LGE2024 CCM pekee imekamilisha maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, huku vyama vingine vikiandaa visingizio vya kushindwa

LGE2024 CCM pekee imekamilisha maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, huku vyama vingine vikiandaa visingizio vya kushindwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Vyama vingine baada ya wanachama wao kugoma kushiriki maandamano haramu yaliyopigwa marufuku na kudhibitiwa na polisi, wame nyong'onyea, wamesinyaa na wamekua kama wamepigwa ganzi hivi, Lakini pia ni kama wamepoteza uelekeo kabisa. Na kwasababu hiyo eti sasa wanalumbana washiriki au wasishiriki uchaguzi huo muhimu sana wa serikali za mitaa. Na mara nyingi matokeo ya malumbano yao huwaathiri woa wenyewe na wanachama wao.

Vyama vingine kwa uchache vinafanya mikutano ya hadhara kwa kusua sua, hawana ratiba ndefu za mbwembwe kama ilivyokua mara baada tu ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan kuruhusu mikutano ya hadhara na maandamano, baada ya mtangulizi wake hayati J.Magufuli kuzuia mambo hayo. Na ukifuatilia kwa karibu hakuna maandalizi ya uchaguzi huo muhimu sana wa serikali za mitaa badala yake ni muendelezo wa siasa za lawama na kulalamika tu bila kua na mbadala wa mipango mikakati ya malalamiko hayo. Bila shaka maandalizi ya zima moto yanatarajiwa.

Kwa hali hiyo,bila shaka yoyote, ukata wa fedheha, madeni ya kupindukia ndani ya vyama vya siasa yana chochea pakubwa maandalizi ya uchaguzi huo muhimu kwa kiasi hiki ambacho kinachoonekana bayana.

Kwa ujumla vyama vya siasa, vinapitia wakati mgumu zaidi kiuchumi kutokana na kutokua na mipango mikakati bora mbadala ya kiuchumi, na badala kutegemea michango ya wanachama, wadau, wafadhili na wafanyabiashara wenye maslahi ya kisiasa kwenye vyama hivyo..

Ukata wa fedha unaweza kuchochea baadhi ya vyama kutoshiriki uchaguzi huo muhimu kwa kisingizio cha kuzuiwa na polisi kufanya maandamano haramu, lakini pia hofu ya kushindwa kufanya kampeni, fedheha na aibu ya kushindwa vibaya sana na vyama vilivyo jiandaa vizuri sana kwa uchaguzi huo muhimu mathalani CCM n.k 🐒

Una maoni gani kwenye hilo?

Mungu Ibariki Tanzania
 
We ni kenge, CCM ni zaidi ya chama cha siasa, ndio inamiriki hazina,mapato yote ya nchi, wanaweza kufanya watakavyo, wajaribu kubadilishana scheme, chadema iwe ikulu, na CCM iwe kitaani, harafu CCM watake kufanya mikutqno, chadema iwazuie, kwa sheria za kipuuzi, waone kama wataweza ku survive, watendaji wote wa tume ya uchaguzi, ni, waajiliwa, wa serikali, ni makada wa CCM, sasa hapo CCM inahitaji kujipanga ni ni?
CCM ni majizi tu, kama, hulijuhi hili,ama una mtindio wa ubongo, au na wewe ni jizi pia
 
Kwahiyo ukiweka heading ya mandishi makubwa makubwa ndio tusome tukuelewe? Useless
dah!
Gentleman, sasa hiyo nayo ni hoja kweli? umetoa wapi makasiriko hata kwenye mambo yasiyo na maana kabisa aise 🤣

ni muhimu ukajielekeza kwenye hoja mahususi ya msingi mezani, na kama huna mawazo mapya wala fikra mbdala ni busara kukaa kimya tu gentleman 🐒
 
Ni kweli, maana maandalizi ya ccm ni tume ya uchaguzi na vyombo vya dola kukubali kuwatumikia ili watangazwe washindi. Hakuna mpiga kura anayejitambua atakayeendelea kushiriki hizi chaguzi za kishenzi.
 
