Wengi wetu wabongo tuna tabia ya kufurahia tukisikia ndugu zetu yanawafika majanga. Hii ni hulka mbaya sijui ni wivu, roho mbaya au malovelence au tuko sadistic sijui ni pepo au shetani gani.
Baadhi ya ambayo tumejukuta tunashangilia kimkumbo mkumbo huku wengine wakiumia ni:
1. Watu wakitumbuliwa hadharani bila kupewa nafasi ya kujitetea. Wakati mwingine kwa hisia tu au majungu yaliyopenya hadi kwa watumbuaji. Akina Mkurugenzi wa Jiji Kabwe (Mungu amrehemu kwani alifariki mara)
2. Kufukuzwa kazi kwa watumishi wa umma ambao wengine wamelitumikia taifa kwa zaidi ya miaka 20 kwasababu ya vyeti. Walimu, manesi, madereva nk
3. Wananchi wenzetu kuvunjiwa nyumba na serikali kuachwa homeless. Ubungo Morogoro Road
4. Wananchi kukamatwa na kutiwa ndani kwa amri za wenye mamlaka bila kufuata haki na sheria.
5. Wanasiasa wa upinzani kuonyeshwa cha mtema kuni.
6. Watu kutekwa, kupotezwa, kupigwa risasi na hata kuuwawa. MO
7. Watu kukamatwa kuwekwa korokoroni kubambikiwa kesi za uongo. Masheikh wa Zanzibar.
8. Wafanya biashara kuporwa fedha zao benki.
Na mengine mengi!!
Sisi wananchi wakati mwingine bila kutafakari nakujiuliza vizuri tumekurupuka na tumeshangilia na kufurahia haya yakitendeka ilimradi hayatugusi sisi binafsi!
Sasa hivi hawa watumishi wa TMA tumeshawahukumu kuwa ni wakosaji tushangilia kama mazuzu eti wapunguziwe mishahara kinyume na sheria sababu tu kiongozi ameituhumu tume iliyokuwa imewaajiri zamani hizo.
Tunataka wapunguziwe mishahara bila kujali madeni na commitment walizoingia kwa kutegemea kulipa kupitia mishahara yao!
Tunasema acha nao walipate joto la jiwe, acha nao wateseke, wapate presha na sukari au hata kufa na wafilie mbali tu. Kwani nini bwana.
Sisi tunaofurahia mateso haya kwa wengine ni sisi tunaojiita wacha Mungu, wazalendo, tuaoipenda Tz, wapenda maendeleo!!
Tumwombe Mungu atubadilishe, tuwe na upendo, huruma, subra, tuipende haki na tuchukie dhuluma. Haya ndiyo maamrisho ya Mola wetu.
Muda wa kuishi ni mfupi tutendeane yaliyo mema na tuitende iliyo hakhi!!
Haki huliinua Taifa.
Tupendane tustahiane.