CCM, tafuteni namna ya kumshauri Rais Magufuli maana muda mwingine anaumiza sana

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2020
Posts
888
Reaction score
821
Nimesikiliza hotuba ya mh. JPM baada ya kumuapisha Naibu Waziri wa madini Prof. S. E.Manya.
Moja ya sababu zilizosababisha kuleta huu uzi ili wana CCM wenzangu ambao wanaweza kutafakari uzi huu na ikibidi kumshauri mh. Rais.

KIMEJIRI KITU GANI KWA MAONO YANGU?
Mh. Rais alizungumzia mambo ya msingi kuhusu hii wizara kuendelea kuwa wabunifu wa kuibua vyanzo vingine kama cool, coper, gas nk. Badara ya kukomalia dhahabu peke yake. Alikuwa sahihi kabisa.

Shida ilikuja alipoanza kuwazungumzia waliokuwa watumishi wa TMAA, ni kweli kulikuwa na mapungufu katika tume ile, na aliivunja, na matokeo kweli tumeyaona na tunayaona. Ila sidhani kama lugha na maagizo aliyotoa yamepitia kwa washauri wake.

KWANINI?
Sidhani kama ni vizuri kuwasema watumishi wale ambao wengine bado wapo ndani ya Wizara na tume kuwa walifanya kazi za hovyo. Katika hili ajue tume hiyo ilianzishwa na Serikali iliyokuwepo chini ya Rais kama yeye, hivyo kabla ya kuwatukana wale amtukane kwanza Rais aliyekuwepo.

Lakini ajue kuwa mishahara waliyopewa watumishi wale hawakujipangia bali walipewa kwa mujibu wa taratibu walizozikuta waajiriwa wale. Hivyo hawakuwa na kosa.

Ok, kama aliona kuna utofauti mkubwa wa mishahara basi angeshauliwa eidha kuwapeleka kufanya kazi maeneo ambayo inalingana na mishahara yao kama vile TRA aliyoitaja kuwa hata yeye inamzidi mshahara maana hata TMAA kazi yao ilikuwa kukusanya kodi zitokanazo na madini kama ilivyo TRA.

Au angewaongeza wafanyakazi wte waliokuwa chini ya hawa watumishi wa TMAA ili kubalance. Mimi binafsi Enzi na Enzi sioni afya ya maagizo aliyoyatoa ya kutaka hata kanuni zibadilishwe kwa lengo la kushusha mshahara wa mtu au kikundi cha watu.

Mh Rais na washauri wake wakae wakijua kuwa hawa kumshusha mtu mshahara ambao amezoea kuuishi na familia yake ni kumpa magonjwa ya moyo au presha kwa aliyekuwa hana.

Lakini pia watumishi hawa najua hawataacha kazi maana maisha ni magumu lkn watakaa wakimlilia yeye muda wote. Ni bora kama alikuwa hawataki angewafanyia hiyo Retrinchment maana nalo lina taratibu zake.

ANGALIZO KWA MH SPIKA JOB NDUGAI
Ifike sehemu Bunge nalo lijisimamie na litetee wananchi na wafanyakazi badala ya kuunga mkono kila hisia za kiongozi.

Wana ccm mshaurini Rais ajifunze kupunguza maadui badala ya kuongeza maadui kila uchwao ikibidi kumkatalia kabisa, ipo siku atakuja na jingine tena.

Huko nje kuna watu walitumikia nchi hii ktk mfumo uliokuwepo walikuja kuachwa bila malipo yeyote hilo nalo lilikuwa ni uonevu, ni bora angewalipa kama alivyofanya Mkapa mwaka 1997 baada yakuwaondoa darasa la7 ktk Wizara ya Afya.

Rais awe anatumia lugha mwanana kushairi, kuonya, au kukemea maana yeye ni kiongozi mkuu hata akiongea anacheka litafanyiwa kazi tu.

Asijitambulishe kuwa nikatiri mno hana huruma nk. Kumbe ni namna ya anavyotatua matatizo hata kaam yana tija lakini nguvu inakuwa kubwa mno, eti kubadili kanuni !! Loh! Kwasababu ya mshahara wa mtu tu. Akumbuke hawa ni waajiriwa. Mh. Asipoangalia atakuja akiponze chama pendwa cha CCM, sijui nao wanamuogopa?