We ni kenge, CCM ni zaidi ya chama cha siasa, ndio inamiriki hazina,mapato yote ya nchi, wanaweza kufanya watakavyo, wajaribu kubadilishana scheme, chadema iwe ikulu, na CCM iwe kitaani, harafu CCM watake kufanya mikutqno, chadema iwazuie, kwa sheria za kipuuzi, waone kama wataweza ku survive, watendaji wote wa tume ya uchaguzi, ni, waajiliwa, wa serikali, ni makada wa CCM, sasa hapo CCM inahitaji kujipanga ni ni?
CCM ni majizi tu, kama, hulijuhi hili,ama una mtindio wa ubongo, au na wewe ni jizi pia
sasa mihemko na makasiriko ya nini gentleman?

ni muhimu kutumia staha, hekima na busara kueleza maoni na mtazamo wako ambao pia ni muhimu sana kuhusu hoja hiyo mahususi sana mezani. Kumbuka wadau wanajifunza na kuongeza uelewa na ufahamu wao juu ya masuala haya kupitia comments na replies mbalimbali humu jukwaani...

so,
kua na staha at a first place kwa faida ya wadau 🐒
 
Ni kweli, maana maandalizi ya ccm ni tume ya uchaguzi na vyombo vya dola kukubali kuwatumikia ili watangazwe washindi. Hakuna mpiga kura anayejitambua atakayeendelea kushiriki hizi chaguzi za kishenzi.
Nazungumzia vyama vya siasa nchini gentleman,

na kama wewe ni mpiga kura usiejitambua, na usie ona umuhimu wa uchaguzi huu muhimu sana wa serikali za mitaa, tulizana nyumbani, waTanzania wengine wazalendo watakuwakilisha, usiwe na makasiriko tulizana tuli 🐒
 
Na uchaguzi mmeshashinda nyie wenyewe kwa kishindo nchi nzima.Aya furahi sasa kwa nyimbo na mapambio.
hakuna habari ya nyimbo, makasiriko , mihemko wala furaha gentleman..

hayo ni maelezo mafupi bayana, ya uhakika, muhimu sana ya hali halisi ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa ndani ya vyama vya siasa nchini..tunapoelekea uchaguzi kwenye Uchaguzi huo muhimu sana wa kihistoria katika Taifa letu 🐒

Hakuna mbambamba yoyote kwenye ukweli huo gentleman..
 
Manufaa ya uchaguzi ukiwa wa uwazi, huru na wa haki ukijumuisha wote kuanzia mwanzo wa mchakato mzima ni haya katika mfano wake hapa chini:

23 September 2024
New York City

Mahojiano na rais Cyril Ramaphosa kuhusu jinsi 4R zilivyoiinua imani ya wananchi na wafanyabishara ndani ya nchi na wale wawekezaji kutoka nje


JINSI CYRIL RAMAPHOSA ANAVYOTUMIA 4R ZA UKWELI, KAMA ZANA YA KUVUTIA MAENDELEO


View: https://m.youtube.com/watch?v=4gF-YkcFMFQ
As part of his itinerary during his visit to New York for the United Nations General Assembly, President Cyril Ramaphosa has spent the day engaging with the American business community. Earlier, the president had encouraged American business people to explore and seize business opportunities in South Africa. He is about to address the American business forum at the New York Stock Exchange
Kwa kujivunia kutoka moyoni bila kuwa na ulaghai wa kutumia 4R kuwezesha chama chake pekee kuwa na wabunge 100% bunge la taifa na bunge la majimbo, Mheshimiwa Cyril Ramaphosa wa South Africa anajivunia jinsi ANC ilivyovuna 40 % ya kura huku chama kinachofuatia DA 21 % huku asilimia zilizobaki 39% zimegawana vyama vingine vidogo.

Kupitia 4R za ukweli nchi inaendelea kuwa na mihimili huru ya Bunge, Mahakama na vyombo vya habari.

