KERO CCM na Serikali yake wameharibu sana Miji ya Tanzania, na imebakia kuwa magulio, miji imejaa Frame hadi kwenye makazi ya watu. Miji ni michafu sana

KERO CCM na Serikali yake wameharibu sana Miji ya Tanzania, na imebakia kuwa magulio, miji imejaa Frame hadi kwenye makazi ya watu. Miji ni michafu sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Yaani hizo frame, masoko, magulio yoote yanamilikiwa na Wana CCM!
Chadema acheni uvivu.
Duniani kote kuna mipango miji na inafuatwa bila siasa, wajinga nyie Tanzania inafuata mipango miji? hao CCM si ndio wanaharibu?
 
Tembelea dar sasa ndo utalia. Barabara za mitaani ni mbovu takataka hazichukuliwi na manispaa kwa wakati, kazi kuwapa m700 Taifa stars tu!
Miji imaharibiwa sana ni michafu sana miji ya Tanzania ni michafu haswa.
 
Gentleman,
it's very simple to interpret that,

ukiona frame za maduka hadi kwenye makazi ya watu, lakini pia ukiona
magulio na minada kila mahali nchini na katika kila mji na kijiji Tanzanian,

Fahamu na kuelewa kwamba hicho ni kielelezo cha hakika, kwamba biashara imekua nchini, na ni uthibitisho kwamba nchi imefunguka kiuchumi, fursa na ajira katika biashara imeongezeka mara dufu, na hivyo uchumi wa nchi unakua, huku kichocheo kikuu ikiwa ni mazingira bora na usalama wa uhakika.

na kwasasabu hiyo hali ya maisha na vipato vya waTanzania inakua bora zaid 🐒
Huwexi kuweka biashara kwenyenjia za waendao kwa migui au kuziba barabara ya magari wala kujenga gulio eneo la wazi la kuchezea watoto.
Ishia kwa kusema hakuna mpango mji
 
Hii kitu inakera hadi basi. Lkn ngoja nikiibgia madarakani nahakikisha tutabomoa. No mercy.
Hatuwezi kuwa na magodwon kwenye makazi ,viwanda uchwara, wachuuzi na boda every where, maeneo yatengwe na kuheshimiwa.
Nawahakikishia sitataka kupendwa kabisa waliouziwa viwanja vilivyotengwa watapoteza na waliouza watafungwa kwa kesi ya kusikilizwa siku moja tu na wengine kwa maelekezo. Majeshi yafanya kazi zao kwa weledi hakuna kutisha watu wala uonezi.
Msiseme sikuwaambia.
Vote for Me
Hahaaaa
 
Naishangaa mpaka sasa bado kipo madarakani!

INAWEZEKANA WENGII WA WATANZANIA NI VICHAA NDIO MAANA WANAENDELEA KUKIWEKA MADARAKANI!
 
Huwexi kuweka biashara kwenyenjia za waendao kwa migui au kuziba barabara ya magari wala kujenga gulio eneo la wazi la kuchezea watoto.
Ishia kwa kusema hakuna mpango mji
hiyo ni kasoro na dosari ndogo mno ambayo maeneo mengi imeshatatuliwa na katika maeneo machache yaliyobaki inaendelea kutafutiwa ufumbuzi,

ni muhimu kutambua jitihada kubwa mno za serikali katika kupanua wigo na fursa za kibiashara nchini licha ya changamoto hizo kidogo ambazo zinatatulika.

serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi na kipenzi cha waTanzania wote Dr Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuboresha mazingira mazuri zaid ya kibiashara nchini na kuhakikisha amani, ulinzi na usalama wa watu, mali, biashara na makazi yao unakua wa uhakika zaid 🐒
 
Oops
Utajiri Wa Fremu Tanzania Kuna Shida
 
Unafanya ushabiki kwenye maswala muhimu maeneo ninayoishi hakuna utatuzi zaidi ya kuona hata maeneo surveyed kwa makazi sasa kuna ujenzi wa ma godwon, barabara ndio usiseme.
 
