Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Vyama vingine baada ya wanachama wao kugoma kushiriki maandamano haramu yaliyopigwa marufuku na kudhibitiwa na polisi, wame nyong'onyea, wamesinyaa na wamekua kama wamepigwa ganzi hivi, Lakini pia ni kama wamepoteza uelekeo kabisa. Na kwasababu hiyo eti sasa wanalumbana washiriki au wasishiriki uchaguzi huo muhimu sana wa serikali za mitaa. Na mara nyingi matokeo ya malumbano yao huwaathiri woa wenyewe na wanachama wao.
Vyama vingine kwa uchache vinafanya mikutano ya hadhara kwa kusua sua, hawana ratiba ndefu za mbwembwe kama ilivyokua mara baada tu ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan kuruhusu mikutano ya hadhara na maandamano, baada ya mtangulizi wake hayati J.Magufuli kuzuia mambo hayo. Na ukifuatilia kwa karibu hakuna maandalizi ya uchaguzi huo muhimu sana wa serikali za mitaa badala yake ni muendelezo wa siasa za lawama na kulalamika tu bila kua na mbadala wa mipango mikakati ya malalamiko hayo. Bila shaka maandalizi ya zima moto yanatarajiwa.
Kwa hali hiyo,bila shaka yoyote, ukata wa fedheha, madeni ya kupindukia ndani ya vyama vya siasa yana chochea pakubwa maandalizi ya uchaguzi huo muhimu kwa kiasi hiki ambacho kinachoonekana bayana.
Kwa ujumla vyama vya siasa, vinapitia wakati mgumu zaidi kiuchumi kutokana na kutokua na mipango mikakati bora mbadala ya kiuchumi, na badala kutegemea michango ya wanachama, wadau, wafadhili na wafanyabiashara wenye maslahi ya kisiasa kwenye vyama hivyo..
Ukata wa fedha unaweza kuchochea baadhi ya vyama kutoshiriki uchaguzi huo muhimu kwa kisingizio cha kuzuiwa na polisi kufanya maandamano haramu, lakini pia hofu ya kushindwa kufanya kampeni, fedheha na aibu ya kushindwa vibaya sana na vyama vilivyo jiandaa vizuri sana kwa uchaguzi huo muhimu mathalani CCM n.k 🐒
Una maoni gani kwenye hilo?
Mungu Ibariki Tanzania