CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Dr. Mdondoaji:

Unajaribu sana kujenga hoja juu ya numbers na kutumia hoja hiyo kutafuta ushindi wakati kama wewe kweli ni PhD holder, majadiliano sio kutafuta ushindi bali kuelimishana, kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu.

Nadhani sasa ni muhimu for me to explain to you why I don't want to deal with numbers as a starting point, pamoja na wewe kushinikiza sana kwamba Numbers should be the starting point, huku ukija na hoja kwamba nyinyi wachumi mnaamini katika "no facts, no right to speak".

Dr:
Napingana na wewe kuja copy and paste ya bajeti kama framework of analysis to determine mfumo upi wa serikali ni bora for our union. Hii ni kwasababu, nikiazima maneno yako hapo juu , naunga mkono hoja lakini kuna kitu muhimu zaidi, ninacho amini kama mwananchi wa Kijiweni, nacho ni kwamba:

Nikuulize:

Do you know how our most important truth that has been ignored for the last 50 years? Jibu ni kwamba - a lot of it, na ndio maana tunaoitwa "maoni ya wachache" tunajaribu kutumia fursa iliyopo to rectify tatizo lililopo. Lakini kikwazo kikubwa ni kwamba wanaojiita "maoni ya wengi" wanajaribu kuboresha tatizo kupitia serikali tatu, sio kutatua tatizo (rejea mabandiko yangu mwanzoni mwa uzi huu). Kinachoshangaza zaidi ni kwamba, for 50 years, tumegundua serikali mbili hazitufai. Badala ya kuwa na consensus kwamba two subnational governments with fiscal autonomy are inevitable, PhD holders kama Dr. Mdondoaji wanashauri jibu ni serikali moja. Hawa wapo out of touch completely kwani the zanzibar question (1984, 2010), has been all about autonomy and self determination kwa sababu ya mfumo wa serikali mbili. Serikali moja sasa ya nini tena???

Dr. mdondaji pamoja na wanasiasa wetu wana tabia to "over use") statistics, figures, na hilo ndio limekuwa linaendelea katika mfumo wetu wa bajeti na uchumi kwa ujumla. Mnafanya kama vile - it's for anyone who ‘doesn't believe it until they see the numbers'.

Ukiwa kama mchumi, ulitakiwa uelewe kwamba huwa pia kuna a false correlation between ‘numbers' and ‘evidence'. Baadae nitakuonyesha jinsi gani this conflation undermines trust and na pia jinsi gani inapelekea to less-than-honest results, kwa kutumia namba zako hizo hizo za copy and paste.

Tatizo la msingi with numbers halipo katika numbers, per se; tatizo ni where numbers fall in our order-of-operations. Wanasiasa wetu (including you Doctor), mnazitazama numbers kama vile "they are an end point", "they are the holy grail of research and analysis". Kwa miaka 50, matokeo yake yamekuwa ni nini nchini? Halafu mnasema jibu ni serikali mbili au moja????

Nilichojadili #108 ni kujenga hoja kwamba numbers aren't the end to themselves kama wewe na kina Mwigulu mnavyotaka tuaminisha kwa kuchukua bajeti na kuichambua kwa miwani ya mbao. Badala yake,
numbers zinatakiwa kuchukuliwa as a step along the journey towards a better understanding. Ni bahati mbaya sana wewe, mwigulu, "@mwanadiwani" na wengine mnajaribu kufanya numbers kuwa ni
"An end". Katika muktadha huo, ndio maana hamuishiwi na pressure ya kuzichakachua, fiddle them, reconfigure them, ili mradi tu numbers zikidhi matakwa yenu. Ndio maana katika mchezo wa numbers hizo za bajeti, tena ambazo hazina input ya wananchi, hautanipata n'go. Call me foolish or whatever.

As much as you might like to pretend, and even force us kwamba hizo numbers represent "an infallible scientific rigor", tupo wachache wenye uzoefu ambao tunajua fika kwamba hata a figure ambayo may not look as a significant, kwa mfano 0.00000000000000000000000000000000000001, bado namba hii has an interpretive flexibility, hasa kama unaihitaji kuchomeka maslahi ya kisiasa kama yenu.

Kuwa na subira, uzi wa gharama utakuja tu dr Mdondoaji. Iwapo nimekuja na threads nyingi tu (visit my profile), hii ya gharama kwanini inishinde. Yote uliyogusia hapo juu nitayajadili. Sitaki kuja na vitu nusu nusu au kwa mtindo wa viporo. Nadhani umeona hata katika uzi huu, niliandaa kwanza content yote pembeni kisha nikaiweka katika mabandiko mbalimbali ili kuepuka unnecessary interruptions.

Until then, ujue tu kwamba mimi sio msomi kama wewe, ni raia tu mwenye interest ya kujisomea masuala ya siasa, uchumi na kijamii - a reader in these areas. Na kila nikipata muda, nayachambua and share my ideas, hence jina la "mchambuzi".

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi kwanza nielewe sijaribu kutafuta mshindi nani kama nilivyosema mwanzo elimu haina mwisho na kila siku mawazo mapya yanasaidia kupanua mawazo. Niko zaidi kujadili issues na style ya kujadiliana ni kubadilishana mawazo na hivyo basi unaweza kuona labda nashindana ila I want to get the best from you.

Turudi katika hoja yako ni kweli namba zinafichaga saa zengine ukweli wa uhalisi uliopo katika mazingira. Ila pamoja kwamba namba zinaficha ukweli ila namba saa zengine zinatoa ukweli wa kinachoendelea. Bila ya namba hatuna mjadala kwasababu kama hesabu zinatupa picha hakuna tatizo sasa tunabishana nini wakati maisha yanaenda pasina kuwa tatizo.

Tuje katika hoja hii:-

Do you know how our most important truth that has been ignored for the last 50 years? Jibu ni kwamba - a lot of it, na ndio maana tunaoitwa "maoni ya wachache" tunajaribu kutumia fursa iliyopo to rectify tatizo lililopo. Lakini kikwazo kikubwa ni kwamba wanaojiita "maoni ya wengi" wanajaribu kuboresha tatizo kupitia serikali tatu, sio kutatua tatizo (rejea mabandiko yangu mwanzoni mwa uzi huu). Kinachoshangaza zaidi ni kwamba, for 50 years, tumegundua serikali mbili hazitufai. Badala ya kuwa na consensus kwamba two subnational governments with fiscal autonomy are inevitable, PhD holders kama Dr. Mdondoaji wanashauri jibu ni serikali moja. Hawa wapo out of touch completely kwani the zanzibar question (1984, 2010), has been all about autonomy and self determination kwa sababu ya mfumo wa serikali mbili. Serikali moja sasa ya nini tena???

Mfumo wa Serikali uliopo una matatizo mengi ila unatokana na muundo wa serikali zenyewe. Unfahamu kuwa muungano huu hakuwa na economical interest but rather ulikuja out of political interest . Political interest hii actually ndio msingi mkuu wa kuunganisha muungano huu. Sasa tulipoungana tukadharau economic interest na matokeo yao economic interest zikaja kufinyangwa ndani ya muundo wa ulioletwa na wanasiasa.

Before the union Zanzibar ilikuwa inamiliki hisa ndani ya benki kuu ya Afrika Mashariki. Na sarafu ya zanzibar ilikuwa ni 2.9 times stronger than sarafu ya Tanganyika, Uganda, Kenya kwasababu zanzibar uchumi wake ulikuwa stronger since 1698!!! Hivyo basi sidhani kama wazanzibari walikuwa na economic interest sana kujiunga na ndani ya East African Currency kama isingelikuwa kulazimishwa na Waingereza after overthrowing the Sultan of Zanzibar. Hata hivyo tulivyounganisha tukawa tushaunganisha currency mbili zenye nguvu tofauti kiuchumi. I am not sure kama wazanzibari wangelikubali hili kama wangeliulizwa.

Hivyo basi utaona malengo ya kuungana yalitokana purely na msukumo wa kisiasa ambao kimsingi hakuwa na factors zozote za kiuchumi. Ilitakiwa tuanze kuungana kwa kuwa mfumo sawa kibiashara (tariffs) ikisha tuende kwenye kuanzisha maeneo huru ya biashara (free trade zone), tuje kuanzisha mfumo sawa wa kodi na masoko na mwishoe tuwe na umoja wa kiuchumi. It is unfortunate Nyerere na mwenzie Karume hawakulifanya hilo.

Sasa tushaungana ni vipi tuyarekebishe? Utakuja kuona kuwa kwakuwa tushakaa katika ndoa hii miaka 50 hakuna haja tena ya kutafuta mke wa pili tukaanza kuunda nyumba imara. Kimsingi kwakuwa malengo yalikuwa kuungana basi tungeliunganisha mifumo yote tukawa nchi moja ili tuwe na mfumo imara wa kiutawala na kiuchumi. Intergovernmental policies whether fiscal or monetary inakuwa mara nyingi haiiishi migogoro. Hata marekani pamoja na uimara wake kiuchumi bado kuna kuwa na malalamiko ya chini kwa chini katika hizi fiscal and monetary policy. Tukianza kufikiria suala la autonomy of Zanzibar tutakuja kukwama kwasababu mfumo uliopo unawapa upendeleo maalum zanzibar na kulibebesha salaba kubwa Tanganyika. Zanzibar kama nilivyosema awali haijachangia muda mrefu katika mfuko wa muungano na imekuwa ikilibebesha jukumu hilo Tanganyika huku wakilalamika wanakandamizwa. Na kama alivyosema Nguruvi matumizi ya zanzibar ni karibia Billioni 700 au 650 wakati mapato yao ni Billioni 300 tofauti ya Billioni 350 inatoka Tanganyika na mikopo ambayo tanganyika inaidhamini.

Sasa tukiwa na serikali 3 swali la kujiuliza je hizi special favours zitaweza kuendelea? Na kama mzigo wa gharama sasa hivi ni mkubwa je ndani ya serikali 3 mzigo hautaongezeka? Kwanini basi tusieleke katika serikali moja ambapo hizi nafasi na madaraka yatapungua na Zanzibar isurrender her sovereignty to bara tukaendelea na mfumo mmoja wa maisha. Au swali gumu kwanini tusiuvunje muungano kila mmoja akaelekea upande wake wa maisha?
 
Kama tulivyotabiri, mheshimiwa MwanaDiwani ametukimbia. Ana lundo la hoja za kujibu kutoka kwa wadau, hasa Nguruvi3. Next time tunamuona active in JF pengine ni katika majukwaa ya siasa akiweka picha za makada wa ccm wakipokewa uwanja wa ndege kwa ngoma na nyoka, akijenga hoja kwamba 'hakuna kama CCM, CCM ni nambari wani, chama kinachanja mbuga, vyama vingine ni vya kilaghai, vyama vingine ni vya kifamilia'. Anasahau kwamba taifa hili limeishia kwa ulaghai kwa miaka 50 (cheti cha kuzaliwa muungano kimechakachuliwa); na suala la familia CCM, ndio usiseme kabisa.