Hali hiyo imewapa imani wawekezaji wa ndani wana imani kuwekeza zaidi ndani na pia hali hiyo inavutia wawekezaji zaidi kutoka nje.

Kutokana na kuwa na kuaminiana ndani, South Africa imekuwa mfano kwa mataifa dada jirani zilizo nchi za SADC na mbali zaidi.

4R za ukweli zisizo na hila ovu zimemuondolea rais wa South Africa kutokukosa usingizi na kuwaza kutumia majeshi ya usalama kama polisi na usalama wa taifa kuwatishia raia.

kutokana na mazingira mazuri yaliyoletwa na 4R kupitia serikali ya Umoja wa Kitaifa GNU, sana nchi ina nafasi ya kutumia viongozi wa vyama vingine vya kisiasa katika kulitumikia taifa ktk nafasi za kiuongozi na hivyo nchi kufaidika na kila raia aliye na upana wa maono bila kujali wametoka vyama vingine.

Tofauti na kama ingekuwa utawala wa kimabavu, kuzuia raia kufikia nafasi za kiuamuzi kupitia kura walizopata baada ya kuaminiwa na wapiga kura waliowacgagua katika uchaguzi ulio wazi, huru na wa haki kuanzia ngazi ya mchakato wa mikutano ya vyama vyao, kampeni hadi kutangazwa wameshinda.
Source: SABC News

CCM watambue kuwa uchaguzi ulio huru na haki una manufaa makubwa mtambuka, badala ya wao chama dola kongwe kufikiria jambo kubwa ni kuingia ofisini kwa uchaguzi usio wa haki, ulioporwa kwa hila kama ule wa 2019, 2020 kurudiwa tena 2024 na 2025 serikali itakayoingia madarakani kupitia uchaguzi fiche wa hila itapata tabu siyo tu kutoka kwa raia tu bali nchi kukosa maendeleo.
 
Nazungumzia vyama vya siasa nchini gentleman,

na kama wewe ni mpiga kura usiejitambua, na usie ona umuhimu wa uchaguzi huu muhimu sana wa serikali za mitaa, tulizana nyumbani, waTanzania wengine wazalendo watakuwakilisha, usiwe na makasiriko tulizana tuli 🐒
Narudia tena, hivyo vyama vya siasa hata kujiandaa ni kupoteza muda, matokeo tayari yameshapangwa na ccm.
 
Novemba 27 nitakuwa kwenye mihangaiko ya kuwatafutia wanangu mkate!
Ni upuuzi mtupu!
Nitasikilizia matokeo kwenye TV!
Ni muhimu sana kua mtulivu,
CCM na wazalendo wengine kupitia serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi wetu makini na kipenz cha waTanzania Dr Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha mazingira yako ya kutafuta mkate huo kwa ajili ya wanao kua mazuri zaidi na ya amani ya uhakika zaidi 🐒
 
02 October 2024
Jimbo la Kibamba
Dar es Salaam, Tanzania

:FIRE:🅻🅸🆅🅴 : TUNDU LISSU ANANGURUMA MUDA HUU


View: https://m.youtube.com/watch?v=YWlRiTOLFXs
Miongozo ya waziri wa TAMISEMI kuchukua na kurudisha fomu, ni njama za kufanya wagombea kuenguliwa. Tundu Lissu awataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi tunataka fomu sasa hivi hatusubiri tarehe 1 November. Maana mitego ya waziri Mohamed Mchengerwa kusambaza taarifa potofu kuhusu uchaguzi wa November 2024 ni mingi wanaCHADEMA

Madudu mengine mengi ni pamoja na yafuayo...
 
Narudia tena, Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Na waTanzania wazalendo wanaendelea kukuonyesha vizuri sana kwamba bila hata wewe wanaweza kupiga kura kuunda serikali na kuongoza mitaa na nchi bila tashwishwi yoyote ile gentleman 🐒

ni kwamba uwepo, au usuwepo kwenye uchaguzi mambo ni Bam Bam yanasongo tu bila mbambamba yoyote 🐒
 
Back
Top Bottom