CCM ni chama kikubwa lakini kimekosa viongozi wenye ushawishi

CCM ni chama kikubwa lakini kimekosa viongozi wenye ushawishi

Jenerali Ulimwengu; Chama cha Mapinduzi kina wanachama zaidi ya elfu 8 lkn wenye mawazo tengefu ni watatu tu.
 
Chama kongwe chama dola kimekosa kuwa na makada na viongozi wenye ushawishi pia ikumbukwe chama cha siasa kisicho na ushawishi basi kimeingia ganzi ya kufanya siasa.

Hivyo msajili wa vyama vya siasa nchini afanye wepesi kukitembelea chama hiki kilichofika ukomo wa kuwa chama cha siasa na kuchukua hatua stahiki kukiondoa ktk rejista ya kutambulika kama ni chama cha siasa Tanzania.

Zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa Kuanza Kesho Agosti 30 2021 source : ORPP Website
 
Chama kongwe chama dola kimekosa kuwa na makada na viongozi wenye ushawishi pia ikumbukwe chama cha siasa kisicho na ushawishi basi kimeingia ganzi ya kufanya siasa.

Hivyo msajili wa vyama vya siasa nchini afanye wepesi kukitembelea chama hiki kilichofika ukomo wa kuwa chama cha siasa na kuchukua hatua stahiki kukiondoa ktk rejista ya kutambulika kama ni chama cha siasa Tanzania.
Hahahaha...Tuanze kwanza kuripoti utafunaji wa ruzuku unaofanywa kule
 
Zifahamu sifa za chama dola

25 November 2019
By Kamundu wa JF

Chama dola kutumia mabavu na ‘zawadi’

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM, Dkt. mwalimu Azaveli Lwaitama amesema siasa za Tanzania kwa sasa zimehodhiwa na chama kimoja ambacho ni chama dola.

“Chama cha TANU kilivyoanzishwa hakikuwa na dola na kilikuwa kinachangiwa na watu. Kilikuwa kinabembelezana na watu wakichague. Lakini kilipoichukuwa dola, kama ilivyo Afrika nzima, hivi vyama vikishachukuwa dola vinajigeuza, badala ya kuishi kwa kushawishi vinakuwa vyama vinavyotumia mabavu na zawadi za vyeo – za kugawa ukuu wa mikoa, ukuu wa wilaya, ukatibu, ukurugenzi’’

“...ama kutumia hela iliyokusanywa kama kodi kwa ajili ya maendeleo na kutumiwa kama zawadi kwa wale wanaheshimu chama tawala. Hiki si chama tena cha siasa, ni chama dola kinachotumia mabavu’’

“…huko nyuma hili halikujitokeza sana kwasababu viongozi walikuwa bado wanafuata nyayo za Mwalimu Nyerere aliyependa awe na ushawishi kwa watu kwa kuwashawishi, na si kushawishi kwa kutumia mabavu.”

Chama dola kupuuzia umuhimu wa upinzani

“Hizi dola baada ya Mwalimu zinatetea maslahi ya nani, si maslahi ya Mabepari tu?”

“…licha ya kwamba Mwalimu Nyerere aliona kuwa na vyama vingi vingeleta nafasi ya chama tawala kujitathmini kiutawala, sasa hivi chama tawala kimejihakikishia kushinda na hivyo kupuuza uwepo wa vyama pinzani.”

“Baada ya kuwaengua washindani na wao kuamua kujitoa, chama kinaamua kutoa tamko la kuwarudisha….sasa munasema warudi, watarudije wakati anayetoa tamko hilo hana mamlaka kikatiba?"

“…sitashangaa kuona bunge la mwaka ujao likiwa ni la chama kimoja.”

Source : Dkt. Lwaitama: Hawa jamaa (CCM) wakiendelea hivi, hata mwakani chama pinzani chenye kujiheshimu kitajitoa
 
Toka Maktaba :
November 24, 2019

Mzee Augustine Lyatonga Mrema alaani uroho wa chama dola kugandamiza siasa


Augustino Lyatonga Mrema atoa maneno mazito kijijini Kiraracha Moshi vijijini nchini Tanzania kuhusiana na uchaguzi ulivyovurugwa aapa kwenda kwa Mh. Rais kumwambia hali hiyo mbaya ya kisiasa na kwa uzoefu wake kama naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani miaka ya nyuma hali hii ni hatari kwa nchi kifupi nanukuu 'anasema hakuna nchi'
 
TOKA MAKTABA:

Uchaguzi wa vitongoji, 2019 CCM yakosa ushawishi, hali ni mbaya

24 November 2019

'Hakuna demokrasia inji hii' - Augustino Mrema awaambia viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro waliokuwa wanapita kukagua zoezi la upigaji kura linavyoenda

 

TOKA MAKTABA :​

27 November 2019​

Jafo atangaza matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019​




Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimeshinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Vijiji 12,260 sawa na asilimia 99.9, Mitaa 4263 sawa na asilimi 100 huku kikijinyakulia vitongoji 63,970 sawa na Asilimia 99.4.

Ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya matokeo ya uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa uliofanyika tarehe 24/11/2019 kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma.

Mhe Jafo amesema katika mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 jumla ya nafasi 332,160 zilihusika katika uchaguzi ambapo kulikuwa na Vijiji 12,262, Mitaa 4,263, vitongoji, 63.992, wajumbe kundi la wanawake 106, 622, wajumbe kundi mchanganyiko 145,021.

Amefafanua kuwa jumla ya wananchi 555,036 kutoka vyama mbalimbali vya siasa walifanikiwa kuchukua fomu za kugombea ambapo wananchi waliorejesha fomu ni 539,993 sawa na asilimia 97.3.

Mhe. Jafo amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kilipita bila kupingwa kwa jumla ya nafasi za uongozi 316, 474 ambapo nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji waliopita ni 12,028, Wenyeviti wa Vitongoji 62,927, Wenyeviti wa Mitaa 4,207, Wajume kundi la Wanawake 105,953 na Wajumbe kundi mchanganyiko 131, 359.

Ameitaja Mikoa ambayo wagombea wa nafasi zote za uongozi walipita bila kupingwa kupitia Chama cha Mapinduzi ni Tanga, Katavi, Ruvuma na Njombe

Ameendelea kusema kuwa Chama cha CUF kimepata nafasi moja katika ngazi ya wenyeviti wa vijiji, wajumbe kundi la wanawake wamepata nafasi tatu na wajumbe kundi mchanganyiko wamepata nafasi 14.

Mhe. Jafo amesema kwa upande wa Chadema, wenyeviti wa vijiji imeshinda nafasi moja, haikufanikiwa kupata Wenyeviti wa Mitaa, Wenyeviti wa vitongoji imepata nafasi 19, wajumbe kundi la wananawake imepata nafasi 39 na wajumbe kundi mchanganyiko nafasi 71.

Amesema Chama cha ACT wazalendo kilipata uongozi ngazi ya Wenyeviti wa Vitongoji nafasi moja, wajumbe kundi la wanawake nafasi moja na wajumbe mchangayiko 11 wakati chama cha UDP kilipata nafasi moja kwa upande wa wajumbe kundi la wanawake na chama cha DP kikipata nafasi moja.

Amevishukuru vyama vya siasa ambavyo vimeonesha ukomavu wa Kisiasa na kudumisha demokrasia nchini kwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Aidha amewashukuru wananchi, Viongozi wa Serikali katika ngazi ya Wizara , Taasisi, Idara za Serikali Mikoa , Wilaya, Halmashauri, Tarafa, Kata, Vijiji na Mtaa kwa kushiriki kikamilifu kusimamia na kukamilisha uchaguzi kwa amani.
 
KANU ilitoka madarakani wakaingia Wapinzani ambao walihamia upinzani miezi mitatu kabla ya uchaguzi

Baadae yule Mgombea Urais wa KANU waliemkataa hadi KANU ikaanguka akaingia madarakani kwa mlango wa nyuma na genge lake la KANU
ipo siku tu ,.....lakin hili chama litatoka madarakani ....ni swala la muda
 
Huwezi kuwa dikteta kama wewe sio Rais, Waziri mkuu au Mfalme wa nchi
Vyama vya upinzani ni vidogo, lakini vimejaa viongozi wahuni, madikteta na wapenda madaraka. kwa maana hiyo bora CCM mara mia
 
Serikali ya Tanzania yatuhumiwa kubana na kukandamiza upinzani kuelekea uchaguzi wa 2020 Oktoba 28
Oct 12, 2020 13:56 UTC

Serikali ya Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania imetunga na kutekeleza sheria kali za kuogofya ili kukandamiza kila aina ya upinzani, wakati nchi hiyo inaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika tarehe 28 ya mwezi huu wa Oktoba 2020 .

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la kutetea haki za binadamu la Msamaha Duniani, Amnesty International.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mamlaka za dola zimebana haki za uhuru wa kutoa maoni na kujumuika kwa amani.

Amnesty International imebainisha katika ripoti yake kuwa, katika miezi ya karibuni, askari usalama wa serikali ya Tanzania wamewatia nguvuni wagombea wa upinzani kwa makosa bandia na kuwazuia kutumia haki yao ya uhuru wa kujumuika, kutangamana na kufika kokote watakako.

