CCM, Siku mtuwekee January Makamba apeperushe bendera ya Urais, ni kutudharau watanzania

CCM, Siku mtuwekee January Makamba apeperushe bendera ya Urais, ni kutudharau watanzania

Masisiem huwa mnawaza nini, ukweli kwenu ni kama tusi?

Makamba hafai hata kulumangia lakin bado mnambeba?
 
CCM, tunawasaidia ili kuendelea kutawala hii nchi, na itabidi muanze kutulipa tunaosaidia na kuwapa mbinu za kuendelea kuaminiwa, bado mna watu makini.

Tukianza kuifanya nchi yetu kuwa ya majaribio, ni kutudharau Watanzania, sio kila mtu aweza kuwa kiongozi, Mungu ametupa vipawa tofauti, wengine wetu wapo wajuzi wa kuchora vikaragosi na wamejaliwa sana kwenye eneo hilo, ila si kwenye kuongoza.

Kuna watu ukiwaweka kwenye eneo la uongozi, nchi nzima inaingiwa baridi.

Mtu kujaribu uwezo wake, ni bora uishie tu kwenye mambo madogo-madogo, na hata kwenye eneo la kuongoza wizara ni hatua kubwa sana kujaribu uwezo wa mtu, kuna watu ambao hata hauhitaji akili kubwa kufahamu hawana uwezo wowote zaidi ya wao kubebwa huku wakiongozwa na roho mbaya na ufanisi wao ni sifuri!

Mmoja wapo ni huyu Mtanzania mwenzetu January Makamba, na sio kwamba hatumpendi, ila kwa sababu ya umhimu mkubwa wa nchi yetu na ikizingatiwa kwamba, Dunia imetutangulia mbele mno, kujaribu kuifukuzia tukiwa na viongozi dhaifu, ni kupoteza muda njiani, huyu hatufai, na sio kwamba hatufai wananchi peke yake, bali hata yeye anajifahamu kuwa hana uwezo, ila kwa kubebwa!

CCM, bado inawatu makini na wenye uthubutu wa kufanya mambo makubwa, hamjawahi tu kuwapa nafasi.

Huyu ndugu yetu hajawahi kufanya vizuri kwenye eneo lolote kwa wizara yoyote ile!

Hajawahi kufanya ubunifu wowote kwenye sekta yoyote ile.

Amehusishwa na makandokando kibao, na iwapo kitengo husika kikaamua kufuatilia makandokando yake, lazima atoroke.

Ni kiongozi dhaifu sana, bahati ni kwamba kuzaliwa kwenye familia inayoamini ina kijana shupavu na mwenye uwezo mkubwa, ila wakasahau kwamba nchi hii ni kubwa kuliko wao, na kwamba sio kweli panapotokea mmoja wa wanafamilia kuwa sehemu ya watu waliowahi kuongoza, waamini kwamba hata kizazi chao, ni kizazi cha viongozi, siyo kweli

Ni eneo lipi tunaweza kusema, kazi zake na usimamizi wake unaweza kummbeba?

Ni kiongozi anayeamini kwamba, pesa ni kila kitu na kwamba, pesa inaweza kununua uongozi na ndio akili kubwa ya kuongoza wananchi na kuwatetea maendeleo

Huyu hafai hata kujaribisha!

Siku CCM mmetuwekea January Makamba kuwa mpeperusha bendera ya Urais kwenye chama, mtakuwa mmetudharau sana Watanzania!
Big up mkuu ...100% ukweli mtupu.
Makamba January ni mmojawapo wa viongozi ambao wanachukiwa na Umma wa watanzania kwa kiwango kikubwa sana.

Na hii haijawa kwa bahati nbaya,bali kwa sababu ya matendo yake ya kutokuwa muadilifu katika masuala ya ubadhilifu wa mali za umma kila anapopewa nafasi katika utumishi wa umma popote pale anapowekwa.

Ni muumini wa siasa za makundi na mbinafsi mwenye kiburi na dharau,
Asiye na heshima wala mahusiano mema hata viongozi wenzake.

Kwake yeye humuheshimu yule aliemteua pekee!

Mjivuni mmoja kutoa Bumbuli-Lushoto.katika familia ya mjivuni na mpika majungu mkuu ...Yusuph Makamba sr.
 
Masisiem huwa mnawaza nini, ukweli kwenu ni kama tusi?

Makamba hafai hata kulumangia lakin bado mnambeba?
Wanajivuna kwa vile wameshatengeneza mfumo ambao kura za kwenye sanduku haziamui nani awe Rais. CCM hata wakiweka sokwe kuwa mgombea wa urais basi sokwe atatangazwa kuwa Raia na ataapishwa kuwa Rais.
 
Big up mkuu ...100% ukweli mtupu.
Makamba January ni mmojawapo wa viongozi ambao wanachukiwa na Umma wa watanzania kwa kiwango kikubwa sana.

Na hii haijawa kwa bahati nbaya,bali kwa sababu ya matendo yake ya kutokuwa muadilifu katika masuala ya ubadhilifu wa mali za umma kila anapopewa nafasi katika utumishi wa umma popote pale anapowekwa.

Ni muumini wa siasa za makundi na mbinafsi mwenye kiburi na dharau,
Asiye na heshima wala mahusiano mema hata viongozi wenzake.

Kwake yeye humuheshimu yule aliemteua pekee!

Mjivuni mmoja kutoa Bumbuli-Lushoto.katika familia ya mjivuni na mpika majungu mkuu ...Yusuph Makamba sr.
Hii haizuii yeye kuwa Rais hapo baadae
 
Kashindwa Nishati nchi ataiweza wapi?

WATANZANIA walipiga kelele nyingi sana baada ya januari na maharage na bodi mpya kuteuliwa wakapuuzwa sasa matokeo yameprove wamefeli vibaya nchi iko gizani

Aibu kwa samia na mamlaka yake ya uteuzi waliteuwa kimihemko badala ya kuangalia weledi ona sasa kamrudisha Mhandisi kuwa Mkurugenzi

Na bodi kaiweka Mwenyekiti mpya

Rais apunguze kuziba masikio 😕
 
Kipindi cha Mkwere huyu jamaa nyota yake iliwaka sana, sijui huwenda yalikuwa ni mambo ya ndumba kumbe ni bure kabisa
 
Back
Top Bottom