Sijafurahishwa na mfululizo wa kejeli, matusi na majibu dhidi ya Dr. Bashiru mara baada ya yeye kutumia Uhuru wa kikatiba wa kujieleza.
Nafahamu akiwa "mtoto pendwa" awamu ya 5 Dr. Bashiru aliwahi kunena maneno ya makufuru dhidi wa watanzania kwamba "ccm itatumia hata vyombo vya dola ili kusalia madarakani".
Pamoja na makosa yake aliyoyafanya awamu ya 5 hapaswi kuhukumiwa kimakosa. Yatupasa kusahihisha kosa kwa kutenda haki ili ajifunze.
CCM siyo marafiki wa demokrasia. Bado tuna kumbukumbu kuwa Ndugai hadi leo hii anaishi kama digidigi kwasabb tu aliikosoa serikali ya awamu ya 6 kwa kukopa Sana. Na sasa Dr. Bashiru anasakamwa Sana kwa kukosoa wananchi na viongozi wanaosifia na kumshukuru mama kwa kazi/huduma zitolewazo na serikali yake.
Kwa mujibu wa Dr. Bashiru huduma ama kazi hizi zinafanywa kwa kodi zetu hivyo ni haki yetu. Hatupaswi kusema "mama anaupiga mwingi" ama "asante mama". Kosa la Dr. Bashiru hapa ni lipi?