Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Katibu wa CCM Wilaya ya Rufiji Prudence Sempa amesema atalifanyia kazi Ombi la Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rufiji la kuwataka kumpitisha Mbunge Mohamed Mchengerwa kuwa Mgombea pekee wa Ubunge kupitia CCM.
Bw. Sempa alitoa kauli hiyo baada ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rufiji Abdul Chobo kukitaka Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya kuitisha Mkutano Mkuu wa wanachama na kuangalia vifungu vya katiba vinasemaje ili waweze kumpitisha Mbunge wa sasa wa Rufiji Mohamed Mchengerwa kuwa Mgombea pekee na Rasmi kupitia CCM kwa Jimbo la Rufiji.
Kombo ambaye pia ni moja wa Madiwani aliibuahoja hiyo leo katika Maadhimisho miaka 48 ya CCM yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Tanki mbili katika Wilaya ya Rufiji.
==
Maoni ya mdau

Kitendo walichokifanya ccm kule Dodoma cha kumpitisha mgombea wa nafasi ya Urais kinyume cha utaratibu kimeweka msingi mbovu sana na wasipoangalia utatokea mgogoro mkubwa sana huko majimboni kama ambavyo huko Rufiji walivyoanza na wakiacha tu hilo jambo litokee huko Rufiji basi wajue wengine watafuata na haitawezekana kuwazuia maana watasema kama Rufiji imewezekana kwanini wao wazuiwe.
Wapunguze tamaa ya madaraka wanajitia aibu tu.
Na inadhihirisha kuwa ccm sasa imekufa rasmi hawana ubunifu tena.