Wana jamvi,
Chini ya Serikali mbili zitakazoboreshwa na CCM, yafuatayo hayatabadilika:
1. Zanzibar kuwa ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano. Hii ni kinyume cha katiba ya muungano (1977) ambayo CCM inasema inataka "iboresha".
2. Zanzibar imechukua madaraka ya muungano ikiwa ni pamoja na kuelekeza sheria zote zinazopitishwa na bunge la jamhuri ya muungano kwanza zipelekwe kwenye baraza la wawakilishi.
Now we have a double edged sword situation: upande wa kwanza - kwa Zanzibar ilipofika, haiwezi tena kurudi ilipotoka (pre - 2010 constitution); na upande wa pili, kuiacha Zanzibar kama ilivyo (post – 2010), chini ya kinachoitwa ni maboresho ya serikali mbli, maana yake ni kwamba Zanzibar sasa itakuwa juu ya Katiba ya jamhuri ya muungano.
Awali tulijadili juu ya mapendekezo ya CCM ya kuanzisha kwa Bunge la Tanzania Bara. Moja ya sababu za msingi za CCM kuja na pendekezo hili ni pamoja na kwamba – tumefikia mahali sasa tutakuwa na wabunge kutoka nchi jirani ya Zanziar kuja kutunga na kupitisha sheria kwa masuala ambayo sio ya muungano, na yasiyo wahusu. Huku hakuna tofauti na kukubali umuhimu wa serikali tatu.
Inawezekana CCM imetambua kwamba, muda sio mrefu, haitaingia akilini mwa wananchi wa Tanzania Bara pale watakapogundua kwamba - sheria zinazotungwa na wabunge wa Muungano, kumbe pia washiriki wa utunzi huo ni watu ambao sheria hizo haziwagusi na wala haziwahusu kwa namna yoyote ile. Kwa maana nyingine, wabunge wa Zanzibar wanashiriki katika utungaji sheria zisizohusu muungano (zenye impact kwa Tanzania Bara). Sasa iwapo CCM inaona tatizo hili, hivyo kulianzishia bunge lake,bunge hili litafanyaje kazi bila ya kuwa na serikali yake? This is a timing bomb for CCM.
Wakiwa "off record", viongozi wengi wa CCM wanakiri kwamba Katiba ya Zanzibar na ya Muungano imejaa migongano mingi sana ambayo suluhisho lake haliwezi kuletwa na serikali mbili zilizoboreshwa bali serikali tatu. Pamoja na kuona ukweli huu, wakiwa bungeni Dodoma, "wanaufyata". Wanaogoa kupoteza vyeo, wakidhania vyeo hivi ni ajira na fursa za kuendesha maisha yao wakati kimsingi, ubunge ni dhamana tu, hakuna lingine lolote.
Tukiendelea na hoja yetu juu ya mgongano baina ya katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar:
Ibara ya (1) ya mkataba wa muungano (1964) ilianisha wazi kwamba Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa NCHI MOJA yenye MAMLAKA MOJA YA KIDOLA. Vile vile, ibara ya (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977) inatamka kwamba Jamhuri ya Muungano ni NCHI MOJA. Wajumbe wa NEC wakikaa ndani kama chama, wanajadili kwa uwazi kabisa kwamba kwa katiba ya Zanzibar kutamka kwamba Zanzibar ni nchi, huku ni kukinzana na Katina ya JMT (1977) inayosema kwamba Jamhuri ya Muungani ni NCHI MOJA NA DOLA MOJA.
Wajumbe wa NEC (CCM), wakiwa ndani ya vikao vyao, wanakiri wazi kwamba – ibara ya (147) ya Katiba ya JMT imekataza mtu yeyote au shirika au kikundi chochote kuunda jeshi katika jamhuri ya muungano wa Tanzania, isipokuwa serikali (cc
Pasco). Pamoja na mamlaka hayo kujulikana kwa mujibu wa sheria ndani ya Katiba ya Muungano, bado Zanzibar imejiundia majeshi yake ya ulinzi. In private, viongozi wengi wa CCM wanakiri wazi kabisa kwamba hii ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Tukiangalia kwa undani juu ya mgongano wa utungaji wa sheria, Zanzibar pia imenyofoa mamlaka ya muungano katika suala hilo (cc
Pasco). In private, Viongozi wengi wa CCM wanakiri wazi kwamba ibara ya 64(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatoa mamlaka kwa Bunge la Muungano kutunga sheria ambazo zinaweza kutumika hadi Zanzibar. Lakini Katiba ya Zanzibar kupitia ibara ya 132(1), inaweka masharti ya kutumika sheria iliyotungwa na bunge la muungano na kutamka kwamba sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya muungano pekee, na sio vinginevyo. Katika ufafanuzi wake, ibara ya 132 (2) ya Katiba ya Zanzibar inafafanua kwamba sheria hiyo lazima ipelekwe kwenye baraza la wawakilishi na waziri anayehusika.
Pia upo mgongano unaohusu mahakama ya rufani ya Jamhuri ya Muungano. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hii ni mahakama yenye uwezo wa kuamua rufaa zote nchini – Tanzania Bara na Zanzibar. Lakini tukiangalia kwa upande wa Zanzibar - masuala yote yanayohusiana na dini ya kislamu ambayo yanahusika na mahakama ya kadhi Zanzibar, na mambo mengine yote yaliyoainishwa katika katiba ya Zanzibar pamoja na sheria nyingine yeyote iliyotungwa na baraza la wawakilishi yanazuiwa kupelekwa kwenye mahakama ya rufaa na katiba ya sasa ya Zanzibar.
Pia upo mgongano juu ya mamlaka baina ya Rais wa Muungano na Yule wa Zanzibar. Tukiangalia ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ibara hii inampa rais wa muungano mamlaka ya kugawa mikoa nchini. Wakati huo huo, Katiba ya Zanzibar pia imetoa mamlaka kama hayo kwa Rais wa Zanzibar.
Vilevile, ibara ya 34 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano (1977), inaweka wazi masuala ambayo serikali ya muungano itakuwa na mamlaka nayo huku pia ikifafanua masuala ambayo serikali ya muungano ina mamlaka nayo. Lakini cha kushangaza, serikali ya muungano haikuweka wazi mipaka yake ni ipi; haikuweka ni wakati gani itasimamia mambo ya muungano, na wakati gani itasimamia mambo yasiyo ya muungano (yani ya Tanzania Bara). Hiki ndio kiini cha hoja kwamba Tanganyika imevaa koti la muungano, na kwamba Tanganyika inatumia mamlaka haya kujinufaisha yenyewe kwa gharama za Zanzibar.
Mengi ya matatizo haya ni mambo ya KISHERIA NA KIKATIBA. Suluhisho lake haliji kwa kukumbushana kwa maneno mazuri na matamu juu ya historia ya muungano wetu, au jinsi gani waasisi walivyojitolea kutuunganisha, au jinsi gani pande mbili za muungano zinavyoishi kwa pamoja. Badala yake, Suluhisho la haya yote lazima liwe ni la KISHERIA NA KIKATIBA.Basi! Iwapo kweli tuna nia ya dhati ya kulinda muungano, nasi ufumbuzi wa mattaizo haya ni kuzinduliwa kwa Serikali ya Tanganyika ili sasa kila upande wa muungano uwe na mamlaka kamili ya kujiendeshea mambo yake nje ya muungano, na kuchangia katika yale machache tu ya muungano kama rasimu ya katiba inavyopendekeza.
Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.