CCM na wanaccm, nini kosa la Bashiru? Demokrasia kwenu ni nongwa?

CCM na wanaccm, nini kosa la Bashiru? Demokrasia kwenu ni nongwa?

Wakati wa Magufuli walitekwa wafuatao;- Mo, Gwanda, Ben Sa8, TitoMagoti, Lwajabe, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, n k

Haya na wewe tutajie waliowahi kutekwa kabla ya Magufuli.
Sengondo Mvungi Dk,Holimboka dk,Mwangosi,mwandishi.
 
Serikali ya awamu ya 5 iliyoongozwa na chama cha mapinduzi (Katibu mkuu akiwa Bashiru) ilifanya maovu ambayo hayawezi kusahaulika katika historia ya nchi yetu. Namuona Bashiru huyu kuwa kwenye vita kali na Bashiru yule. Bashiru ni mnafiki sana. Anazungumza utadha si yeye aliyekuwa akitoa sifa lukuki kwa mwendazake leo anawazuiaje wanaccm kumsifia mama.

Anyways, truth be, huyu mkomunist/ msosholost ni mnafiki sana ila ukweli aliousema utabakia kuwa ukweli. Mama anaweza kuwa anapenda kusifiwa lakini hawezi kupenda kitu ambacho hakina maslahi kwa taifa. Kumsifia mama kwa matumizi mazuri ya kodi zetu hakuna maslahi kwa taifa. Hebu mama aambiwe ukweli kuwa hali ni ngumu sana kitaani. Bei za bidhaa ziko juu mno, maji hakuna ila bili za maji zipo, umeme hakuna na uchumi umezorota.

Miaka 61 ya uhuru nchi yetu yenye mito mingi na maziwa makubwa, bado ina tatizo la maji kuliko nchi zilizo jangwani. Hii ni aibu tosha kwake na kwa raia.

Namuunga mkono mnafiki.
 
Sengondo Mvungi Dk,Holimboka dk,Mwangosi,mwandishi.
Hawa hawakutekwa. Sengondo Mvungi aliuawa na wahuni, Dr. Ulimboka aling'olewa kucha na wahuni, wakati mwandishi Mwangosi aliuawa na mabomu ya polisi.
 
Sijafurahishwa na mfululizo wa kejeli, matusi na majibu dhidi ya Dr. Bashiru mara baada ya yeye kutumia Uhuru wa kikatiba wa kujieleza.

Nafahamu akiwa "mtoto pendwa" awamu ya 5 Dr. Bashiru aliwahi kunena maneno ya makufuru dhidi wa watanzania kwamba "ccm itatumia hata vyombo vya dola ili kusalia madarakani".

Pamoja na makosa yake aliyoyafanya awamu ya 5 hapaswi kuhukumiwa kimakosa. Yatupasa kusahihisha kosa kwa kutenda haki ili ajifunze.

CCM siyo marafiki wa demokrasia. Bado tuna kumbukumbu kuwa Ndugai hadi leo hii anaishi kama digidigi kwasabb tu aliikosoa serikali ya awamu ya 6 kwa kukopa Sana. Na sasa Dr. Bashiru anasakamwa Sana kwa kukosoa wananchi na viongozi wanaosifia na kumshukuru mama kwa kazi/huduma zitolewazo na serikali yake.

Kwa mujibu wa Dr. Bashiru huduma ama kazi hizi zinafanywa kwa kodi zetu hivyo ni haki yetu. Hatupaswi kusema "mama anaupiga mwingi" ama "asante mama". Kosa la Dr. Bashiru hapa ni lipi?
Uaneni tu ,we don't care ,fisiemu ni fisi
 
Hakuna kibaya alichosema maana huo ndio ukweli ila shida unafiki kwamba wewe jana ndio ulikuwa kwanza kushabikia haya kwa maslahi yako leo kwa mwenzako unaona mabaya. Kwa bahati nzuri anachosema ni sahihi lakini kwanini leo? sababu hauko madarakani tena
Yeah alikuwa madarakani hivyo hakuwa kwenye nafasi ya kukosoa bali utekelezaji.
 
Hawa hawakutekwa. Sengondo Mvungi aliuawa na wahuni, Dr. Ulimboka aling'olewa kucha na wahuni, wakati mwandishi Mwangosi aliuawa na mabomu ya polisi.
Kwani hao wakina saa8 Ninani kawadhibitisha kuwa waliuwawa na Magufuli Sio wauni?,hakuna utawala usio uwa kama utafuata Sheria za nchi hata Sasahivi watu wanauwawa kwa jina la panya lord.
 
Tatizo la CCM huwezi kuwatetea kimantiki.

Even when they do right, they do right wrongly!

Huyo Ndugai alijiuzulu mwenyewe. Spika wa Bunge ni kiongozi wa muhimili unaojitegemea. Angesimamia anachoona sawa tu, sasa kajiuzulu mwenyewe, au hata kama kashinikizwa, hakutakiwa kujiuzulu kama hajataka.

Hakuna popote katika katiba ya Tanzania ambapo rais anaweza kumuondoa Spika.

Marekani Federal Prosecutor/ US Attorney tu, Preet Bharara, alipigwa mkwala na rais Donald Trump (rais ndiye ana appoint, like Bharara aliteuliwa na Obama). Trump alimwambia Bharara ajiuzulu. Bharara akakataa kujiuzulu, akamwambia Trump ni lazima unifukuze kazi wewe mwenyewe dunia nzima ione umenifukuza kazi, lakini sijiuzulu ng'o, kwa kuwa sina sababu ya kujiuzulu.

