Uchaguzi 2020 CCM mwaka huu kubalini kuwa Wananchi wamewakataa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Mmelazimisha sana ushindi, kupelekea Mawaziri waandamizi kupita bila kupingwa kwenye majimbo yao. Madiwani wengi wamepata bila kupingwa. Unapomshinda mpinzani wako kwa 90% ni dalili ya kuwa mashindano yalikuwa na matatizo. Kuna kila dalili ya kuwa mshindani mmoja alitumia nguvu na mabavu kuupata ushindi.

Kampeni zenu mpaka mtumie gharama kubwa ya wasanii, watoto wa shule, watu kupewa 5,000, Kofia na T-shirts ndiyo waende kwenye mikutano. Hizi nguvu mnazotumia ni nyingi mno.

Kwenye sanduku la kura mnatumia vyombo vya dola kuchakachua ushindi. Utawala wenu ni wa kibabe, mnasema hadharani kuwa tusipochagua wabunge wa CCM hamleti maendeleo. CCM tumewachoka ondokeni madarakani.

Tundu Lissu ametutoka hofu. Ametuambia maandamano ndiyo sauti pekee tuliyonayo kama sanduku la kura litachakachuliwa. Hao wanajeshi na polisi ni Watanzania wenzetu hawsepipe kutuma wote. Wengine ni watoto wa dada na kaka zetu, majirani zetu.nk

Afadhali muondoke madarakani mkiwa na heshima kidogo mliyonayo kuliko kuvuliwa heshima yote iliyobaki.
 
kilichobaki kwa ccm ni kututisha kwa mabomu ya machozi. wapinzani tukiondoa hofu ya mabomu ya machozi ccm itabaki katika historia ya nchi hii.
Ni Kheri kufa kishujaa kama kifo chako kitaleta amani na furaha kwa kizazi kijacho.
 
CCM mpya hawakujua kula na vipofu. kwa miaka mingi hatukujali mambo ya ccm sababu tuliishi kwa amani na furaha. CCM ya magufuli inatawala watu kwa kuwajaza hofu.

uchaguzi wa mwaka huu ccm inakataliwa kwa nguvu kubwa sababu watu wamechoka kuishi kwa hofu. CCM ijiandae kukabidhi nchi kwa amani ama iondolewe kwa nguvu ya umma.
 
ccm mpya hawakujua kula na vipofu. kwa miaka mingi hatukujali mambo ya ccm sababu tuliishi kwa amani na furaha. ccm ya magufuli inatawala watu kwa kuwajaza hofu...
Kushindwa kufanya kazi na wabunge wa upinzani ili kuwapelekea maendeleo wananchi ni dalili ya mapungufu makubwa katika uongozi.
 
wachague wakabidhi nchi kwa amani wajipange upya ama waondolewe kwa nguvu ya umma wafutike kabisa.
 
wachague wakabidhi nchi kwa amani wajipange upya ama waondolewe kwa nguvu ya umma wafutike kabisa.
Watu wana hasira, huo ushindi mnaopanga kwa Magufuli utazidisha hasira za wananchi.
 
CCM Mpya wakubali yaishe 2020 wasilazimishe, chama kongwe kiwe chama cha upinzani .

Tundu Lissu akisalimia mjini Moshi jioni hii

 
30 September 2020

Kampeni za leo CHADEMA : URAIS 2020, UBUNGE NA UDIWANI Kilimanjaro 2020

Chama cha CHADEMA leo waliendesha kampeni za uchaguzi Mkuu katika wilaya kadhaa mkoani Kilimanjaro, hali ilikuwa hivi katika maeneo Siha, Marangu, Rombo Mkuu n.k:

Source : swahili villa
 
Msituhadae sisi wananchi bado tunakipenda sana chama chetu cha CCM. Chama kilichotulea hadi tumekua na kuoa, na wewe mleta mada hadi umeolewa Ulaya na Beberu mmoja mweupe.

Raisi wetu anawapenda sana wananchi wake. Hadi akawanunulia Drimlinner kumi na moja ili waachane na kupanda madaladala kila siku.
Lisu ni Kibaraka tu wa Mabeberu.
 
Waliopita bila kupingwa wajiandae maana Rais ajaye kasema hakuna kiongozi wa kuchaguliwa atakayehesabiwa kuwa kiongozi pasipo kupigwa kura
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala,safari hii tunasema hapana kwa magaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…