Sera ya JF ya kulinda identity ina umuhimu wake, lakini pia ina mapungufu yake kwa vile inatufanya wengi wetu tuwe kama tunaongea na "majini". Inawezekana isiwe na shida katika masuala mengine lakini ni tatizo iwapo inahusisha masuala ya kitaifa, hasa iwapo wahusika ndio decision makers wa maisha ya wananchi milioni 45.

Na misukule ya Lumumba ndio inatumia fursa hii kuleta porojo za nguvu ya giza humu. Lakini wana haja ya kujificha kwani kama wanaojitokeza, hoja zao ndio zile za kina nape, lemutuz, makonda, kigwangalla, tutarajie kitu gani zaidi.

Kilicho Muhimu ni kwamba, Tanganyika inarudi, hata kama sio kesho, na wale wasaliti wote hawatakuwa na nafasi katika ujenzi wa Tanganyika yetu kwani wakipewa nafasi, wataenda kuivuruga ili ionekane ni "failure". Misukule itafanikiwa kupenya penya kwani unafiki wao unawa ficha. Lakini haitachukua muda mrefu kabla na wao kugundulika na watanganyika. Nao watang'oka tu.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi,

Pamoja na kuipenda Tanganyika na kusema itarudi ni vema kutafakari haya:-

a. Ni Tanganyika ipi ungelipendelea irudi kwani historia inasema vyenginevyo pamoja na sheria na hansard za kimataifa. Nikustue tu kwani kabla ya mapinduzi Sheikh Ali Muhsin Barwani aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Zanzibar alipeleka case Umoja wa Mataifa kutaka Zanzibar irudishiwe ukanda wake wa kilometa 10 kutoka Kenya, Tanganyika na Mozambique. Je unafikiria ni kwasababu gani?

b. Uwepo wa Tanganyika lazima uwe unajustification ya sheria ya jamii grund norm kuwa wananchi waliopo bado wanahitaji uwepo wa Tanganyika na sheria zinaonyesha uwepo wa kuwepo Tanganyika ilishakufa ilipoletwa katiba ya Tanzania. Kwa kutumia grund norm utaona kwamba Tanzania ndio iliyopo na sio Tanganyika. Saa zengine huwa nawashangaa watu wanaopigia kelele hati ya muungano wakati kama katiba ilishatungwa hati haina umuhimu tena.

Kimsingi kurudisha Tanganyika sio kama ina umuhimu ila kama inao basi kama tunautaka muungano then tuipe mamlaka makubwa serikali ya JMT vyenginevyo hapa muungano haupo bali tunadanganyana au tuelekee katika muundo wa serikali moja tu.
 
Nimeshanga saaana. Nimerejea maandiko yako ya nyuma, wewe ni muumini wa znz huru. Ulishawahi kutetea S3.
sijui kipi kimekusibu ukakata kona bila indicator.

S1 haiwezekani kwasababu kuna Uzanzibar ambao ni bora.
Kama hawawezi kurkrbisha katiba ya 2010 watawezaje ku surrender soreignity yao?

Uwepo wa S3 unatoa fiscal autonomy ili znz irudi kuwa na uchumi imara kabla ya mapinduzi.
Unatoa nafasi ili Tanganyika nayo itue zigo la gharama lisiloihusu.

Kama nitakuelewa, tukiwa na S3 ile ya shirikisho ndiyo tutahudumia. Hizo nyingine kila mtu atabeba mzigo wake.
Hakuna sababu za kusema gharama za S3 zitakuwa kubwa kwa ujumla. Ukubwa utatoka wapi?

Mfano, znz wakiamua kuwa na wizara 2 na Tanganyika 50 hilo linawaathiri vipi nchi washirika?
Hatuwezi kusema tuna jumla ya wizara 52 na 7 za shirikisho hivyo 59. Ni upotoshaji
Muhimu ni mambo 7 ambayo tutachangia, kwingine ni kila mtu na nyumba yake.

Nikupe mfano, ukiwa na familia yako nami nina yangu, tukaamua kuwa na shamba la pamoja interest zetu zitakuwa katika shamba la pamoja, kukodi matrekta na mbolea tu. Masuala ya watoto wako au wangu wanavaa nini na wanakula nini ni yetu binafasi.
Hatuwezi kusema kwavile tunashamba la pamoja basi niingilie mambo yako ya ndani.

Nikiamua mke wangu atavaa gauni la dhahabu hilo ni shauri langu, na ukiamua kusomesha watoto wako oxford ni hilo ni shauri lako. Muhimu ni kuwa shamba letu tunalihudumiaje.

Ni kwa msingi huo Warioba akasema tuwe na mambo 7 tu, vibarua, matrekata, mbolea, soko la kuuza n.k.

Ni upotoshaji kusema shamba letu linahusu gharama za familia zetu.

Kama hatuwezi kuwa na shamba la pamoja, tupasue jahazi tugawane mbao.
 
Nguruvi,

Hilo silikatai nilitetea sana Zanzibar huru na nikatoa evidence nyingi za kuwa zanzibar ilikuwa na mafanikio kiuchumi before union. Ila nawaogopa wanaotetea zanzibar huru sasa na pia unafiki wa wanaotetea zanzibar huru sasa hivi. Kakisome kitabu cha Maalim Seif kuhusu maisha yake na aliyayafanya dhidi ya Aboud Jumbe. Utagundua kwanini naogopa kwasababu kama aliweza kumsaliti Aboud Jumbe mtu aliyemleta katika ulimwengu wa siasa atashindwa nini kuwasaliti wazanzibar ambao anawapeleka anavyotaka yeye mwenyewe.