Unafanya ushabiki kwenye maswala muhimu maeneo ninayoishi hakuna utatuzi zaidi ya kuona hata maeneo surveyed kwa makazi sasa kuna ujenzi wa ma godwon, barabara ndio usiseme.
Gentleman,
apriciate basi hata hivyo viashiria vya wazi vya ukuaji wa uchumi nchini, kabla ya kulaumu na kulalamikia mambo ambayo yanahitajika kufanyiwa kazi kwa weledi na umakini wa kiwango cha juu sana.

Ni muhimu sana kua wastahimilivu na wenye subra wakati mambo hayo katika maeneo machache yanafanyiwa kazi na wataalamu wa maeneo husika 🐒
 
Mi naona sio kazi ngumu kupangilia miji bado haijaharibika kwa kiwango cha kutopangika, maeneo ya wazi bado yapo(japo yanauzwa kwa kasi), barabara za waenda kwa miguu zipo ni vile wamachinga wamejimilikisha kwa muda.

Tatizo ni kua ni mtaji wao wa propaganda, wanawekea kiporo wawatengenezee tatizo halafu walitatie huku wakijisifu.
 
Mkuu nakubaliana na wewe ku appreciate kile serkali inafanya , vipo narudia vipo, issue hapa ni ni sahihi huu uchumi unaokuwa kufanywa nje ya mpango mji? mfano machinga wafanyie biashara eneo la kuchezea watoto?
Jambo lingine ni kutetea pasipo kuona kuwa ni tatizo a.k,a ushabiki au uchawa, hii namna hatatufikisha mbali maana tunakuwa wanafiki, lkn pia kuna watendaji hususan ngazi za juu hawawezi kujua kila kitu huku chini kinafanywa na watendaji wa ngazi za huku. Mfano mtu anauziwa eneo surveyed kwa shule au uwanja
 
Yule aliesema waacheni hawa ndio walionichagua
Ukawa ndio muendelezo wa uchafu na mpaka sasa hakuna wa kuwaambia kitu
Haiwezekani tukawa na Taifa linalo ongozwa na siasa na mihemko

Yaani kila kitu mnaona sawa tu
Na kuna watu wanafurahia kelele kwenye mabasi na kuona ni kiburudisho kumbe ni ujinga na ushamba
Unakuta mpaka wauza sabuni wanazunguka kwenye basi hadi basi
Ukilalamika wanasema ndio riziki yao
Sasa kila ujinga tukiutetea hapo tutafanya kila kitu bila nidhamu na mipango miji
Jitu linaamua kupanga mbele ya duka la mtu halafu wakusanya kodi wanampita yeye wanakuja kuhesabiana na mwenye duka
Hakuna nidhamu kabisa
Na hao ndio wamesababisha kwa kuwalea
 
Mi naona sio kazi ngumu kupangilia miji bado haijaharibika kwa kiwango cha kutopangika, maeneo ya wazi bado yapo(japo yanauzwa kwa kasi), barabara za waenda kwa miguu zipo ni vile wamachinga wamejimilikisha kwa muda.

Tatizo ni kua ni mtaji wao wa propaganda, wanawekea kiporo wawatengenezee tatizo halafu walitatie huku wakijisifu.
Yako wapi?
 
Hii kitu inakera hadi basi. Lkn ngoja nikiibgia madarakani nahakikisha tutabomoa. No mercy.
Hatuwezi kuwa na magodwon kwenye makazi ,viwanda uchwara, wachuuzi na boda every where, maeneo yatengwe na kuheshimiwa.
Nawahakikishia sitataka kupendwa kabisa waliouziwa viwanja vilivyotengwa watapoteza na waliouza watafungwa kwa kesi ya kusikilizwa siku moja tu na wengine kwa maelekezo. Majeshi yafanya kazi zao kwa weledi hakuna kutisha watu wala uonezi.
Msiseme sikuwaambia.
Vote for MeeK

Keko eneo la MSD ina.majengo ya viwanda yako wazi kabisa lakini watu wanaenda kuweka mtaani viwanda
 
Shida mkuu ya usimamizi wa sera ambazo zipo, ukiona hivyo ujue kunavuja sehemu
 
Back
Top Bottom