Mkurugenzi wa Shirika la Msamaha Duniani kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Deprose Muchena amesema: "Tanzania imezitumia sheria kama silaha mpaka imefika hadi, hakuna mtu anayejua ni katika hali gani anakuwa ametekeleza au kukiuka sheria."

Kwa mujibu wa Muchena "wanasiasa wametiwa nguvuni kwa kufanya au kuhudhuria mikutano, vyombo vya habari vimefungiwa au kupigwa marufuku, harakati za mitandaoni zimebambikiziwa makosa ya uhalifu na asasi zisizo za kiserikali NGOs zimeminywa kwa kuwekewa kanuni zisizo na kikomo."

4bve8f69417c521qwil_800C450.jpg
Deprose Muchena Mkurugenzi huyo wa Amnesty International kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika amesema, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli anapaswa kuchukua hatua haraka za kurekebisha uporomokaji wa uhuru wa kisiasa na kiraia nchini humo na kuhakikisha watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati na jumuiya za kiraia zinaendesha shughuli zao kwa uhuru na bila kuingiliwa wala kuwa na hofu yoyote ya kuandamwa na visasi vya vyombo vya dola.

Uchaguzi mkuu wa Tanzania unatazamiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba huku kukiwepo na malalamiko makubwa ya vyama vya upinzani dhidi ya utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya chaguzi za vyama vingi nchini humo, wagombea wengi wa ubunge, uwakilishi na udiwani wa vyama vya upinzani wameenguliwa na tume hizo bila kuonekana kwenye orodha ya waenguliwa hao mgombea yeyote wa chama tawala CCM.

Aidha uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC wa kutenga siku mbili za tarehe 27 na 28 kwa ajili ya upigaji kura katika visiwa hivyo vyenye idadi ndogo ya wapigakura umelalamikiwa vikali na chama kikuu cha upinzani visiwani humo ACT Wazalendo kikidai kuwa, ni njama ya kufanya udanganyifu wa kura kwa manufaa ya chama tawala CCM.../
 
Kwa nafasi yake Magufuli alikiheshimisha Chama cha Mapinduzi lakini hiyo haina maana wengine hawakufanya kitu. Hii ndio inatoa picha ya umuhimu wa kuachiana kijiti unavyoonekana, inasaidia chama kupata mawazo mapya.

Ndugu Samia pia akimaliza kwa mazuri yake na mwenzake atayaendeleza.
.
CCM haikuwa Magufuli na wala sasa sio Samia ndio maana umeona licha ya Magufuli kutokuwepo CCM bado ipo
Ipo ikiwa na hali gani kwa sasa!
Au unaongelea uzuri wa nguo za wana CCM.
 
ipo siku tu ,.....lakin hili chama litatoka madarakani ....ni swala la muda
Tatizo hatuna chama mubadala, vyama vya upinzani vilivyopo ni vya kuhuni tu. Chama kipya kinatakiwa kwa sasa kuichachafya CCM na ikiwezekana kiongoze nchi.
 
Huwezi kuwa dikteta kama wewe sio Rais, Waziri mkuu au Mfalme wa nchi
Udikteka ni kutumia mabavu au amri tu bila kujali anayeitoa amri ni shehe, askofu au Rais. Tumezoea kuona udikteta kwenye siasa kwa sababu siasa ni jumla ya maisha ya watu
 
28 March 2022

PROF. LIPUMBA ACHAFUA HALI YA HEWA, Awaita KIKOSI KAZI MADALALI WA MAMA, AMWANIKA PROF.MUKANDALA



Prof. Ibrahim Lipumba akosoa na kutilia shaka wajumbe wa Kikosi Kazi kilichoteuliwa, kufuatia mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa na Msajili wa Vyama vya Siasa Dodoma wa tarehe 15 - 17 December 2021 pamoja na wadau wa demokrasia.

Source : MwanaHALISI TV


HABARI YA ZIADA :

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi, Machi 12, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu
1648504863615.png

Machi 12, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo Jumamosi Machi 12, 2022 baada ya kupokea maazimio ya awali kutoka kikosi kazi alichokiteua cha kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa uliofanyika Desemba 15-17, 2021 Dodoma.
Rais Samia amemwagiza Waziri huyo kushirikiana na Tanganyika Lawa Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) kutengeneza kanuni hizo.
“Kikosi kazi hicho chenye wajumbe 24, na ambacho kinawajibika moja kwa moja kwa Mhe. Rais, kiliwasilisha maazimio hayo Ikulu Jijijni Dodoma. Maazimio hayo yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji” imeeleza taarifa hiyo ....

Source : Rais aagiza ziandaliwe kanuni zitakazoongoza mikutano ya siasa | Mwananchi
 
Back
Top Bottom