CCM, tafuteni namna ya kumshauri Rais Magufuli maana muda mwingine anaumiza sana

CCM, tafuteni namna ya kumshauri Rais Magufuli maana muda mwingine anaumiza sana

Vururu tupu chi hii. Nani ndani ya Chama atadiriki kumushauri? Mtu huyo hajipendi?
 
Hoja ya rais iko sawa, inatufundisha tufanye kazi
 
Ndio unaamka sasa, mbona hizi hulka binafsi zimekuwa ni sehemu ya uongozi wake na wanaccm mkawa mnasifia kuwa nchi inanyooshwa? Unataka bunge la wanaccm lisimame dhidi ya maagizo ya rais ambayo unadhani sio sahihi. Kwa taarifa yako nusu ya wabunge wa ccm wamepatikana kwa kutoa rushwa, na yeye hilo analifahamu. Na zaidi ya nusu wako ndani ya hilo bunge bila kushinda kihalali kwenye majimbo, bali kwa amri yake.

Angalia spika wa bunge na waziri Mkuu wote wamepatikana kwa kupita bila kupingwa, na fuatilia kilichowafanya wapite bila kupingwa ni njia za kihalifu. Hao ni mifano hai tu ya wabunge wengi walioko kwenye hilo bunge. Unapokuwa na wabunge zaidi ya 60% walioko bunge kwa mbinu za kihalifu na matumizi mabaya ya madaraka, wanapata nguvu ya kumkemea rais ambaye ndio alitumia madaraka yake vibaya kuwapatia ubunge?
Kamwe. Kamwe; huwezi kuuma mkono unakupatia shibe na heshima.
 
Mbona unabugi jamaa yangu? Kwani nini maana ya ofisi ya rais? Rais aliyepita akiajiri mtu akafanya makosa atukanwe yeye? Yaani unataka watu walioharibu waachwe na mishahara minono kisa? Wewe ndio hao mlioharibu.
 
Ndio unaamka sasa, mbona hizi hulka binafsi zimekuwa ni sehemu ya uongozi wake na wanaccm mkawa mnasifia kuwa nchi inanyooshwa? Unataka bunge la wanaccm lisimame dhidi ya maagizo ya rais ambayo unadhani sio sahihi. Kwa taarifa yako nusu ya wabunge wa ccm wamepatikana kwa kutoa rushwa, na yeye hilo analifahamu. Na zaidi ya nusu wako ndani ya hilo bunge bila kushinda kihalali kwenye majimbo, bali kwa amri yake.

Angalia spika wa bunge na waziri Mkuu wote wamepatikana kwa kupita bila kupingwa, na fuatilia kilichowafanya wapite bila kupingwa ni njia za kihalifu. Hao ni mifano hai tu ya wabunge wengi walioko kwenye hilo bunge. Unapokuwa na wabunge zaidi ya 60% walioko bunge kwa mbinu za kihalifu na matumizi mabaya ya madaraka, wanapata nguvu ya kumkemea rais ambaye ndio alitumia madaraka yake vibaya kuwapatia ubunge?
Sina mfano duniani wa Rais aliyeingia madarakani kihalifu kisha akaongoza nchi kiungwana. CCM walikenua meno ya furaha walipojiingiza madarakani kwa uhalifu, sasa wayapokee machungu ya uhalifu wao. Rais wao ni dikteta.
 
Ukiona mtu anajiita Jiwe, mara Jembe, unadhani utamshauri nini?
Mtu anayemgawa mama yake kwa malipo ya jogoo
Rais mwenye majina mengi ujue hafai na dikteta. Hivyo Idi Amin, Kamuzu Banda, et al walikuwa na majina mangapi kila mmoja? Tena majina ya hovyooo. Wengine waliitwa Dada (Idd Amin), kuku (Kamuzu) na sasa nasi tuna Jiwe!!!.
 
Wengi wetu wabongo tuna tabia ya kufurahia tukisikia ndugu zetu yanawafika majanga. Hii ni hulka mbaya sijui ni wivu, roho mbaya au malovelence au tuko sadistic sijui ni pepo au shetani gani.