Tuje katika hoja ya serikali 3 pamoja na hoja zako nyingi nzuri ila fahamu kuwa tuna mambo saba tutakuwa tunashirikiana katika serikali ya muungano. Hata hivyo Nguruvi fahamu kuwa serikali hii ya muungano itakuwa haina rasilimali wala vyanzo vya mapato. Na kama vyanzo vya mapato vinatoka kwa washirika ni wazi washirika watakuwa wamekubali vyanzo hivyo viende serikali ya muungano. Sasa changamoto inakuja pale vyanzo hivyo vinabeba asilimia kubwa ya mapato kutoka kwa washirika na washirika wakawa hawana njia nyengine ya kuongeza mapato mnafanyaje?

Au tukirudi katika mfano wako wa ujirani tunashirkiana ndio katika shamba lakini wewe ukikodi trekta mie naleta wakulima au mashine ya kupalilia. Wewe ukileta seeds mie naleta makapu ya kuvuna. Sasa kama sisi majirani wewe ukatoa trekta na mie nikawa sitoi kitu halafu wakati wa mavuno nikaleta kapu langu nivune swali ni je utanipa mazao yako?

Na kama hatuwezi kushirikiana tukagawana mbao kwanini tusigawane mbao sasa tukawa tu majirani wema maisha yakaendelea ? Tukaja kuunda ujirani hapo baadae tukiona umuhimu wa kufanya hilo baadae. Hii ni kwasababu kila mmoja atajua weakness na strength zake na pengine tutakuwa na ushirikiano imara kuliko huu wa kukurupuka na mwisho tukaishia kukimbiana?
 
Sasa mkuu, hilo ni kosa la tume ambayo unasema haina makosa au serikali au CCM?
Maana unasema huoni kosa la tume wakati huohuo unaishutumu kwa kuwabana watoa mawazo .... sasa tukuelewe vipi? Kwamba labda kulikuwa na watu wengi waliotaka kuunga mkiono serikali moja wakazuiwa au?

Ili tusiende mbali sana, mimi nimeangalia post nyingi sana kuhusu muundo wa serikali za muungano na sijaona mtu yeyoite aliyekuja na kutuelezea uhalali wa kutokuhusisha asilimia 80 ya wasiotoa maoni kuhusu muungano, labda ungenipa link ila nitajaribu kuitafuta.
All in all, kuna propaganda nyingi mno humu JF ambazo msingi wake kwa kweli hata siuelewi na mara nyingi nikitaka kuuliza undani wake, majibu huwa mafupi na sometimes ni kama mtu unalazimishwa ukubaliane na maelezo ya watu fulani hata kama basis ya maelezo hayo haieleweki.

Kwa mfano, sijasikia bungeni CCM wakija na hoja ya bunge la Tanzania bara/tanganyika, sijasikia kuhusu zanzibar kupewa kiti UN,
Sijasikia rais Kikwete akisema jeshi litachukua nchi kama kutakuwa na serikali tatu, ila labda kuna goals zinazotakiwa kuwa reached and im standing on the way. Sijasikia wala kuona mahali popote takwimu za tume ya Warioba zikiwajumuisha watanzania ambao hawakutoa maoni yao kuhusu muundo wa muungano na maelezo kwanini wasijumuishwe.

Kama hata hujasikia Rais Kikwete akisema kuwepo kwa serikali tatu kutasababisha Jeshi kuasi /kuchukua nchi basi kalale au la unafanya makusudi kutaka kutupoteza!
 
Kama hata hujasikia Rais Kikwete akisema kuwepo kwa serikali tatu kutasababisha Jeshi kuasi /kuchukua nchi basi kalale au la unafanya makusudi kutaka kutupoteza!
Kilichozungumzwa ni ukosefu wa fedha za kuiendesha serikali ya jamhuri ya muungano.
Ndiyo ukatolewa mfano, kama jeshi halitalipwa litaweza kuchukua nchi. Ni moja ya mifano ya serikali kushindwa kujiendesha. Sasa nyie mnakuza kuwa kasema direct kuwa kukiwa na serikali tatu basi jeshi litapindua nchi ... thats absurd.
Quote maneno hayo kwenye hotuba, uturushie humu, acha kufuata mkumbo.
 
Mdondoaji,

Yah:Bandiko lako #186

Hoja kuhusu serikali ya muungano kukosa mapato ni hoja ya kisiasa kuliko kiuchumi. Awali nilieleza kwamba katika masuala ya public finance, ambapo key variables to mapato (kodi) na matumizi (recurrent expenditures and investments), yapo maeneo ambayo serikali kuu (ya muungano) ipo more competent lakini yapo maeneo ambayo serikali kuu sio competent, na badala yake serikali shiriki. Nipo mbali kidogo, nikirudi nitakupa mifano ya kodi zipi serikali kuu ipo more competent to deal with, na it brings overall efficiency katika uchumi na sehemu zipi haipo competent na haileti overall efficiency kuliko kodi hizi zikiwa mikononi mwa serikali shiriki. Same applies to matumizi, yapo maeneo ambayo serikali kuu ipo more competent na inaleta more efficiency, lakini pia yapo maeneo ya matumizi ambayoo yakiachiwa kwa serikali shiriki, ni more efficient kwa vile hizi zipo more competent. Nilijadili hili #108 , nikielekeza hoja hii kwako binafsi.
Kazi ya bunge la katiba ni pamoja na determination ya hizi competencies baina ya serikali kuu serikali shiriki, na kuziweka sawa, sio kulalama tu na kujadili bajeti za kila mwaka na jinsi gani zimejaa constraints. Kwa kiasi kikubwa sana, bungeni mle hakuna wataalam na kama wapo basi wapo over consumed na siasa.