Sasa huyo Ndugai kwa nini kakubali kujiuzulu kama aliona ana hoja ya msingi? Yeye kama kiongozi wa bunge kazi yake si kuisimamia serikali? Sasa kwa nini alijiuzulu baada ya kuisimamia serikali kama majukumu ya kazi yake yanavyosema?

Huyo Bashiru katika hoja zote za msingi za madudu yanayofanywa na serikali hii, yeye na usomi wake wote kaona kitu subjective kama watu kushadadia "mama kaupiga mwingi" ndiyo kitu cha msingi? Is this the best criticism he could come up with?
Huyo Ndugai anajua kabisa hakutakiwa kujiuzuru lakini anazijua internal dealings za CCM zinavyofanya kazi na ameshazitumia sana tuu, kumbuka alipigwa risasi mbunge wake ,karibu na maeneo ya bunge na chini ya uongozi wake, lakini hata uchunguzi hakuwahi kufanya, asingejiuzuru nisingeshangaa kusikia speaker yuko nje kwa matibabu na usingemsikia tena, au wangemvua uanachama wa CCM na kupoteza ubunge wake na haki ya kuwa speaker, kumbambikizia kesi na kumuondolea security zote, kujizuru kwake ilikuwa ni kutetea uhai wake sio siasa
 
Sijafurahishwa na mfululizo wa kejeli, matusi na majibu dhidi ya Dr. Bashiru mara baada ya yeye kutumia Uhuru wa kikatiba wa kujieleza.

Nafahamu akiwa "mtoto pendwa" awamu ya 5 Dr. Bashiru aliwahi kunena maneno ya makufuru dhidi wa watanzania kwamba "ccm itatumia hata vyombo vya dola ili kusalia madarakani".

Pamoja na makosa yake aliyoyafanya awamu ya 5 hapaswi kuhukumiwa kimakosa. Yatupasa kusahihisha kosa kwa kutenda haki ili ajifunze.

CCM siyo marafiki wa demokrasia. Bado tuna kumbukumbu kuwa Ndugai hadi leo hii anaishi kama digidigi kwasabb tu aliikosoa serikali ya awamu ya 6 kwa kukopa Sana. Na sasa Dr. Bashiru anasakamwa Sana kwa kukosoa wananchi na viongozi wanaosifia na kumshukuru mama kwa kazi/huduma zitolewazo na serikali yake.

Kwa mujibu wa Dr. Bashiru huduma ama kazi hizi zinafanywa kwa kodi zetu hivyo ni haki yetu. Hatupaswi kusema "mama anaupiga mwingi" ama "asante mama". Kosa la Dr. Bashiru hapa ni lipi?
swadktaaa
 
Unaweza usisikie ila haina maana kwamba uhalifu wa kutekena hakuna, kama kipindi hiki panya road wameibuka tena kwa kasi wanapiga watu mapanga na hadi kuuwa ndio itakuwa huo uhalifu wa kutekana? Itakuwa akili mbovu kuaminishana kwamba kabla ya Magufuli kulikuwa hakuna uhalifu wa kutekwa watu.
Panya road ni wahalifu wa kawaida, ila watekaji ni wahalifu waliokuwa sponsored na Magufuli
 
Mbona kipindi Cha magufuli hakusema hayo na wakati watu walikua wanamsifia magu wakati na yeye pia alikua anatumia Kodi zetu .
Angekaa kimya tu nadhani kajiharibia zaidi aisee
Hapa ndio nakumbuka alichosema Einstein kwamba akili ni kile kinachobaki ukitoa ulichofundishwa.
 
Sijafurahishwa na mfululizo wa kejeli, matusi na majibu dhidi ya Dr. Bashiru mara baada ya yeye kutumia Uhuru wa kikatiba wa kujieleza.

Nafahamu akiwa "mtoto pendwa" awamu ya 5 Dr. Bashiru aliwahi kunena maneno ya makufuru dhidi wa watanzania kwamba "ccm itatumia hata vyombo vya dola ili kusalia madarakani".

Pamoja na makosa yake aliyoyafanya awamu ya 5 hapaswi kuhukumiwa kimakosa. Yatupasa kusahihisha kosa kwa kutenda haki ili ajifunze.

CCM siyo marafiki wa demokrasia. Bado tuna kumbukumbu kuwa Ndugai hadi leo hii anaishi kama digidigi kwasabb tu aliikosoa serikali ya awamu ya 6 kwa kukopa Sana. Na sasa Dr. Bashiru anasakamwa Sana kwa kukosoa wananchi na viongozi wanaosifia na kumshukuru mama kwa kazi/huduma zitolewazo na serikali yake.

Kwa mujibu wa Dr. Bashiru huduma ama kazi hizi zinafanywa kwa kodi zetu hivyo ni haki yetu. Hatupaswi kusema "mama anaupiga mwingi" ama "asante mama". Kosa la Dr. Bashiru hapa ni lipi?
Wengi wanaomkosoa Bashiru hawakosoi kwa hoja zaid ya personal attack, hawasemi kosa lake ni nini!
 
Panya road ni wahalifu wa kawaida, ila watekaji ni wahalifu waliokuwa sponsored na Magufuli
Watu wanapigwa mapanga ya kichwa na wengine wameuliwa kabisa halafu wewe unaita uhalifu wa kawaida.
 
Watu wanapigwa mapanga ya kichwa na wengine wameuliwa kabisa halafu wewe unaita uhalifu wa kawaida.
Sio uhalifu ambao ulikuwa sponsored na serikaki, tofauti na ule wa Magufuli ambaye alikuwa akituma watu kutekwa na kupigwa risasi
 
Back
Top Bottom