CCM na wanaccm, nini kosa la Bashiru? Demokrasia kwenu ni nongwa?

CCM na wanaccm, nini kosa la Bashiru? Demokrasia kwenu ni nongwa?

Sijafurahishwa na mfululizo wa kejeli, matusi na majibu dhidi ya Dr. Bashiru mara baada ya yeye kutumia Uhuru wa kikatiba wa kujieleza.

Nafahamu akiwa "mtoto pendwa" awamu ya 5 Dr. Bashiru aliwahi kunena maneno ya makufuru dhidi wa watanzania kwamba "ccm itatumia hata vyombo vya dola ili kusalia madarakani".

Pamoja na makosa yake aliyoyafanya awamu ya 5 hapaswi kuhukumiwa kimakosa. Yatupasa kusahihisha kosa kwa kutenda haki ili ajifunze.

CCM siyo marafiki wa demokrasia. Bado tuna kumbukumbu kuwa Ndugai hadi leo hii anaishi kama digidigi kwasabb tu aliikosoa serikali ya awamu ya 6 kwa kukopa Sana. Na sasa Dr. Bashiru anasakamwa Sana kwa kukosoa wananchi na viongozi wanaosifia na kumshukuru mama kwa kazi/huduma zitolewazo na serikali yake.

Kwa mujibu wa Dr. Bashiru huduma ama kazi hizi zinafanywa kwa kodi zetu hivyo ni haki yetu. Hatupaswi kusema "mama anaupiga mwingi" ama "asante mama". Kosa la Dr. Bashiru hapa ni lipi?
Hakuna anaemchukia bashiru ila tunashangaa kuona alikunya na leo anayakataa mavi yake mwenyewe
 
Itakuwa akili mbovu kuaminishana kwamba kabla ya Magufuli kulikuwa hakuna uhalifu wa kutekwa watu.
Wakati wa Magufuli walitekwa wafuatao;- Mo, Gwanda, Ben Sa8, TitoMagoti, Lwajabe, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, n k

Haya na wewe tutajie waliowahi kutekwa kabla ya Magufuli.
 
Sasa huyo Ndugai kwa nini kakubali kujiuzulu kama aliona ana hoja ya msingi? Yeye kama kiongozi wa bunge kazi yake si kuisimamia serikali? Sasa kwa nini alijiuzulu baada ya kuisimamia serikali kama majukumu ya kazi yake yanavyosema?
Ndugai alikuwa hana uwezo wa kukataa amri ya mwenyekiti wa chama chake kilichompendekeza kuwa spika. Angekataa kujiuzulu angefukuzwa ama kufutwa uqnachama kwanza kisha kupoteza uspika.

Nchi hii tu rais ni kama Mungu. Anaweza kumpora hata mkeo/mumeo mbele ya hadhara na usimfanye kitu. Anaweza kuangamiza ukoo wako na usimfanye kitu.
 
Tatizo la CCM huwezi kuwatetea kimantiki.

Even when they do right, they do right wrongly!

Huyo Ndugai alijiuzulu mwenyewe. Spika wa Bunge ni kiongozi wa muhimili unaojitegemea. Angesimamia anachoona sawa tu, sasa kajiuzulu mwenyewe, au hata kama kashinikizwa, hakutakiwa kujiuzulu kama hajataka.

Hakuna popote katika katiba ya Tanzania ambapo rais anaweza kumuondoa Spika.

Marekani Federal Prosecutor/ US Attorney tu, Preet Bharara, alipigwa mkwala na rais Donald Trump (rais ndiye ana appoint, like Bharara aliteuliwa na Obama). Trump alimwambia Bharara ajiuzulu. Bharara akakataa kujiuzulu, akamwambia Trump ni lazima unifukuze kazi wewe mwenyewe dunia nzima ione umenifukuza kazi, lakini sijiuzulu ng'o, kwa kuwa sina sababu ya kujiuzulu.

Sasa huyo Ndugai kwa nini kakubali kujiuzulu kama aliona ana hoja ya msingi? Yeye kama kiongozi wa bunge kazi yake si kuisimamia serikali? Sasa kwa nini alijiuzulu baada ya kuisimamia serikali kama majukumu ya kazi yake yanavyosema?

Huyo Bashiru katika hoja zote za msingi za madudu yanayofanywa na serikali hii, yeye na usomi wake wote kaona kitu subjective kama watu kushadadia "mama kaupiga mwingi" ndiyo kitu cha msingi? Is this the best criticism he could come up with?
Kiranga siku hizi huonekani sana hapa jamvini. Busara na vision zako zinahitajika! Tatizo la CCM (na wanasiasa wengi wa Bongo) ni kuwa kila mtu yuko pale kwa ajili ya tumbo lake na si kufanya kazi. Mtu akipata cheo anaona kama amepewa ulaji (kama inavyojulikana na kila mtanzania). Na pia hata kama huyo Ndugai angeleta upinzani, sana sana angeishia pabaya na ni wananchi wachache sana wangetoka kumtetea. Siyo kama napinga ulichoandika ila najaribu kuonyesha kuwa kama nchi tuna safari ndefu. Bila wananchi wengi kujitambua na kuthubutu kujitokeza kutetea viongozi wazuri na kuwajibisha viongozi wabovu, viongozi hawatabadilika wenyewe kamwe.
 
