Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mmelazimisha sana ushindi, kupelekea Mawaziri waandamizi kupita bila kupingwa kwenye majimbo yao. Madiwani wengi wamepata bila kupingwa. Unapomshinda mpinzani wako kwa 90% ni dalili ya kuwa mashindano yalikuwa na matatizo. Kuna kila dalili ya kuwa mshindani mmoja alitumia nguvu na mabavu kuupata ushindi.
Kampeni zenu mpaka mtumie gharama kubwa ya wasanii, watoto wa shule, watu kupewa 5,000, Kofia na T-shirts ndiyo waende kwenye mikutano. Hizi nguvu mnazotumia ni nyingi mno.
Kwenye sanduku la kura mnatumia vyombo vya dola kuchakachua ushindi. Utawala wenu ni wa kibabe, mnasema hadharani kuwa tusipochagua wabunge wa CCM hamleti maendeleo. CCM tumewachoka ondokeni madarakani.
Tundu Lissu ametutoka hofu. Ametuambia maandamano ndiyo sauti pekee tuliyonayo kama sanduku la kura litachakachuliwa. Hao wanajeshi na polisi ni Watanzania wenzetu hawsepipe kutuma wote. Wengine ni watoto wa dada na kaka zetu, majirani zetu.nk
Afadhali muondoke madarakani mkiwa na heshima kidogo mliyonayo kuliko kuvuliwa heshima yote iliyobaki.