I keep on repeating myself kwamba naweka uzi sawa juu ya haya then nitawasilisha, niwie radhi kwa hilo. Ila kwa sasa hata kama bandiko #108 halikuvutii, naomba kwa sasa liwe indicative tu juu ya tuna maana gani serikali tatu ni more desirable in terms of gharama, lakini pia, in terms of outcome za kodi na matumizi kwa wananchi. Nguruvi3 anagusia hili pia hapo juu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi,

Hilo silikatai nilitetea sana Zanzibar huru na nikatoa evidence nyingi za kuwa zanzibar ilikuwa na mafanikio kiuchumi before union. Ila nawaogopa wanaotetea zanzibar huru sasa na pia unafiki wa wanaotetea zanzibar huru sasa hivi. Kakisome kitabu cha Maalim Seif kuhusu maisha yake na aliyayafanya dhidi ya Aboud Jumbe. Utagundua kwanini naogopa kwasababu kama aliweza kumsaliti Aboud Jumbe mtu aliyemleta katika ulimwengu wa siasa atashindwa nini kuwasaliti wazanzibar ambao anawapeleka anavyotaka yeye mwenyewe.

Tuje katika hoja ya serikali 3 pamoja na hoja zako nyingi nzuri ila fahamu kuwa tuna mambo saba tutakuwa tunashirikiana katika serikali ya muungano. Hata hivyo Nguruvi fahamu kuwa serikali hii ya muungano itakuwa haina rasilimali wala vyanzo vya mapato. Na kama vyanzo vya mapato vinatoka kwa washirika ni wazi washirika watakuwa wamekubali vyanzo hivyo viende serikali ya muungano. Sasa changamoto inakuja pale vyanzo hivyo vinabeba asilimia kubwa ya mapato kutoka kwa washirika na washirika wakawa hawana njia nyengine ya kuongeza mapato mnafanyaje?

Au tukirudi katika mfano wako wa ujirani tunashirkiana ndio katika shamba lakini wewe ukikodi trekta mie naleta wakulima au mashine ya kupalilia. Wewe ukileta seeds mie naleta makapu ya kuvuna. Sasa kama sisi majirani wewe ukatoa trekta na mie nikawa sitoi kitu halafu wakati wa mavuno nikaleta kapu langu nivune swali ni je utanipa mazao yako?

Na kama hatuwezi kushirikiana tukagawana mbao kwanini tusigawane mbao sasa tukawa tu majirani wema maisha yakaendelea ? Tukaja kuunda ujirani hapo baadae tukiona umuhimu wa kufanya hilo baadae. Hii ni kwasababu kila mmoja atajua weakness na strength zake na pengine tutakuwa na ushirikiano imara kuliko huu wa kukurupuka na mwisho tukaishia kukimbiana?
Nichangie hoja zako hasa ya gharama katika serikali ya shirikisho.
Kumekuwa na madai kuwa haitakuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato.

Nimemuuliza MwanaDiwani kwani sasa hivi vyanzo vya uhakika ni vipi? Nina maana kinachowezekana sasa hivi hakiwezi kushindikana katika kugawanya. Labda una mawazo tofauti kuhusu hili na ningekuomba unifahamishe. Kwani kwasasa ambapo tuna S2, JMT na SMZ na kama mada inavyosema 'zilizoboreshwa' vyanzo vya uhakika baada ya maboresho ni vipi?

Hapa ndipo nasema wanataka kutuuzia mbuzi katika gunia. Hawatuambii vyanzo vya uhakika vya Serikali 2 zilizoboreshwa, wanachotuambi ni hatari ya S3. CCM na washabiki wao kama akina MwanaDiwani walitakiwa watumie muda kutushawishi kwa hilo na si kutumia muda kumnanga mzee Warioba na tume.

Mzee Warioba na tume wamekuja na mapendekezo yao yanayokosolewa. Sasa mbadala wa mapendekezo yao ambao una usahihi katika S2 kuhusu vyanzo vya mapato uko wapi?
Mdondoaji hebu tuanzie hapa kwanza, kwa S2 Maboresho vyanzo vya uhakika vya mapato ya serikali kuu ya muungano ni vipi?
 
Nimeshanga saaana. Nimerejea maandiko yako ya nyuma, wewe ni muumini wa znz huru. Ulishawahi kutetea S3.
sijui kipi kimekusibu ukakata kona bila indicator.

S1 haiwezekani kwasababu kuna Uzanzibar ambao ni bora.
Kama hawawezi kurkrbisha katiba ya 2010 watawezaje ku surrender soreignity yao?

Uwepo wa S3 unatoa fiscal autonomy ili znz irudi kuwa na uchumi imara kabla ya mapinduzi.
Unatoa nafasi ili Tanganyika nayo itue zigo la gharama lisiloihusu.

Kama nitakuelewa, tukiwa na S3 ile ya shirikisho ndiyo tutahudumia. Hizo nyingine kila mtu atabeba mzigo wake.
Hakuna sababu za kusema gharama za S3 zitakuwa kubwa kwa ujumla. Ukubwa utatoka wapi?

Mfano, znz wakiamua kuwa na wizara 2 na Tanganyika 50 hilo linawaathiri vipi nchi washirika?
Hatuwezi kusema tuna jumla ya wizara 52 na 7 za shirikisho hivyo 59. Ni upotoshaji
Muhimu ni mambo 7 ambayo tutachangia, kwingine ni kila mtu na nyumba yake.

Nikupe mfano, ukiwa na familia yako nami nina yangu, tukaamua kuwa na shamba la pamoja interest zetu zitakuwa katika shamba la pamoja, kukodi matrekta na mbolea tu. Masuala ya watoto wako au wangu wanavaa nini na wanakula nini ni yetu binafasi.
Hatuwezi kusema kwavile tunashamba la pamoja basi niingilie mambo yako ya ndani.