Ndugai alikuwa hana uwezo wa kukataa amri ya mwenyekiti wa chama chake kilichompendekeza kuwa spika. Angekataa kujiuzulu angefukuzwa ama kufutwa uqnachama kwanza kisha kupoteza uspika.

Nchi hii tu rais ni kama Mungu. Anaweza kumpora hata mkeo/mumeo mbele ya hadhara na usimfanye kitu. Anaweza kuangamiza ukoo wako na usimfanye kitu.
Unajuaje kulikuwa au kungekuwa na amri ya mwenyekiti wake? Hapa si kwamba unafanya ubashiri na utabiri wa mambo ambayo hayakutokea, unakisia tu bila ushahidi wala uhakika?

Unajuaje angekataa amri angefukuzwa uanachama? Hapa huoni kwamba kwa mara nyingine unafanya ubashiri na utabiri wa mambo ambayo hayakutokea, unakisia tu bila ushahidi wala uhakika?

Na kama angefukuzwa uanachama kweli, kwa sababu ya jambo aliloliona muhimu, kwa nini kufukuzwa uanachama kwa kitu mtu anachokiamini ni jambo baya?
 
Nimeshangaa mpaka Fatma Karume nae twitter anamponda Bashiru, anatoa kisingizio cha Bashiru kupewa ubunge na Samia kama ndio alitakiwa kufunga
Huyu Fatma ni mkabila na mkanda. Tangu mzanzibari mwenziwe akalie kiti cha ikulu reasoning yake imeathiriwa na ukanda. Haoni matatizo wala madhaifu ktk uongozi wa awamu hiii. Tanzania tuna safari ndefu Sana.
 
Hii nchi ina mambo ya ajabu sana, mentality zetu wengi ni za kibinafsi sana, tunaojiona malaika tusiokosea ambao tuko sharp kuwanyooshea vidole wengine.

Nimeshangaa mpaka Fatma Karume nae twitter anamponda Bashiru, anatoa kisingizio cha Bashiru kupewa ubunge na Samia kama ndio alitakiwa kufunga mdomo, a very stupid reasoning.

Huyu mwanamke anayejinadi kuijua demokrasia siku zote, leo anasimama upande wa kidikteta kumfunga Bashiru mdomo kisa alipewa ubunge na Samia?!

Taifa letu linaendeshwa kimahaba sana, na kibinafsi; hakuna wakumuamini wengi wapo kimaslahi zaidi, na maslahi yenyewe yanatofautiana kuanzia kiuchumi, mpaka kwenye mahaba ya vyama yaliyopitiliza, urafiki nk.
Hivi mlikuwa mmeamini kuwa Fatma Karume ni mtetezi wa haki na wananchi? Huyu mama alijigeuza mwanademokrasia baada ya maslahi yake kuguswa na mwendazake basi. Chaguzi za nyuma CCM iliua sana ili baba yake aingie ikulu, mlisikia lolote kutoka kwake? Na hivi ndivyo tulivyo watanzania wengi.
 
Kiranga siku hizi huonekani sana hapa jamvini. Busara na vision zako zinahitajika! Tatizo la CCM (na wanasiasa wengi wa Bongo) ni kuwa kila mtu yuko pale kwa ajili ya tumbo lake na si kufanya kazi. Mtu akipata cheo anaona kama amepewa ulaji (kama inavyojulikana na kila mtanzania). Na pia hata kama huyo Ndugai angeleta upinzani, sana sana angeishia pabaya na ni wananchi wachache sana wangetoka kumtetea. Siyo kama napinga ulichoandika ila najaribu kuonyesha kuwa kama nchi tuna safari ndefu. Bila wananchi wengi kujitambua na kuthubutu kujitokeza kutetea viongozi wazuri na kuwajibisha viongozi wabovu, viongozi hawatabadilika wenyewe kamwe.
Nakuelewa.

Kwa hiyo hoja nzima ya kusema Ndugai kaonewa ni ujinga.

Kwa sababu hata yeye mwenyewe Ndugai kakosoa kisiasa, hakukosoa kwa kupinga mabaya on principle.

Magufuli alikopa sana, Ndugai hakusema kitu.

Alivyoingia Samia, mara Ndugai kapata mwanga kuona kukopa ni jambo baya sana?

Haya.

Tuseme kukopa jambo baya sana.

Sasa, yeye Spika ametumwa na watu awapiganie. Aondoe mambo mabaya, kwa nini hakupigania wananchi serikali iache kukooa sana? Kwa nini kajiuzulu?

Yani hata kama unakubaliana na hoja ya Ndugai kwamba kukooa ni jambo baya, alichifanya kujiuzulu bika kuisimamia serikali, ni scandal.

Mimi nilitegemea Speaker aisimamie serikali atuambue serikali inakopa bila kupitisha mikopo bungeni.

Spika ndiye anaendesha bunge linalopitisha bajeti. Analalamikia vipi mikopo? Ina maana mikopo haikupitishwa bungeni? Kama haikupita, kwa nini anajiuzulu badala ya kuonesha udhaifu huu wa serikali (executive) kama kazi yake inavyomtaka?

Hapi ndipo utaona huu ujinga ni maigizo matupu.

Ndugai alikuwa anafanya some other power moves. Hakuwa anapinga mikopo.
 
Alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Bashiru alisema nafasi hiyo ni kubwa sana. Hatagombea nafasi yoyote wala hatokubali uteuzi wowote.
Kateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Na sasa ni mbunge wa kuteuliwa.
 
Bashiru anafaa kuingia katika kuzimu ya kisiasa, ni moja ya wahandisi wa Siasa za kijambazi na kiuaji. Kwa usalama wa nchi, asipate nafasi yoyote ile maisha yake yote. Ni Samia tu ana huruma, huyo alifaa awe kemondo anavua dagaa
 
Wakati wa Magufuli walitekwa wafuatao;- Mo, Gwanda, Ben Sa8, TitoMagoti, Lwajabe, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, n k

Haya na wewe tutajie waliowahi kutekwa kabla ya Magufuli.
Narudia tena kuwa ni akili mbovu kuaminishana kwamba uhalifu wa watu kutekwa haukuwepo kabla ya Magufuli, halafu sikuwa najua kama Ney wa mitego nae kumbe alitekwa.
 
halafu sikuwa najua kama Ney wa mitego nae kumbe alitekwa.
Utakuwa ulikuwa mlamba asali enzi za Yuda, ndiyo maana hukuwa unafuatilia matukio maovu ya serikali yake.

Ney ni miongoni mwa waliotekwa enzi za dikteta jiwe
 
Huyu Fatma ni mkabila na mkanda. Tangu mzanzibari mwenziwe akalie kiti cha ikulu reasoning yake imeathiriwa na ukanda. Haoni matatizo wala madhaifu ktk uongozi wa awamu hiii. Tanzania tuna safari ndefu Sana.
Ukanda ni sababu nyingine ambayo sikuiweka, tuna siasa za hovyo sana.
 
Hivi mlikuwa mmeamini kuwa Fatma Karume ni mtetezi wa haki na wananchi? Huyu mama alijigeuza mwanademokrasia baada ya maslahi yake kuguswa na mwendazake basi. Chaguzi za nyuma CCM iliua sana ili baba yake aingie ikulu, mlisikia lolote kutoka kwake? Na hivi ndivyo tulivyo watanzania wengi.
Hawa wanatumia poor reasoning ya wafuatiliaji wao kuwaendesha wanavyotaka, na kwasababu wengi wanatembea na tag ya "Fatma msomi wa nje" ndio wanaingizwa kingi kizembe bila kujiuliza chochote ..

Wao wanabaki kuimba shangazi this.. shangazi that..!!
 
Utakuwa ulikuwa mlamba asali enzi za Yuda, ndiyo maana hukuwa unafuatilia matukio maovu ya serikali yake.

Ney ni miongoni mwa waliotekwa enzi za dikteta jiwe
Tuna mitazamo tofauti mkuu, mimi sikuwa nasubiri mtu kutekwa ili tu nihusishe utekaji huo na Magufuli. Ndio maana nimeshangaa kusikia kuwa hata Ney kuwa nae alitekwa na Magufuli, najiuliza lipi hasa lilofanya hadi nae afikie kutekwa.
 
Mtu wenu hasafishiki hata kwa dodoki
 
Tuna mitazamo tofauti mkuu, mimi sikuwa nasubiri mtu kutekwa ili tu nihusishe utekaji huo na Magufuli. Ndio maana nimeshangaa kusikia kuwa hata Ney kuwa nae alitekwa na Magufuli, najiuliza lipi hasa lilofanya hadi nae afikie kutekwa.
Screenshot_20221120-104101_1.jpg

Yule mtu hakupenda kukosolewa. Ney alipotoa wimbo wa kuikosoa serikali yake akatuma polisi manane ya usiku wamteke.
 
Back
Top Bottom