CCM na wanaccm, nini kosa la Bashiru? Demokrasia kwenu ni nongwa?

CCM na wanaccm, nini kosa la Bashiru? Demokrasia kwenu ni nongwa?

Mbona kipindi Cha magufuli hakusema hayo na wakati watu walikua wanamsifia magu wakati na yeye pia alikua anatumia Kodi zetu .
Angekaa kimya tu nadhani kajiharibia zaidi aisee
Hana haki ya kusema chochote wakati huu kisa alikuwa kipindi cha JPM?
 
Hana haki ya kusema chochote wakati huu kisa alikuwa kipindi cha JPM?
Misingi ya demokrasia iheshimiwe. Vinginevyo tutateseka kwa zamu, leo kwa Dr. Bashiru kesho kwa anayemcheka Dr. Bashiru
 
Bashiru huwa ni mpuuzi flani namba moja tena msomi bure ambaye hajaelimika,
Ila hoja zake nyie MaCCM mngezijibu kwa hoja.

Mataga pori nendeni hapo maktaba ya mkoa mtafute kitabu cha Mwalimu Nyerere kinaitwa TUJISAHIHISHE mfanye homework yenu ya Logic and Reasoning.
 
Wakati wa Magufuli walitekwa wafuatao;- Mo, Gwanda, Ben Sa8, TitoMagoti, Lwajabe, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, n k

Haya na wewe tutajie waliowahi kutekwa kabla ya Magufuli.
Profesa Juan mwakyusa, Dr ulimboka, Dr Semvungi, yule mwandishi wa habari pale Iringa,Kubenea etc
 
Sasa kwanini mumdanganye bibi wa watu eti anaupiga mwingi wakati she's hopeless
 
Sijafurahishwa na mfululizo wa kejeli, matusi na majibu dhidi ya Dr. Bashiru mara baada ya yeye kutumia Uhuru wa kikatiba wa kujieleza.

Nafahamu akiwa "mtoto pendwa" awamu ya 5 Dr. Bashiru aliwahi kunena maneno ya makufuru dhidi wa watanzania kwamba "ccm itatumia hata vyombo vya dola ili kusalia madarakani".

Pamoja na makosa yake aliyoyafanya awamu ya 5 hapaswi kuhukumiwa kimakosa. Yatupasa kusahihisha kosa kwa kutenda haki ili ajifunze.

CCM siyo marafiki wa demokrasia. Bado tuna kumbukumbu kuwa Ndugai hadi leo hii anaishi kama digidigi kwasabb tu aliikosoa serikali ya awamu ya 6 kwa kukopa Sana. Na sasa Dr. Bashiru anasakamwa Sana kwa kukosoa wananchi na viongozi wanaosifia na kumshukuru mama kwa kazi/huduma zitolewazo na serikali yake.

Kwa mujibu wa Dr. Bashiru huduma ama kazi hizi zinafanywa kwa kodi zetu hivyo ni haki yetu. Hatupaswi kusema "mama anaupiga mwingi" ama "asante mama". Kosa la Dr. Bashiru hapa ni lipi?
Chama na serikali yake vikikaa madarakani hujikuta imejingiza kwenye mfumo.Ndo maana hata marehemu allikuwa akitafuta sifa kwa miradi yote hata iliyofadhiliwa.Tuhuma kwamba mama naye anapenda sifa ni kutokana na mfumo kwamba kila kitu kinaletwa na Rais na siyo walipakodi ambao hawaitwi hata kupokea ndege,hivyo bashiru asimhukumu mother wakati huo ni mfumo ambao utavunjwa na ujio wa katiba ya wananchi
 
Bashiru anafaa kuingia katika kuzimu ya kisiasa, ni moja ya wahandisi wa Siasa za kijambazi na kiuaji. Kwa usalama wa nchi, asipate nafasi yoyote ile maisha yake yote. Ni Samia tu ana huruma, huyo alifaa awe kemondo anavua dagaa
Bahati nzuri wewe chinembe huna mamlaka yoyote nchi hii ya kutekeleza hayo mawazo yako ya kishetani na husda. Hizo mamlaka ulizozitaja ndio zinazoona Bashiru anafaa na anapewa nafasi, utaendelea kumuona hivihivi akizidi kupaa na kupasua anga.
 
Mtu wenu hasafishiki hata kwa dodoki
Sina kazi ya kuchafua watu wala kusafisha watu mkuu sina muda huo, mie huwa sijengi chuki wala mahaba kwa hawa wanasiasa huwa nawachukulia kama walivyo tu.

Mkuu nilipitwa na habari ya kutekwa Nay wa mitego, ningekuwa mimi hata nisingehangaika kumteka mtu kama huyo maana hana athari yeyote muziki wenyewe ushamshinda.
 
Sijafurahishwa na mfululizo wa kejeli, matusi na majibu dhidi ya Dr. Bashiru mara baada ya yeye kutumia Uhuru wa kikatiba wa kujieleza.

Nafahamu akiwa "mtoto pendwa" awamu ya 5 Dr. Bashiru aliwahi kunena maneno ya makufuru dhidi wa watanzania kwamba "ccm itatumia hata vyombo vya dola ili kusalia madarakani".