Baadhi ya ambayo tumejukuta tunashangilia kimkumbo mkumbo huku wengine wakiumia ni:

1. Watu wakitumbuliwa hadharani bila kupewa nafasi ya kujitetea. Wakati mwingine kwa hisia tu au majungu yaliyopenya hadi kwa watumbuaji. Akina Mkurugenzi wa Jiji Kabwe (Mungu amrehemu kwani alifariki mara)

2. Kufukuzwa kazi kwa watumishi wa umma ambao wengine wamelitumikia taifa kwa zaidi ya miaka 20 kwasababu ya vyeti. Walimu, manesi, madereva nk

3. Wananchi wenzetu kuvunjiwa nyumba na serikali kuachwa homeless. Ubungo Morogoro Road

4. Wananchi kukamatwa na kutiwa ndani kwa amri za wenye mamlaka bila kufuata haki na sheria.

5. Wanasiasa wa upinzani kuonyeshwa cha mtema kuni.

6. Watu kutekwa, kupotezwa, kupigwa risasi na hata kuuwawa. MO

7. Watu kukamatwa kuwekwa korokoroni kubambikiwa kesi za uongo. Masheikh wa Zanzibar.

8. Wafanya biashara kuporwa fedha zao benki.

Na mengine mengi!!

Sisi wananchi wakati mwingine bila kutafakari nakujiuliza vizuri tumekurupuka na tumeshangilia na kufurahia haya yakitendeka ilimradi hayatugusi sisi binafsi!

Sasa hivi hawa watumishi wa TMA tumeshawahukumu kuwa ni wakosaji tushangilia kama mazuzu eti wapunguziwe mishahara kinyume na sheria sababu tu kiongozi ameituhumu tume iliyokuwa imewaajiri zamani hizo.

Tunataka wapunguziwe mishahara bila kujali madeni na commitment walizoingia kwa kutegemea kulipa kupitia mishahara yao!
Tunasema acha nao walipate joto la jiwe, acha nao wateseke, wapate presha na sukari au hata kufa na wafilie mbali tu. Kwani nini bwana.

Sisi tunaofurahia mateso haya kwa wengine ni sisi tunaojiita wacha Mungu, wazalendo, tuaoipenda Tz, wapenda maendeleo!!

Tumwombe Mungu atubadilishe, tuwe na upendo, huruma, subra, tuipende haki na tuchukie dhuluma. Haya ndiyo maamrisho ya Mola wetu.

Muda wa kuishi ni mfupi tutendeane yaliyo mema na tuitende iliyo hakhi!!

Haki huliinua Taifa.
Tupendane tustahiane.
 
JPM hataki watumishi wazembe kazini, anataka mtumishi alipwe kwa kadri anavyojitutuma kazini. Watumishj wa umma walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea wakijua kwamba hata wakiboronga wataendelea kupokea mshahara wao bila shida, hii ilipunguza ufanisi wa kazi kwa kiasi kikubwa.

Ukilinganisha na sekta binafsi, mfanyakazi analipwa kulingana na mchango anaoutoa katika kazi husika, mfanyakazi anapangiwa kazi ambazo mwisho wa mwaka zinakuwa evaluated kuangalia performance yake. Akifanya vizuri anakuwa promoted akifanya vibaya anakuwa demoted au kuachishwa kazi. Hii inasaidia mfanyakazi ajitume na awe mbunifu ili mwisho wa siku kazi yake ionekane bora.

Kwa hiyo hata hao waliokuwa TMA ilikuwa sawa kuwa demoted, kwa sababu walipangiwa majukumu wakayatekeleza chini ya kiwango. Haingii akilini watu walioboronga wakiwa na mishahara minono wahamishwhe na mishahara yao hiyo hiyo, hii ni ku promote uzembe kazini, watu Kama hao hawawezi kujituma hata siku moja kwa sababu wanajua hakuna kitakachobadilika.
 
Bora hio pesa waongezewe hawa maana wanachapa kazi 'kweri kweri' lkn wanacholipwa hakina sifa ya kuitwa mshahara bali 'marupurupu'.

Rais katoa hoja ya msingi tu, watu wameboronga huko walikotoka kisha wanahama na hilo 'limshahara' kwenda kuwanyanyasa watumishi wenzao tena mabosi wao ktk taasisi mpya.

Ili tuelewe kwanini msijadili kwa kuzingatia sheria ya utumishi wa umma inasemaje badala ya kutujazia blah blah za kisiasa.
Ninachokiona, huu mjadala umejaa wapinga kila kitu, waunga mkono kila kitu na wale wa roho za kwanini ambao labda maisha yameshawachapa wako stuck kwenye nyumba za shemeji zao.
 
Back
Top Bottom