Nikiamua mke wangu atavaa gauni la dhahabu hilo ni shauri langu, na ukiamua kusomesha watoto wako oxford ni hilo ni shauri lako. Muhimu ni kuwa shamba letu tunalihudumiaje.

Ni kwa msingi huo Warioba akasema tuwe na mambo 7 tu, vibarua, matrekata, mbolea, soko la kuuza n.k.

Ni upotoshaji kusema shamba letu linahusu gharama za familia zetu.

Kama hatuwezi kuwa na shamba la pamoja, tupasue jahazi tugawane mbao.
Judiciary? Bunge?
Mbona unagusia wizara 7 tu?
 
Uwepo wa Tanganyika lazima uwe unajustification ya sheria ya jamii grund norm kuwa wananchi waliopo bado wanahitaji uwepo wa Tanganyika na sheria zinaonyesha uwepo wa kuwepo Tanganyika ilishakufa ilipoletwa katiba ya Tanzania. Kwa kutumia grund norm utaona kwamba Tanzania ndio iliyopo na sio Tanganyika. Saa zengine huwa nawashangaa watu wanaopigia kelele hati ya muungano wakati kama katiba ilishatungwa hati haina umuhimu tena.

Articles of the union zilikuwa ni katiba ya kwanza ya muungano. Hati ikasema katiba ya kudumu itapatikana ndani ya kipindi cha mpito (mwaka mmoja) not later then April 25, 1965. Just a month before expiry date ya kipindi cha mpito (march 25,) suala hili la katiba mpya ya JMT likachakachuliwa. Nimejadili kwa kina kwenye uzi wangu titled "Siri ya hati ya muungano na njama za kuificha".

Kuna mtu, nadhani wewe awali ulisema kwamba muungano ulikuwa shwari wakati wa karume, na kwamba mgogoro ulianza after 1972. Hii sio sahihi. Hata Shivji anasema hivi (Let the people speak: Tanzania down the road to neoliberalism, page 90):

Karume however had no time for legal arrangements. He continued to exercise powers in complete disregard of the union matters. Karume declared that there would be no elections in Zanzibar for the next 50 years. Nyerere was exasperated but he could do little without pushing Karume out of the union.

Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi hapo juu, hasa in relation to hoja yako kwamba hakuna haja ya Tanganyika wala hati ya muungano tena kisheria kwa vile Katiba ya Muungano (1977) ilishapatikana, this is very misleading. Naomba ukasome uzi wangu nilioelekeza hapo juu. Katiba ya JMT haikuwa halali na bado sio halali. Uhalali wa awamu wa Mwalimu na pia baadae katika kutawala na kuendesha nchi haukutokana na katiba ya nchi bali legitimacy ilitokana na mengineyo - hasa mafanikio ya tanu kutetea wanyonge, mafanikio ya CCM kuunganisha historia za TANU na ASP, azimio la arusha na uadilifu na uzalendo wa Mwalimu. Haya yalifanya watanzania wasijali katiba inasema nini katika kutetea their political, social and economic justice kwani - why bother wakati azimio la arusha linatetea haki, usawa, linasimamia huduma kwa wananchi, linapinga ufisadi? Haya yote leo hakuna ndio maana legitimacy ya chama kushika nchi lazima itokane na katiba ya nchi. CCM sio wajinga kukubali mchakato 2010.

Mwisho, we have hardly undergone constitutionalism since 1964. Kwa maana hii, hoja kwamba Tanganyika haina uzito tena, na hoja kwamba katiba ya JMT imefanya suala la hati lisiwe na maana, ni upotoshaji to the extreme. Kwanini ccm inaificha ficha basi. Na kwanini tume ya katiba imependekeza makubaliano yale yawe ndio msingi wa muungano? Ni kwa sababu mkataba ule unaendelea kuwa ndio uhalali wa muungano over and above katiba ya JMT unayoijadili. Hata issa shivji anasema hivi katika kitabu tajwa hapo juu, page 94 kwamba):

If one was to judge by the standards of constituality, which are proclaimed today, our union has hardly had a constitutional government for the last 30 years. There were so many major breaches - including surreptitious manipulation of the constitution - that in reality, we did not live by our constitution. We even forgot to swear by it. We at the HILL, stopped teaching constitutional Law in 1971 or 1972.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mdondoaji,

Yah:Bandiko lako #186

Hoja kuhusu serikali ya muungano kukosa mapato ni hoja ya kisiasa kuliko kiuchumi. Awali nilieleza kwamba katika masuala ya public finance, ambapo key variables to mapato (kodi) na matumizi (recurrent expenditures and investments), yapo maeneo ambayo serikali kuu (ya muungano) ipo more competent lakini yapo maeneo ambayo serikali kuu sio competent, na badala yake serikali shiriki. Nipo mbali kidogo, nikirudi nitakupa mifano ya kodi zipi serikali kuu ipo more competent to deal with, na it brings overall efficiency katika uchumi na sehemu zipi haipo competent na haileti overall efficiency kuliko kodi hizi zikiwa mikononi mwa serikali shiriki. Same applies to matumizi, yapo maeneo ambayo serikali kuu ipo more competent na inaleta more efficiency, lakini pia yapo maeneo ya matumizi ambayoo yakiachiwa kwa serikali shiriki, ni more efficient kwa vile hizi zipo more competent. Nilijadili hili #108 , nikielekeza hoja hii kwako binafsi.
Kazi ya bunge la katiba ni pamoja na determination ya hizi competencies baina ya serikali kuu serikali shiriki, na kuziweka sawa, sio kulalama tu na kujadili bajeti za kila mwaka na jinsi gani zimejaa constraints. Kwa kiasi kikubwa sana, bungeni mle hakuna wataalam na kama wapo basi wapo over consumed na siasa.

