Dr. Mdondoaji:
Unajaribu sana kujenga hoja juu ya numbers na kutumia hoja hiyo kutafuta ushindi wakati kama wewe kweli ni PhD holder, majadiliano sio kutafuta ushindi bali kuelimishana, kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu.
Nadhani sasa ni muhimu for me to explain to you why I don't want to deal with numbers as a starting point, pamoja na wewe kushinikiza sana kwamba Numbers should be the starting point, huku ukija na hoja kwamba nyinyi wachumi mnaamini katika "no facts, no right to speak".
Dr:
Napingana na wewe kuja copy and paste ya bajeti kama framework of analysis to determine mfumo upi wa serikali ni bora for our union. Hii ni kwasababu, nikiazima maneno yako hapo juu , naunga mkono hoja lakini kuna kitu muhimu zaidi, ninacho amini kama mwananchi wa Kijiweni, nacho ni kwamba:
Nikuulize:
Do you know how our most important truth that has been ignored for the last 50 years? Jibu ni kwamba - a lot of it, na ndio maana tunaoitwa "maoni ya wachache" tunajaribu kutumia fursa iliyopo to rectify tatizo lililopo. Lakini kikwazo kikubwa ni kwamba wanaojiita "maoni ya wengi" wanajaribu kuboresha tatizo kupitia serikali tatu, sio kutatua tatizo (rejea mabandiko yangu mwanzoni mwa uzi huu). Kinachoshangaza zaidi ni kwamba, for 50 years, tumegundua serikali mbili hazitufai. Badala ya kuwa na consensus kwamba two subnational governments with fiscal autonomy are inevitable, PhD holders kama Dr. Mdondoaji wanashauri jibu ni serikali moja. Hawa wapo out of touch completely kwani the zanzibar question (1984, 2010), has been all about autonomy and self determination kwa sababu ya mfumo wa serikali mbili. Serikali moja sasa ya nini tena???
Dr. mdondaji pamoja na wanasiasa wetu wana tabia to "over use") statistics, figures, na hilo ndio limekuwa linaendelea katika mfumo wetu wa bajeti na uchumi kwa ujumla. Mnafanya kama vile - it's for anyone who ‘doesn't believe it until they see the numbers'.
Ukiwa kama mchumi, ulitakiwa uelewe kwamba huwa pia kuna a false correlation between ‘numbers' and ‘evidence'. Baadae nitakuonyesha jinsi gani this conflation undermines trust and na pia jinsi gani inapelekea to less-than-honest results, kwa kutumia namba zako hizo hizo za copy and paste.
Tatizo la msingi with numbers halipo katika numbers, per se; tatizo ni where numbers fall in our order-of-operations. Wanasiasa wetu (including you Doctor), mnazitazama numbers kama vile "they are an end point", "they are the holy grail of research and analysis". Kwa miaka 50, matokeo yake yamekuwa ni nini nchini? Halafu mnasema jibu ni serikali mbili au moja????
Nilichojadili #108 ni kujenga hoja kwamba numbers aren't the end to themselves kama wewe na kina Mwigulu mnavyotaka tuaminisha kwa kuchukua bajeti na kuichambua kwa miwani ya mbao. Badala yake,
numbers zinatakiwa kuchukuliwa as a step along the journey towards a better understanding. Ni bahati mbaya sana wewe, mwigulu, "@mwanadiwani" na wengine mnajaribu kufanya numbers kuwa ni
"An end". Katika muktadha huo, ndio maana hamuishiwi na pressure ya kuzichakachua, fiddle them, reconfigure them, ili mradi tu numbers zikidhi matakwa yenu. Ndio maana katika mchezo wa numbers hizo za bajeti, tena ambazo hazina input ya wananchi, hautanipata n'go. Call me foolish or whatever.
As much as you might like to pretend, and even force us kwamba hizo numbers represent "an infallible scientific rigor", tupo wachache wenye uzoefu ambao tunajua fika kwamba hata a figure ambayo may not look as a significant, kwa mfano 0.00000000000000000000000000000000000001, bado namba hii has an interpretive flexibility, hasa kama unaihitaji kuchomeka maslahi ya kisiasa kama yenu.
Kuwa na subira, uzi wa gharama utakuja tu dr Mdondoaji. Iwapo nimekuja na threads nyingi tu (visit my profile), hii ya gharama kwanini inishinde. Yote uliyogusia hapo juu nitayajadili. Sitaki kuja na vitu nusu nusu au kwa mtindo wa viporo. Nadhani umeona hata katika uzi huu, niliandaa kwanza content yote pembeni kisha nikaiweka katika mabandiko mbalimbali ili kuepuka unnecessary interruptions.
Until then, ujue tu kwamba mimi sio msomi kama wewe, ni raia tu mwenye interest ya kujisomea masuala ya siasa, uchumi na kijamii - a reader in these areas. Na kila nikipata muda, nayachambua and share my ideas, hence jina la "mchambuzi".
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi kwanza nielewe sijaribu kutafuta mshindi nani kama nilivyosema mwanzo elimu haina mwisho na kila siku mawazo mapya yanasaidia kupanua mawazo. Niko zaidi kujadili issues na style ya kujadiliana ni kubadilishana mawazo na hivyo basi unaweza kuona labda nashindana ila I want to get the best from you.
