Dogo1,
Tetty,
Kobello,
Nguruvi3,
Ritz
Mapendekezo ya CCM kuhusu rasimu ya pili ya Katiba pamoja na mchanganuo wa kero zilizopo ndani ya muungano na tiba zake yaliwasilishwa na Asha Migiro kwenye kikao cha NEC mwishoni mwa mwezi February, 2014. Wanaopinga hili waje hapa kutueleza vinginevyo.
Nguruvi3, hoja kuhusu wabunge wa Bara kuhisi yatima - mapendekezo ya CCM katika maboresho ya serikali mbili ni pamoja na uundwaji upya wa majimbo ya uchaguzi - ambayo yanaitwa "majimbo ya jamhuri ya muungano". Kwa upande wa znz, majimbo ya uchaguzi ya BLW yataendelea kuwa hayo hayo kama majimbo ya uchaguzi ya bunge la jamhuri ya muungano. Je, mabadiliko haya yataleta tofauti gani na hali ya sasa? Je tutakuwa na bunge la Tanzania bara na likafanya kazi kama bunge la wananchi wa Tanzania Bara? Bunge hili litafanyaje kazi bila ya serikali? Wananchi wa Bara wanashindwa kuelewa kwamba - hata kwenye halmashauri zao Songea, Mpanda, Rungwe, Karagwe, Biharamulo, Nzega, Newala, Hai, na kwingineko, kote huku pia kunakuwa na serikali. Madiwani husika hawawezi fanya kazi bila ya serikali. Hatuwezi kuwa na bunge la Tanzania Bara bila ya bunge hili kuwa na serikali yake - mawaziri na rais au waziri mkuu, vinginevyo ni kujenga migogoro na uhasama usio na sababu, na ni kupoteza fedha za walipa kodi kwani hakuna accountability.
Zipo taarifa kutoka ndani ya tume zinazosema kwamba baadhi ya viongozi wa ccm walipendekeza serikali mbili huku wakija na maboresho ambayo yatavunja muungano. Yet, ni hawa hawa ambao wanaona maboresho yao ni bora kwa muungano kuliko serikali tatu, na wanamshutumu warioba anavunja muungano. Rekodi zipo ndani ya tume kwamba viongozi kadhaa walipendekeza serikali mbili huku katiba ikifanyiwa mabadiliko - just to accommodate znz. Kwa mfano, walitaka:
1. Znz iwe na kiti chake UN. Hili moja kwa moja linavunja muungano.
2. Znz iwe na sarafu, jeshi, usalama wa taifa, polisi, rais wake kutambulika kama amiri jeshi mkuu. Haya yote yanavunja muungano.
Makada hawa wanaona mapendekezo yao ni bora kuliko serikali tatu. Na ni hawa ndio wamesaidia ile ripoti ya Asha Rose Migiro ije na mapendekezo tuliyojadili.
MAKOSA YA TUME: CCM INATAFUTA TU PA KUJIFICHA
Tukirudi nyuma kidogo, mjadala wa muundo wa muungano uliingizwa kwenye sheria ya muswada wa sheria ya kuundwa kwa tume ya katiba kwa sababu mbili:
Kwanza - mabadiliko ya katiba znz (2010) yalileta athari ya moja kwa moja juu ya muundo wa muungano. Kwa mfano, znz ikatambulika kama nchi yenye mipaka yake, wimbo wa taifa, bendera yake na vikosi vyake vya ulinzi na usalama. Kufuatia mabadiliko haya, ndio maana ikaja serikali ya umoja wa kitaifa. Hili halipo kwenye katiba ya JMT (1977) ambayo CCM inataka "iboresha".
Pili, mjadala juu ya muundo wa muungano haukuja na matakwa ya watawala. Tuliwasikia Jaji Werema, Celina Kombani (akiwa waziri wa sheria na katiba) wakisema hatuna haja ya katiba mpya. Lakini hali ikabadilika pale wazanzibari walipogoma mbele ya Samuel Sitta na kuchoma waraka ule moto kwa kudai suala la muundo wa muungano lazima lijadiliwe.
Sasa Jaji warioba analaumiwa kwa lipi? Tume yake imekoosea wapi? Kwa kweli kwa hili, CCM na viongozi wake wanaionea tu tume, wanatafuta mahali pa kusukumia lawama, basi. Na ipo siku wananchi amba leo hawaoni hili, watakuja ona ukweli upo wapi, kwani historia ndio inaandikwa...
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums