Kwanza tukubaliane sote kwamba, kila mwenye kutokukidhi mahitaji yake binafsi na ya familia yake, na kwamba umasikini alionao umechangiwa kwa asilimia kubwa sana na viongozi wa chama cha CCM ambao hawana ubunifu wowote wa kuwatoa wananchi kwenye umasikini uliopo.
Wanakosaje Ubunifu?
Ni kwa sababu moja tu, ni vigumu sana kuongozwa na watu ambao mawazo yao yote yapo kwenye...nitapataje, nifanye nini ili nipate pesa za kuiba?
Watu wa aina hiyo, hata kama Mungu amewajalia kuwa na upeo mzuri, lakini kwa namna hiyo, akili zao haziwazi nje na kuiba, hawawezi kuwatoa watu kwenye umasikini, narudia tena, mgalagale, mlie na mtakesha kuwaombea, lakini haitatokea watu dizaini hiyo mtegemee miujiza licha kwamba nchi yetu imejaliwa kila lililo jema!
Tufanye nini sasa?
Kwa kuwa nchi yetu, watu wake wote karibu wamefanana na asilimia kubwa ni wacha Mungu, watu ambao wanameza mengi, machungu, karaha, mateso na kila aina ya shuruba na bado wakasema Asante Mungu!
Hata Mimi naungana nao kwa sababu moja, Mimi binafsi naamini katika Amani, kupiganisha watu na kuwaandamanisha ili wakamtoe kiongozi wao, sio njia nzuri, licha kwamba zipo faida zake lakini huwezi kulinganisha na madhara yake.
Faida yake ni kwamba, ni kuwaonyesha viongozi kwamba, wananchi siyo ma mbuzi, wananchi ndio wenye nchi na siyo nchi ni ya kiongozi.
Hasara zake ni kwamba, mnaweza mkajikuta mmeanza upyaaa kabisa kwa kila kitu na wakati mwingine huo upya unaweza kushindanana namna ya kuuanza, kwa sababu itategemeana na mwisho wa dholuba hizo!
Kwa kuwa nchi yetu masikini ni wengi sana ukiondoa tu wachache mno ambao ndio haswaa wanaosumbua na kuwafanya wananchi zaidi ya 80% kuwa hivyo walivyo kwa manufaa yao!
Tunachotakiwa kufanya ni hiki
Ikiwa nchi yetu inakitengo maalumu ambacho kwa hicho kikisema sawa, kiongozi anakuwepo, na kikisema hapana, basi ni hapana!
Naamini kitengo hicho, ndicho haswaa, kwanza hakina ubaguzi, na ni kitengo cha watu wazalendo haswaa, ambao ndani yake huwa kinaumia sana kuhusu hali za watanzania, na ndiyo maana kinauwezo wa kumkataa ama kumkubali kiongozi yeyote yule! Ni wakati wao sasa, kuona nchi ikiondokana na aibu kama hii, ni wakati wao wa kusema hapana!
Najiuliza tu hapa, inawezekanaje watu wanaiba matrlion ya pesa na bado kitengo hiki kinaendelea kuwaamini watu hao?
Hapa Ngoja niseme kwa unyenyekevu, kama si hivyo, nitazilaumu akili zangu kitengo cha watu hawa, wote ni watanzania? Na wana ndugu hapa tanzania? Je, thamani ya nchi kuheshimika wanaijua? Wao wenyewe wanawaza nini juu ya Tanzania? Wanaweza kuumia kama wananchi wa kawaida kuihusu Tanzania?
Ni nani ataiheshimisha nchi? Kama na nyinyi mnaoumizwa juu ya maisha ya watanzania na ndio sauti ya mwisho katika mamlaka ya dunia hii hususani Tanzania mtakaa kustarehe wakati watanzania wenzenu wanaishi kushindia mkate na kodi zao kugawanwa na wachache?
Tanzania nakupenda mpaka naumwa!
Mungu, Ibariki Tanzania