Turudi katika hoja yako ni kweli namba zinafichaga saa zengine ukweli wa uhalisi uliopo katika mazingira. Ila pamoja kwamba namba zinaficha ukweli ila namba saa zengine zinatoa ukweli wa kinachoendelea. Bila ya namba hatuna mjadala kwasababu kama hesabu zinatupa picha hakuna tatizo sasa tunabishana nini wakati maisha yanaenda pasina kuwa tatizo.
Tuje katika hoja hii:-
Do you know how our most important truth that has been ignored for the last 50 years? Jibu ni kwamba - a lot of it, na ndio maana tunaoitwa "maoni ya wachache" tunajaribu kutumia fursa iliyopo to rectify tatizo lililopo. Lakini kikwazo kikubwa ni kwamba wanaojiita "maoni ya wengi" wanajaribu kuboresha tatizo kupitia serikali tatu, sio kutatua tatizo (rejea mabandiko yangu mwanzoni mwa uzi huu). Kinachoshangaza zaidi ni kwamba, for 50 years, tumegundua serikali mbili hazitufai. Badala ya kuwa na consensus kwamba two subnational governments with fiscal autonomy are inevitable, PhD holders kama Dr. Mdondoaji wanashauri jibu ni serikali moja. Hawa wapo out of touch completely kwani the zanzibar question (1984, 2010), has been all about autonomy and self determination kwa sababu ya mfumo wa serikali mbili. Serikali moja sasa ya nini tena???
Mfumo wa Serikali uliopo una matatizo mengi ila unatokana na muundo wa serikali zenyewe. Unfahamu kuwa muungano huu hakuwa na economical interest but rather ulikuja out of political interest . Political interest hii actually ndio msingi mkuu wa kuunganisha muungano huu. Sasa tulipoungana tukadharau economic interest na matokeo yao economic interest zikaja kufinyangwa ndani ya muundo wa ulioletwa na wanasiasa.
Before the union Zanzibar ilikuwa inamiliki hisa ndani ya benki kuu ya Afrika Mashariki. Na sarafu ya zanzibar ilikuwa ni 2.9 times stronger than sarafu ya Tanganyika, Uganda, Kenya kwasababu zanzibar uchumi wake ulikuwa stronger since 1698!!! Hivyo basi sidhani kama wazanzibari walikuwa na economic interest sana kujiunga na ndani ya East African Currency kama isingelikuwa kulazimishwa na Waingereza after overthrowing the Sultan of Zanzibar. Hata hivyo tulivyounganisha tukawa tushaunganisha currency mbili zenye nguvu tofauti kiuchumi. I am not sure kama wazanzibari wangelikubali hili kama wangeliulizwa.
Hivyo basi utaona malengo ya kuungana yalitokana purely na msukumo wa kisiasa ambao kimsingi hakuwa na factors zozote za kiuchumi. Ilitakiwa tuanze kuungana kwa kuwa mfumo sawa kibiashara (tariffs) ikisha tuende kwenye kuanzisha maeneo huru ya biashara (free trade zone), tuje kuanzisha mfumo sawa wa kodi na masoko na mwishoe tuwe na umoja wa kiuchumi. It is unfortunate Nyerere na mwenzie Karume hawakulifanya hilo.
Sasa tushaungana ni vipi tuyarekebishe? Utakuja kuona kuwa kwakuwa tushakaa katika ndoa hii miaka 50 hakuna haja tena ya kutafuta mke wa pili tukaanza kuunda nyumba imara. Kimsingi kwakuwa malengo yalikuwa kuungana basi tungeliunganisha mifumo yote tukawa nchi moja ili tuwe na mfumo imara wa kiutawala na kiuchumi. Intergovernmental policies whether fiscal or monetary inakuwa mara nyingi haiiishi migogoro. Hata marekani pamoja na uimara wake kiuchumi bado kuna kuwa na malalamiko ya chini kwa chini katika hizi fiscal and monetary policy. Tukianza kufikiria suala la autonomy of Zanzibar tutakuja kukwama kwasababu mfumo uliopo unawapa upendeleo maalum zanzibar na kulibebesha salaba kubwa Tanganyika. Zanzibar kama nilivyosema awali haijachangia muda mrefu katika mfuko wa muungano na imekuwa ikilibebesha jukumu hilo Tanganyika huku wakilalamika wanakandamizwa. Na kama alivyosema Nguruvi matumizi ya zanzibar ni karibia Billioni 700 au 650 wakati mapato yao ni Billioni 300 tofauti ya Billioni 350 inatoka Tanganyika na mikopo ambayo tanganyika inaidhamini.
Sasa tukiwa na serikali 3 swali la kujiuliza je hizi special favours zitaweza kuendelea? Na kama mzigo wa gharama sasa hivi ni mkubwa je ndani ya serikali 3 mzigo hautaongezeka? Kwanini basi tusieleke katika serikali moja ambapo hizi nafasi na madaraka yatapungua na Zanzibar isurrender her sovereignty to bara tukaendelea na mfumo mmoja wa maisha. Au swali gumu kwanini tusiuvunje muungano kila mmoja akaelekea upande wake wa maisha?