Tatizo la CCM huwezi kuwatetea kimantiki.
Even when they do right, they do right wrongly!
Huyo Ndugai alijiuzulu mwenyewe. Spika wa Bunge ni kiongozi wa muhimili unaojitegemea. Angesimamia anachoona sawa tu, sasa kajiuzulu mwenyewe, au hata kama kashinikizwa, hakutakiwa kujiuzulu kama hajataka.
Hakuna popote katika katiba ya Tanzania ambapo rais anaweza kumuondoa Spika.
Marekani Federal Prosecutor/ US Attorney tu, Preet Bharara, alipigwa mkwala na rais Donald Trump (rais ndiye ana appoint, like Bharara aliteuliwa na Obama). Trump alimwambia Bharara ajiuzulu. Bharara akakataa kujiuzulu, akamwambia Trump ni lazima unifukuze kazi wewe mwenyewe dunia nzima ione umenifukuza kazi, lakini sijiuzulu ng'o, kwa kuwa sina sababu ya kujiuzulu.
Sasa huyo Ndugai kwa nini kakubali kujiuzulu kama aliona ana hoja ya msingi? Yeye kama kiongozi wa bunge kazi yake si kuisimamia serikali? Sasa kwa nini alijiuzulu baada ya kuisimamia serikali kama majukumu ya kazi yake yanavyosema?
Huyo Bashiru katika hoja zote za msingi za madudu yanayofanywa na serikali hii, yeye na usomi wake wote kaona kitu subjective kama watu kushadadia "mama kaupiga mwingi" ndiyo kitu cha msingi? Is this the best criticism he could come up with?