shetani aliona sitaweza mtii!!
 
Nimetoa mada "Rais Samia Suluhu Hassan, alama ya mwisho ya anguko la utawala wa siasa za CCM Tanzania...."

Wengi hawajanielewa na kusema it's a delusional....

Dunia hii ina historia pevu sana inayoweza kutufundisha na kutujuza tulikotoka. Tunaweza kutumia matukio yaliyopita (historia) ili kutuelekeza yatupasayo kufanya sasa.....

Tanzania ni sehemu muhimu ya dunia hii. Haiwezi kujitenga na historia ya dunia ya kale, ya Jana, ya juzi na ya sasa....

CCM ni chama kinachotawala Tanzania tangu Uhuru wa Tanganyika 1961 na tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964....

Hawa watu mpaka sasa wanachojua wao ni kitu kimoja tu kwa sasa....

"....Kwa kuwa TUNAKULA na KUNYWA na KUSHIBA hadi kusaza, basi ni nani awezaye kuwa juu yetu....?"

Kunywa, kula na kushiba hadi kusaza kumeshawalevya. Hawaioni hatari iliyoko mbele yao. Hawauoni mwisho wao unaowatazama kwa macho makali na angavu....

Dunia ya kale ya kina Luthu, Nuhu, Nebukadneza, Dario, Alexabder The Great (Roman Empire) inaweza kutupa somo zuri sana....

Na the Latest ni dunia ya kina Adolf Hitler, Benito Mussolini, Iddi Amin Dada, Daniel Arap Moi (KANU) Kenya, Kenneth Kaunda (UNIP) Zambia and so forth inaweza kuwapa somo nzuri CCM, watawala wa sasa katika Tanzania yetu....

Lakini ni heri yetu kwa kuwa kula na kunywa na kushiba na na kusaza na kisha kulewa, kumewapumbaza na kuua fikra za ufahamu zao....

Kula na kunywa kumewapumbaza kiasi cha kila sauti inayosikika masikio mwao inaonekana kuwa ni upuuzi na kelele zisizo na maana....

Wamejisahau na kutojua kuwa wamepewa dhamana na Mungu muumba kutawala watu wake kwa HAKI....

Hata Roman empire iliyooanguka kwa kishindo kikuu, walikuwa kama walivyo watawala hawa wa Leo...

Walikuwa wakila na kunywa huku mauti na anguko la dola yao kuu iliyotawala ulimwengu wote liliwanyemelea kimya kimya bila wao kujua....

Hawakujali sauti yoyote ya kukosoa wala ya maonyo kwa sababu walisema, "sauti za chura kwenye dimbwi la maji hazimzuii ng'ombe kunywa maji hayo....."

Walikuwa wakila na kunywa na kulewa ,na mwisho wao uliwakuta bila taarifa ktk starehe zao na mpaka leo hawaelewi nini kilitokea....

Hata hivyo, ni bora mwisho huo wa CCM ukaja haraka na mapema. Na huo unakuja. Nasi tunasema na uje sasa...AMEN.
Mungu amewaonjesha kidogo mwezi march
 
Upinzani ulipofeli 2015 tu!! Sjui tena itachukua miongo mingapi
Upinzani haukufeli. Ni dhulma ya kutumia tume na jeshi ndugu yangu ndo mana Mungu aliingilia kati march hii.
 
CCM ndio chama kilichofanikisha mafanikio na maendeleo yote tuliyonayo kiuchumi, kisiasa na hata kijamii

Pamoja na mapungufu yaliyopo CCM imejenga msingi imara sana wa Taifa hili. Imejenga msingi wa umoja, upendo, amani kwa njia ambayo ni ngumu sana kwa nchi nyingine.

Miaka 60 ya uhuru Tanzania hakuna ugomvi wala vita ya wenyewe kwa wenyewe kwenye udini wala ukabila, na wala kwa jinsia; kwa maana hiyo kwa yoyote mwenye nia ya kulisambaratisha taifa letu njia yoyote ni ngumu sana.

