Enzi na Enzi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 888
- 821
Nimesikiliza hotuba ya mh. JPM baada ya kumuapisha Naibu Waziri wa madini Prof. S. E.Manya.
Moja ya sababu zilizosababisha kuleta huu uzi ili wana CCM wenzangu ambao wanaweza kutafakari uzi huu na ikibidi kumshauri mh. Rais.
KIMEJIRI KITU GANI KWA MAONO YANGU?
Mh. Rais alizungumzia mambo ya msingi kuhusu hii wizara kuendelea kuwa wabunifu wa kuibua vyanzo vingine kama cool, coper, gas nk. Badara ya kukomalia dhahabu peke yake. Alikuwa sahihi kabisa.
Shida ilikuja alipoanza kuwazungumzia waliokuwa watumishi wa TMAA, ni kweli kulikuwa na mapungufu katika tume ile, na aliivunja, na matokeo kweli tumeyaona na tunayaona. Ila sidhani kama lugha na maagizo aliyotoa yamepitia kwa washauri wake.
KWANINI?
Sidhani kama ni vizuri kuwasema watumishi wale ambao wengine bado wapo ndani ya Wizara na tume kuwa walifanya kazi za hovyo. Katika hili ajue tume hiyo ilianzishwa na Serikali iliyokuwepo chini ya Rais kama yeye, hivyo kabla ya kuwatukana wale amtukane kwanza Rais aliyekuwepo.
Lakini ajue kuwa mishahara waliyopewa watumishi wale hawakujipangia bali walipewa kwa mujibu wa taratibu walizozikuta waajiriwa wale. Hivyo hawakuwa na kosa.
Ok, kama aliona kuna utofauti mkubwa wa mishahara basi angeshauliwa eidha kuwapeleka kufanya kazi maeneo ambayo inalingana na mishahara yao kama vile TRA aliyoitaja kuwa hata yeye inamzidi mshahara maana hata TMAA kazi yao ilikuwa kukusanya kodi zitokanazo na madini kama ilivyo TRA.
Au angewaongeza wafanyakazi wte waliokuwa chini ya hawa watumishi wa TMAA ili kubalance. Mimi binafsi Enzi na Enzi sioni afya ya maagizo aliyoyatoa ya kutaka hata kanuni zibadilishwe kwa lengo la kushusha mshahara wa mtu au kikundi cha watu.
Mh Rais na washauri wake wakae wakijua kuwa hawa kumshusha mtu mshahara ambao amezoea kuuishi na familia yake ni kumpa magonjwa ya moyo au presha kwa aliyekuwa hana.
Lakini pia watumishi hawa najua hawataacha kazi maana maisha ni magumu lkn watakaa wakimlilia yeye muda wote. Ni bora kama alikuwa hawataki angewafanyia hiyo Retrinchment maana nalo lina taratibu zake.
ANGALIZO KWA MH SPIKA JOB NDUGAI
Ifike sehemu Bunge nalo lijisimamie na litetee wananchi na wafanyakazi badala ya kuunga mkono kila hisia za kiongozi.
Wana ccm mshaurini Rais ajifunze kupunguza maadui badala ya kuongeza maadui kila uchwao ikibidi kumkatalia kabisa, ipo siku atakuja na jingine tena.
Huko nje kuna watu walitumikia nchi hii ktk mfumo uliokuwepo walikuja kuachwa bila malipo yeyote hilo nalo lilikuwa ni uonevu, ni bora angewalipa kama alivyofanya Mkapa mwaka 1997 baada yakuwaondoa darasa la7 ktk Wizara ya Afya.
Rais awe anatumia lugha mwanana kushairi, kuonya, au kukemea maana yeye ni kiongozi mkuu hata akiongea anacheka litafanyiwa kazi tu.
Asijitambulishe kuwa nikatiri mno hana huruma nk. Kumbe ni namna ya anavyotatua matatizo hata kaam yana tija lakini nguvu inakuwa kubwa mno, eti kubadili kanuni !! Loh! Kwasababu ya mshahara wa mtu tu. Akumbuke hawa ni waajiriwa. Mh. Asipoangalia atakuja akiponze chama pendwa cha CCM, sijui nao wanamuogopa?
Nawasilisha tafadhali.
Enzi na enzi.