Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
"Msituletee" wewe na nani,mbona mimi nilimpenda?Aina ya uongozi kama ule wa Awamu ya Tano ulikuwa balaa kwa mustakabali wa umoja wa nchi yetu.
Sina haja ya kurudia madhambi mabaya ya Awamu ya Tano maana kila mtu yalimgusa.
Kiini cha hayo matatizo ni kinyang'anyiro cha urais wa 2015 ambapo walijitokeza wagombea zaidi ya 40.
Naona hili linajirudia mbio za Uspika.
CCM waliboronga vibaya mwaka 2015, na matokeo tuliyaona.
Sasa hivi CCM iwe makini na waache umavikundi, mitandao, na "gangs" za kimasilahi binafsi.