Pamoja na makosa yake aliyoyafanya awamu ya 5 hapaswi kuhukumiwa kimakosa. Yatupasa kusahihisha kosa kwa kutenda haki ili ajifunze.

CCM siyo marafiki wa demokrasia. Bado tuna kumbukumbu kuwa Ndugai hadi leo hii anaishi kama digidigi kwasabb tu aliikosoa serikali ya awamu ya 6 kwa kukopa Sana. Na sasa Dr. Bashiru anasakamwa Sana kwa kukosoa wananchi na viongozi wanaosifia na kumshukuru mama kwa kazi/huduma zitolewazo na serikali yake.

Kwa mujibu wa Dr. Bashiru huduma ama kazi hizi zinafanywa kwa kodi zetu hivyo ni haki yetu. Hatupaswi kusema "mama anaupiga mwingi" ama "asante mama". Kosa la Dr. Bashiru hapa ni lipi?
Tunahitaji mabadiliko , haiwezekani tangu uhuru mpaka sasa matatizo ni yale yale maji, umeme aiwezekani asee ccm itoke

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Watanzania % kubwa wanatamani ccm iondoke madarakani. Lkn tutaitoaje?
Mkuu unapima kwa kipimo gani hadi ukaweza kujua kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanatamani ccm itoke madarakani ukilinganisha na ambao hawana hayo mawazo kabisa?
 
Hii nchi ikikosa wasema ukweli itakuwa nchi inayoteketea... wapumbafu hawaelewi ndomana watawala wanatuswaga kama ng'ombe!!
Simamia ukweli muda wote siyo ukipewa cheo unajisahau, ukiachwa kwenye mataa ndiyo unakuwa msema kweli namba moja.
 
Kosa la Bashir ni njaa aliyonayo tu,, kasubiri uteuzi hadi amekata tamaa,, anajiandaa kurudi CUF yeye na rafikie Mpina, waje kugombea urais😂😂.
Je mpo tayari kuongozwa na mnyarwanda?
 
Ndiyo maana nimeandika kuwa kosa halisahihishwi kwa kosa
Ndiyo kosa halisahihishwi kwa kosa, ila ili ipate kuungwa mkono na watanzania alipaswa kwanza kutoka hadharani akiri aliyotukosea alipokuwa kiongozi maana naye kauli zake ziliumiza wengi.

Vingenevyo ni kumsafishia njia shetani ambaye hakuwahi kuonyesha kujutia hata kidogo makosa yake kwamba yeye hadi sasa yuko sahihi kwa aliyotufanyia, akiropoka ni sawa tu ila wengine hapana.

Atoke kwanza hadharani atuombe radhi kwa maneno yake ya kuudhi ili tumwamini kuwa sasa anastahilli kukosoa hapa na mimi niko tayari kumuunga mkono vinginevyo ni unafiki mbaya wa msomi kama Bashiru.
 
Sijafurahishwa na mfululizo wa kejeli, matusi na majibu dhidi ya Dr. Bashiru mara baada ya yeye kutumia Uhuru wa kikatiba wa kujieleza.

Nafahamu akiwa "mtoto pendwa" awamu ya 5 Dr. Bashiru aliwahi kunena maneno ya makufuru dhidi wa watanzania kwamba "ccm itatumia hata vyombo vya dola ili kusalia madarakani".

Pamoja na makosa yake aliyoyafanya awamu ya 5 hapaswi kuhukumiwa kimakosa. Yatupasa kusahihisha kosa kwa kutenda haki ili ajifunze.

CCM siyo marafiki wa demokrasia. Bado tuna kumbukumbu kuwa Ndugai hadi leo hii anaishi kama digidigi kwasabb tu aliikosoa serikali ya awamu ya 6 kwa kukopa Sana. Na sasa Dr. Bashiru anasakamwa Sana kwa kukosoa wananchi na viongozi wanaosifia na kumshukuru mama kwa kazi/huduma zitolewazo na serikali yake.

Kwa mujibu wa Dr. Bashiru huduma ama kazi hizi zinafanywa kwa kodi zetu hivyo ni haki yetu. Hatupaswi kusema "mama anaupiga mwingi" ama "asante mama". Kosa la Dr. Bashiru hapa ni lipi?
Ni wapi Dk. Bashiru alipomtaja Mhe. Rais? Au wapi alisema kuhusu, "Mama anaupiga mwingi?" Hebu watu waache kuchonganisha viongozi. CCM ni moja na nchi ina Rais mmoja ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM.🙏🙏🙏
 
Mbona kipindi Cha magufuli hakusema hayo na wakati watu walikua wanamsifia magu wakati na yeye pia alikua anatumia Kodi zetu .
Angekaa kimya tu nadhani kajiharibia zaidi aisee
Na yeye pia alikuwacakimsifia magu hadi akateuliwa kuwa katibu kiongozi. Ukiwq mnafiki ujanani, unaweza kuwa mchawi uzeeni. Hata hivyo katika unafiki wake kasema ukweli. Hiyo inatosha ila acha aadhibiwe kwa unafiki wake!
 
Back
Top Bottom