CCM msipumbazike na kula, kunywa na kushiba hata mkalewa msioone hatari iliyoko mbele yenu

Upinzani ulipofeli 2015 tu!! Sjui tena itachukua miongo mingapi
Upinzani si vyama vya si-hasa.... Upinzani ni watu, maisha halisi ya watu je wameridhika nayo? Kila kukicha wanaendelea kuerevuka hivyo ipo siku wataiva na kuamua kujikwamua kutoka ktk minyororo ya hao wanaokula na kusaza ilhali wananchi maisha duni.... HISTORIA NI MWALOMU MZURI
 
Good points. Kuongoza nchi si kazi ndogo. Umoja naweza kukubali, ila upendo na amani tulikuwa nao kabla hata ya uhuru. Dini tofauti zilikuwepo kabla ya uhuru na kulikuwa hakuna vita vya kidini.
 

Maneno meeeengi

Jibu swali.... Wewe nani amekuambia serikali ya Tanzania haijatoka kwa Mungu
 
Mkuu una hekima sana na MUNGU akubariki,ila Bahati mbaya umetoa ushauri kwa mapepo,CCM ni kizazi cha nyoka,Tarajia matusi tu kutoka kwa haya Mataga yaliyolaaniwa na Mungu

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Matendo ya Mitume 5
29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
 
Mama D umeingia mtegoni,umeshindwa kutofautisha CCM na Taifa la Tanzania.
 
Mama D umeingia mtegoni,umeshindwa kutofautisha CCM na Taifa la Tanzania.

Mtego gani?

Serikali ya Tanzania ni ya Chama gani cha siasa?

Au unataka tuanze kuhubiri hapa ndio utaelewa☺☺☺
 
Akichukua mke wako, kwa madaraka yake tumwachie, aliwalala watoto wako unamwacha, sababu ni mtumishi wa Mungu. Ninavyojua hilo neno linasehem yake, sii hapa tunahitaji katiba mpya yenye mawazo ya kila mwananchi, kuendelea kutumia katiba hii nikuishi kwa kufuata misingi ya kikoloni bila wakoloni.
 

Akichukua mke wako unamwacha Mungu aseme nae kama alivyosema na Abimeleki kwa Sara MWANZO 20.

Mradi uhakikishe kabla hujamhukumu mwenzio wewe uko safi
 
Shida waganga njaa wana ID hata kumi humu,ukiandika mambo ya maana unashangaa unaanza kupingwa na members,kumbe mtu mmoja mwenye Nia ovu.
Mungu akutie nguvu kuisema kweli Kama unavyoongozwa na Roho mtakatifu wasije sema hawakujua.
 
mkuu bado hoja zako ni za kufikirika sana. Umesema CCM imetawala toka 1961 tulipo pata uhuru ni sawa. Leo ni kama miaka 60 imepita na upinzani bado haujashika hatamu.
hivi inawezekanaje kwa kipindi chote cha miaka 60 upinzani(japo rasmi ulianza1992) bado haujawa na ushawishi wa kutosha mbele ya wananchi? Hapa usizungumzie katiba mpya kwa sababu mageuzi yanaweza kufanyika hata bila katiba mpya cha msingi tu muwe na nguvu ya umma nyuma yenu. Nguvu ya umma haijawahi kushindwa na wala haitaweza kushindwa bila kujali katiba iliyopo inaupungufu ama la.
Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba upinzani wa nchi hii bado haujawa na nguvu kubwa kuweza kuungwa mkono na walio wengi.
 
Mkuu tafadhari tuache kutumia isivyo halali maadiko matakatifu kuhalalisha uovu & dhuluma!
 
Mkuu tafadhari tuache kutumia isivyo halali maadiko matakatifu kuhalalisha uovu & dhuluma!

Wewe mwenyewe kwanza unatakiwa utuambie una mamlaka gani ya kuondoa uhalali wa hayo maandiko😅😅😅
 
Wewe mwenyewe kwanza unatakiwa utuambie una mamlaka gani ya kuondoa uhalali wa hayo maandiko😅😅😅
Suala la kuwa halali au kutokuwa halali kwa serikali yoyote iliyoko madarakai hutegemea nama ilivyojiweka au kuwekwa madarakai! Pia katika ilia tuafundishwa kuwa Mungu amempa mwanadamu akili, uhuru na utashi, Hivyo mwansdamu mweyewe ndiye hutenda akiwa amepewa uhuru na Mungu , ila matumizi mabaya ya uhuru huo kama vile wizi wa kura wa kutisha uliofanywa na CCM katika uchaguzi mkuu uliopita ndiyo msingi wa dhambi na ubatili vinapoanzia! Hivyo si sahihi kusema kila kilichopo kimewekwa na Mungu kwasababu tu maandiko matakatifu yamesema hivyo!
 

Wenye maoni kama yako walikuako na wapo tangu enzi za mitume

Wenzio wa aina yako walimkataa Mtume Mohamad na Yesu sembuse wewe kumkataa rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake
 
Wenye maoni kama yako walikuako na wapo tangu enzi za mitume

Wenzio wa aina yako walimkataa Mtume Mohamad na Yesu sembuse wewe kumkataa rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake
Acha kupotosha hoja! Sijamkataa Rais Samia, bali tatizo langu lipo kwenye uhalali wa ushindi uliowezesha CCM kuunda serikali , hapa ndipo msingi wa uhalali au uatili wa serikali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…