I keep on repeating myself kwamba naweka uzi sawa juu ya haya then nitawasilisha, niwie radhi kwa hilo. Ila kwa sasa hata kama bandiko #108 halikuvutii, naomba kwa sasa liwe indicative tu juu ya tuna maana gani serikali tatu ni more desirable in terms of gharama, lakini pia, in terms of outcome za kodi na matumizi kwa wananchi. Nguruvi3 anagusia hili pia hapo juu.
Niwie radhi kidogo, nitatoka nje ya mada hata hivyo nikikimbia katika chaki ili kutopoteza maana iliyokusudiwa ya bandiko. Nimeguswa na la gharama nasubiri sana huo uzi mwingine.

Nichangie kuhusu effeciency
Mfano, Mwaka 2012/13 shirika la umeme znz (ZESCO)lilikusanya Ts Bilioni 20.
Pesa hizo zikaishia mikononi mwa wajanja, hakuna aliyechukuliwa hatua. Hizo ni pesa zilizopaswa kuingia katika SMZ ima kulipia deni au kwa mipango ya maendeleo.

Mwaka 2013, SMZ ikakosa bilioni 80 kukamilisha mradi wa umeme kutoka Tanga kwenda Pemba. Ikabidi iombe msaada wa bilioni 80 kutoka JMT ambao walipewa.

Hii maana yake ni mambo haya
1. Kwamba, kwavile SMZ inajua deni la umeme litasukumwa katika muungano haikujali kiasi gani kimepotea. Ndiyo maana hakuna hatua dhidi ya wezi, jambo linalosababisha inefficiency ya serikali kwa SMZ na JMT

2. JMT ililipa pesa za umeme wa Pemba kwasababu ni shamba la bibi.
Hivyo mwananchi wa Mtimbira akajikuta analipia umeme wa nchi jirani ya znz.

Tungekuwa nchi moja isingekuwa tatizo, tatizo ni kuwa znz ni nchi na kila kitu.
Kitendo cha kumlipisha gharama mwananchi wa Magoroto au Kicheba kwa gharama za ujenzi wa miundo mbinu inayokwena nje(export) ni kutotenda haki.
Ipo siku tutasikia Serikali ya JMT ikilipia umeme wa kwenda Malawi kwa gharama za mtu wa Isevya.

3. Kwavile hakuna Tanganyika, utendaji wa SMZ unakuwa dhifu.
Tegemeo lao ni shamba la bibi lisilo na mlinzi.

Laiti kungekuwa na serikali ya Tanganyika,ungekuwa wakati wa kusema, no! gharama za umeme kwenda nchi jirani tutakopeshana. Tunafanya hivyo na Kenya na nchi nyingine, isingekuwa taabu.
Serikali ya Tanganyika ingekuwa makini na rasilimali zake ambazo sasa hazina mlinzi.

4. Znz ilipotangaza bandari huru, bidhaa ziliingia kutoka znz bure.
Pesa na makusanyo mengine yalibaki znz tena mikononi mwa wahuni wa kizanzibar ambao leo wengine wanasimama majukwaani na kusema wananyonywa.

Tanganyika ikapoteza mapato sana kwasababu hakuna watch dog wa kuiambia SMZ izuie loophole za namna hiyo.

5. Mwaka 2010 znz imepoteza kiasi cha bilioni 20 kutoka mapato ya uwanja wa ndege na vyanzo vingine. Haikujali kufuatilia kwasababu yupo Tanganyika anayeziba pengo la bajeti.
Katika S3 hilo halitatokea na kutakuwa na efficiency katika ukusanyaji wa mapato.

6. Kwa upande wa Tanganyika, nayo imekuwa inapoteza kiasi kikubwa bila sababu.
Mwaka 2013 JMT ilitoa bilioni 32 kwenda ofisi ya makamu wa rais.

Pesa hizo hazikuwa na mchanganuo zitatumika wapi.
Huenda ndizo zinatumika kwa mambo ya kisiasa sasa hivi. JMT ambayo inagharamiwa na Tanganyika inapoteza fedha kwasababu hakuna audit ya pesa zinazokwenda znz.
A) Mwezi January Tanganyika imetoa bilioni 80 kwenda kujenga miundo mbinu ya umeme wa znz

Udhaifu wa SMZ ukazaa udhaifu wa Tanganyika na sote tukabaki kulaumiana.
Again, laiti kungekuwa na serikali ya Tanganyika ingekuwepo modality ya kuhakikisha kuwa wizi haufanywi kwasababu SMZ ingekuwa responsible na serikali ya Tanganyika pia.

Hii ni mifano ya kuonyesha kuwa S3 zinaongeza effeciency kuliko S2.
Serikali 2 basically ni moja ya SMZ. Ile ya JMT haiwezi kuwa kuwa ya pili, kwasababu ndiyo muungano. Ya pili ni Tanganyika inayogomewa kwasababu tu
 
Mradi wa umeme pemba umefadhiliwa na norway na finland.
Na ule wa zanzibar ni Millenium challenge.
But wat is 89billion? Wakati visa moja ya utaliii ni $100 na $ 50
Ni hizi miaka yote zinskusanywa na SMT ?
Watalii wa zanzibaar sasa wanakaribia 750000 ambazo ni wasyani wa 75 million $ zote zinaingia hazina ya muungani.
 
Mkuu crabat,

Finida, Danida, MCC, zote ni aina ya AID ambayo inapitia hazina (DSM), na inakuwa registered deni la Jamhuri ya Muungano, of which koti lake limevaliwa na Tanganyika.