Tunapokua tunawakosoa tusisahau kwamba hata huu uwezo wa kukosoa wametujengea wao
Tanzania hata kabla ya Uhuru ilikuwa na umoja, hakuna vita. Tusidanganyane. Ccm ndo inachokoza wananchi ili wapigane
 
Upinzani haukufeli. Ni dhulma ya kutumia tume na jeshi ndugu yangu ndo mana Mungu aliingilia kati march hii.
Unawaza kifupi sana mkuu

Unashindwa kabisa kuelewa kwamba hata mtoto mchanga huzaliwa tu na kufariki na au huzaliwa tayari akiwa kesha kufa, sembuse na mtu mzima, ni nani atakayebaki hai milele?

Yule unayesema Mungu aliingilia kati, sio sahihi, bali wakati wake ulifika, na mimi na wewe wakati wetu ukifika, hata tukutwe ndo kwaanza tumeajiliwa na mwezi bado haujafika, tutaondoka tu
 
Warumi 13: 1-7​

Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.

Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu.

Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.

Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu.

Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala.

Walipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.
Unaekezea isivyo. Mungu haweki serikali madarakani bali ameruhusu ziwepo. Serikali dhalimu ni nyingi duniani, huwezi muhusisha Mungu mtakatifu na udhalimu.
Andiko hilo litafakari vizuri.Watawala hupenda kutafsiri hivyo ili waonekane kuwa wamewekwa na Mungu kumbe isivyo.
 
Upinzani haukufeli. Ni dhulma ya kutumia tume na jeshi ndugu yangu ndo mana Mungu aliingilia kati march hii.
Unawaza kifupi sana mkuu

Unashindwa kabisa kuelewa kwamba hata mtoto mchanga huzaliwa tu na kufariki na au huzaliwa tayari akiwa kesha kufa, sembuse na mtu mzima, ni nani atakayebaki hai milele?

Yule unayesema Mungu aliingilia kati, sio sahihi, bali wakati wake ulifika, na mimi na wewe wakati wetu ukifika, hata tukutwe ndo kwaanza tumeajiliwa na mwezi bado haujafika, tutaondoka tu
 
Hakuna hatari YEYOTE....

CCM ni Kama BAHARI.....huwa inapitia vipindi vyote.....

1)"Kuchinjwa" kwa mh.Jakaya Kikwete na hayati Ben Mkapa baada ya lile duru la pili la uchaguzi(vijana wengi tumeisoma tu historia hiyo)....CCM ILIPITA KIPINDI HICHO......

2)Kuchinjwa kwa mmoja wa BOYZ TWO MEN na mwenzake....swahiba yake uchaguzi wa ndani 2015 na mh.Lowassa kuhamishia MAFURIKO CHADEMA.....CCM ilitikisa na IKABAKI SALAMA......

CCM.....CCM.....CCM.....CCM....

Chama hiki BORA barani AFRIKA kamwe hakitakuja kuondolewa MADARAKANI na vichwa vyepesi kama MBOWE ,TUNDU LISSU NA ZITTO KABWE......

Siempre CCM..... Siempreeeeeeee

#VijanaImaraJeuriYaChama
#CCMHoooyeee

#KaziInaendelea
#DieHardFanOfCCM
 
Unawaza kifupi sana mkuu

Unashindwa kabisa kuelewa kwamba hata mtoto mchanga huzaliwa tu na kufariki na au huzaliwa tayari akiwa kesha kufa, sembuse na mtu mzima, ni nani atakayebaki hai milele?

Yule unayesema Mungu aliingilia kati, sio sahihi, bali wakati wake ulifika, na mimi na wewe wakati wetu ukifika, hata tukutwe ndo kwaanza tumeajiliwa na mwezi bado haujafika, tutaondoka tu
Mungu uwaondoa waovu kwa ajili ya Jina lake.
Kunawatawala wengi waovu waliondolewa kama hivi. Soma vizuri neno lake.
 
Wenye maoni kama yako walikuako na wapo tangu enzi za mitume

Wenzio wa aina yako walimkataa Mtume Mohamad na Yesu sembuse wewe kumkataa rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake
Hivi unajua maana ya kumkataa Yesu?
Yesu alitaka awe nani kwa nani? Nani walio mkataa.
Usichanganye mambo usiyo yajua. Eti kumkataa Polepole ni sawa na kumkataa Yesu, kweli?
 
Back
Top Bottom