CCM na Serikali jibuni hoja za Humphrey Polepole, msimzime kidola

Neno term kwenye katiba lina maana ya kipindi au vipindi. Kila rais aweza kuwa na terms 2 au vipindi viwili na si zaidi. neno term halikumaanisha awamu kama uavotaka kutuaminisha hapa. Habari ya kazi iendelee ni kaslogan tu ambako hakana maana yoyote kakisemwa au kasiposemwa
 
Kwani kuna mtu amesema Samia siyo Rais halali?

Halafu suala la awamu na mihula ya kila awamu lipo kwenye Civics form one.

Shida mna shule ndogo sana vijana, njaa zitawaua.

Uhuni siyo deal. #kataawahuni
 
Kwani kuna mtu amesema Samia siyo Rais halali?

Halafu suala la awamu na mihula ya kila awamu lipo kwenye Civics form one.

Shida mna shule ndogo sana vijana, njaa zitawaua.

Uhuni siyo deal. #kataawahuni
civics form one ndio katiba ya JMT inayoelekeza mamba haya ya msingi? marais wanaongozwa na civics form one?
 
Huyo rais samia anapojitambulisha kama rais wa awamu ya Sita,iyo tafsiri ya awamu ameitoa wapi?
kajisikia tu kuiitwa awamu ya sita ambayo hakatazwi na wala hajatukana. kusema kasi mpya nguvu mpya au hapa kazi tu au kazi iendelee au awamu ya nne ni maneno anayoweza kuyatumia yeyote ikiwemo rais aliya madarakani kuhamasisha utendaji wa serikali anayoongoza hakuna kanuni maalum kwenye hili
 
Na tunapenda iwe hivyo, amalizie hii minne, halafu aanze 10 ya kwake kisha atamalizia na mitano ya shukrani.
Kweli akili za celebrity forum haziwezi kufit sehemu zote.

Ni vizuri mkawa mnasubiria hoja mserereko mlizozoea kabla ya kuandika mada zilizowapita uwezo kiakili.
 
Nilishawahi kusema kuwa ndani ya CCM huwa wanaupinzani wa asili. Ukiona upinzani unang'ra nje ya CCM ujue watu waliomo ndani wanafanana na wananufaika kwa kadri ya fursa wanayopata. Upinzani uliomo humo unasababishwa na vita dhidi ya haki,ufisadi, kiburi, kujiona bora, dharau, fursa za dhuluma ya kumiliki mali na mamlaka hicho ndicho kinachoendelea kwa sasa na hapo huenda tukapoteza mtu wa mhimu kwenye taifa kutokana na vita zao zisizozingatia maslahi ya wananchi na taifa.
 
Sikuwa najua kuwa nchi inaongozwa kwa kujisikia tu, mpaka leo niliposoma hii hoja yako😅.
 
Sikuwa najua kuwa nchi inaongozwa kwa kujisikia tu, mpaka leo niliposoma hii hoja yako😅.
of course kila jambo analolifanya mtu ni kwa kujisikia kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zilizopo kwenye taifa au kwa lugha iliyozoeleka ni kwa kuamua kwa utaratibu huo huo. mtu anaweza kujisikia kufanya lolote ili mradi havunji sheria na katiba ya JMT
 
Nimemsikiliza Polepole mara kadhaa,anazo hoja zenye mashiko.
Tunatakiwa kushambulia hoja na sio mtu.Hoja za Polepole ni wanasiasa wachache sana wanaweza kuzijibu.Polepole anajua kujenga hoja.Nape anaongea mipasho,vijembe,mijisifu na kuzomea, hakuna cha zaidi.Tofauti ya Polepole na Nape kisiasa,ni sawa kuifananisha mbingu na ardhi! Polepole (mbingu),Nape(Ardhi).
CDM acheni kuingilia maugomvi ya CCM yatawaondoa kwenye ramani .
Endeleeni kukijenga chama,kuandikisha wanachama kidigitali na kupaza sauti nchini na duniani kote kuhusu uonevu anaofanyiwa Mwenyekiti pamoja na wanachama wengine waliowekwa korokoroni!
 

Wewe jamaa utakuwa umechanganyikiwa nakuhakikishia haiwezekani kuwa na mfumo huo
Labfa ndio huu utumbo uliokoment.
Haiwezekani kusema kuna mfumo mtu unafanya kazi kwa kujisikia huku ukifuata sheria,kanuni na taratibu.
Ukishasema sheria,kanuni na taratibu hapo suala la kujisikia halipo
 
ni kwa sababu tu akili yako imekukatalia kukubali kuwa pale unapoinua mkono wako kufanya jambo ni kuwa umefanya maamuzi ya kufanya hilo jambo ukijua matokeo yake na ndio kujisikia huko. akili nyepesi zenye kutenda kwa haziwezi kuconceptualize mambo kama haya. we sema tu kuwa nimechanganyikiwa kwa sababu hivyo ndivyo unavyojisikia
 
Kutakuwaje na Sheria na kanuni Kisha mtu afanye kwa namna anavyojisikia? Vipi asipojisikia kufanya kitu fulani ilihali sheria inamtaka?

Acheni kuleta hoja mlendamlenda kama mmekatwa vichwa.
 
Chochea kuni .
 
Kutakuwaje na Sheria na kanuni Kisha mtu afanye kwa namna anavyojisikia? Vipi asipojisikia kufanya kitu fulani ilihali sheria inamtaka?

Acheni kuleta hoja mlendamlenda kama mmekatwa vichwa.
ndo maana nakwambia kichwa chako kibovu kinakukatalia tu hili jambo. je akijisikia kutenda kulingana na sheria? au je akijisikia kutenda kinyume na sheria? kwani kote si huwa kuna matokeo yake. we hujawahi kusikia rais wa chad alimuondoa CAG wake kwa kujisikia tu. we hujawahi kusikia kuwa rais wa JMT aweza kujisikia kuwaachilia au kutowaachilia wafungwa wenye sifa fulani hata kama wana sifa fulani fulani za kusamehewa vifungo. hujawahi kusikia rais akijisikia anaweza kumteua mtu anayemtaka kuwa mbunge wa bunge wa JMT. akili yako yaonekana imefungwa ndani ya boxi ambalo limeshaachwa wazi lakini hujui ufanye nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…