Mapato nje ya kodi - kama sekta ya utalii yatabakia kuwa mapato nje ya muungano au yanajadilika. Suala la visa kuna njia nyingi, moja wapo ikiwa declaration ya mtalii anapoenda chukua visa anaenda wapi, hivyo fedha kupelekwa serikali husika; am just thinking out loud, cha msingi yanajadilika;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mradi wa umeme pemba umefadhiliwa na norway na finland.
Na ule wa zanzibar ni Millenium challenge.
But wat is 89billion? Wakati visa moja ya utaliii ni $100 na $ 50
Ni hizi miaka yote zinskusanywa na SMT ?
Watalii wa zanzibaar sasa wanakaribia 750000 ambazo ni wasyani wa 75 million $ zote zinaingia hazina ya muungani.
Nitakuwekea video waziri wa znz akithibitisha ninachosema. Mradi ulifadhiliwa na Norway na SMZ ambayo ilikosa pesa za kumalizia ikapewa kutoka muungano.

Utalii si muungano, na sijui kama kuna asilimia inayoingia huko. Hata hivyo lazima utambue sehemu kubwa ya utalii wa znz inatokea wapi. Takwimu za utalii tunaomba source.
 
Wana jamvi, mimi kabla ya kuendelea nawaomba mumsikilize kwa makini aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba, akijibu maswali mbalimbali kuhusiana na rasimu kama alivyoiwakilisha BMLK. Maswali aliyoyatolea ufafanuzi yanahusu takwimu walizozitumia, kero za Muungano, usaliti anaodaiwa kuufanya kuhusu muundo wa Muungano, gharama za kuendesha serikali tatu na tahadhari kwa jeshi kutumiwa kisiasa. Ni dakika 45 tu akihojiwa na ITV, karibuni.

Last edited by a moderator:
Niliposoma hili bandiko mwanzo kabisa nilijiweka sawa kusikia hoja za why S2..

Nilitarajia majibu ya maswali husika kama serikali ipi itawajibika kwa bunge la Tanganyika, n.k

Badala yake naona watu wanakuja na hoja za kwa nini S3 hazifai....pengine tusubiri uzi wenye kuzungumzia uzuri/ubaya wa S3.

Nawaomba mlio na ufahamu mpana juu ya utendaji kazi wa S2 mtiririke
 
Mchambuzi
Inasikitisha sana unapomnukuu Mwalimu wakati wewe mwenyewe umejikita kwenye ujinga; sisi CCM kama taasisi tuna haki ya kusimamia kile tunachoamini juu ya muungano na ndio maaana tunapigania serikali 2; hatima ya katiba yetu ipo mikononi mwa wananchi wao ndio waamuzi wa mwisho sasa kosa la CCM ni lipi? sisi wanaCCM tuna utaratibu wetu ambao ndio tumeutumia sasa kama kweli wewe ni mwanaCCM ulikuwa na nafasi hiyo inashangaza sana eti leo badala ya kutumia jukwaa sahihi leo umejikita JF nadhani umejinyima haki yako ya msingi kama mwanaCCM ( I doubt); CCM milango yetu ipo tunaendelea kusikiliza maoni na kuwaelemisha wananchi; ila mwisho wa yote wananchi ndio watakaoamua katiba yetu iweje; sasa kama wewe na kundi lako la Tanganyika na serikali 3 mna uhakika kuwa wananchi wanayakubali maoni yenu mna wasiwasi gani? nyie endeeleni kutoa somo na sisi kwa upande wetu tunaendelea. Nilikwaambia awali hakuna hata katiba moja katika dunia inayomridhisha kila mtu sisi CCM tupo tayari kupokea matokeo ya maamuzi ya wananchi na nyie tuanchowaomba muwe tayari kuyapokea maamuzi ya wananchi. Kazi ya tume ilikuwa ni kukusanya maoni sio kutengeneza katiba huu wenu ujinga usio na kipimo.
 
Hoja zako tumezijadili kwenye uzi uitwao: Duru Za Siasa: Mbinu za CCM za kuingiza katiba yao ya mafichoni". Nenda kule ukajadili
hayo, na utakutana na majibu mengi ya hoja zako mufilisi.

Hapa tupo kwenye mjadala wa je - maboresho ya serikali mbili na ccm yataboresha au yataua muungano? Hatujasikia ukijadili hili, lakini ni dhahiri hauna majibu. Lakini haupo peke yako bali hata wajumbe wengi wa NEC (CCM). Ni vitisho tu ndio vinawafanya wafyate, sio maamuzi yao kwani wanaona kwa uwazi kabisa jinsi gani CCM imeshindwa kulinda katiba ya jamhuri kupitia serikali yake, na wanaona hatima ya muungano haipo mbali. Huko juu nimeeleza kwanini.

Jadili hoja iliyopo mbele yako, usijadili mtoa hoja.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Muungano umeyumba sana wakati wa utawala wa Kikwete na Karume. Wakati Karume alitaka Zanzibar iwe mbali sana na Dodoma, Kikwete aliogopa kumkabili kuwa hiyo ni kinyume cha katiba. Hata sisi tuliokuwa mashabiki wa serikali moja ya muungano yenye nguvu sehemu zote na ile ya Zanzibar yenye nguvu katika mambo fulani fulani ndani ya Zanzibar tuliona hilo haliwezekani tena.

Kikwete anaweza kuwa anageuka leo kupinga serikali tatu, lakini akiwa rais wa jamhuri ya Muungano ndiye aliyeruhusu Zanzibar kujitenga. Unless wakubale kurekebisha kosa hilo Tanganyika lazima irudi chini ya mikono ya Kikwete; huenda hiyo itamjengea jina kubwa katika historia kuwa alirudisha Tanganyika au ikamharibia jina kuwa alishindwa kuimarisha muungano.
 
Back
Top Bottom