Nawasilisha tafadhali.
Enzi na enzi.
 
Watu walipwe kulingana na uzalishaji wao, kwa vile waliboronga kazi basi ni busara wapunguziwe mshahara kufidia hasara waliolisababishia taifa na tena walipaswa kustaafishwa kabisa, rais ana huruma.
 
Duuuh, basi kama hao wanapunguzwa basi waongezewe waalimu. Au nao uzalishaji wao ni mdogo?😭😭😭
Bora hio pesa waongezewe hawa maana wanachapa kazi 'kweri kweri' lkn wanacholipwa hakina sifa ya kuitwa mshahara bali 'marupurupu'.

Rais katoa hoja ya msingi tu, watu wameboronga huko walikotoka kisha wanahama na hilo 'limshahara' kwenda kuwanyanyasa watumishi wenzao tena mabosi wao ktk taasisi mpya.
 
Wana ccm mshaurini mh.Rais ajifunze kupunguza maadui badara ya kuongeza maadui kila uchwao ikibidi kumkatalia kabisa, ipo siku atakuja najingine tena.
Hata akiwafanya watanzania karibu wote kuwa adui zake watamfanya nn? Watanzania hawana la kumfanya huyu jiwe.

Anajiamini, ana dola, yuko juu ya sheria na anaweza hata kuwaua hao watumishi wa TMAA na hakuna wa kumgusa. Rais wa Tanzania ni Mungu wa watanzania.
 

Kwanini waliwapeleka huko ambako mishahara ni midogo? Siwangewapeleka huko alikokutaja TRA? Kwahiyo wabadili kanuni ili kushusha mshahara wa mtu?? Nahizo kanuni zitakuwa za mwaka gani? Yaani GN no ngapi ya mwaka gani?
Labda niuoga wa maisha tu.
Au khari ngumu ya maisha
Km vp mnasongeshana CMA
 
Jamaa kasema ,jamaa kaamua, Iq yake ina ana amini niko sahihi makamu alshapewa vyake, waziri alpewa vyake ni spika na raisi ndio marafiki, Mizengo pinda hawezi sema mwanae yuko bungeni, Mwinyi hawezi sema mwanae ni raisi. Kikwete mwanae na mkewe wapo chini ya bosi.

Kamati gani ya kumshauri wakati jamaa yeye ni yeye tusubiri apite hivi, mbona ukiwaunasali hata kama unashona viatu maisha ni ya furaha sana.

Mmeambiwa kama hamtaki acheni kazi jamaa hawawazi hata kidogo.
 
Ndio unaamka sasa, mbona hizi hulka binafsi zimekuwa ni sehemu ya uongozi wake na wanaccm mkawa mnasifia kuwa nchi inanyooshwa? Unataka bunge la wanaccm lisimame dhidi ya maagizo ya rais ambayo unadhani sio sahihi. Kwa taarifa yako nusu ya wabunge wa ccm wamepatikana kwa kutoa rushwa, na yeye hilo analifahamu. Na zaidi ya nusu wako ndani ya hilo bunge bila kushinda kihalali kwenye majimbo, bali kwa amri yake.

Angalia spika wa bunge na waziri Mkuu wote wamepatikana kwa kupita bila kupingwa, na fuatilia kilichowafanya wapite bila kupingwa ni njia za kihalifu. Hao ni mifano hai tu ya wabunge wengi walioko kwenye hilo bunge. Unapokuwa na wabunge zaidi ya 60% walioko bunge kwa mbinu za kihalifu na matumizi mabaya ya madaraka, wanapata nguvu ya kumkemea rais ambaye ndio alitumia madaraka yake vibaya kuwapatia ubunge?
 
Hajasema upungue kiasi gani kwahiyo katibu mkuu anaweza kupunguza laki 2 tu msijali
 
Usikute hawa wanaobatizwa kwa mshahara mpya wa moto ndo wavaa za kijani pure maana green pasture kama hiyo mpinzani utapenyea wapi?
Nawaonea huruma ubatizaji unaendelea bila kutazama sura.
Haya mambo yasikie kwa mwenzako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…