CCM, tafuteni namna ya kumshauri Rais Magufuli maana muda mwingine anaumiza sana

Sijaona hoja hapo. Umeisoma mada vizuuri lakini Pascal? Hii imefanana na kijana aliyejaribu kumchumbia binti, alipomkosa akaanza kuona makovu aliyo nayo usoni na kuanza kutangazia watu kuwa ana sura mbaya .

Utakuwa unadhani mtoa mada ni mtumishi , au muathirika wa hiyo habari!! La hasha!
Nakama huwa unafatilia mada za mleta uzi huu, ni team jpm leo jana nahata siku zijazo.

Nampenda sana jpm, na jpm siyo maraika, lkn pia tunayohaki ya kumshauri kwa njia hizi au kuonyesha kuwa sisi wapambe wake, kuna mambo hatukubaliani nae. Siyo kila kitu ndio. Au kushangilia, tutakuwa tunampoteza, ni kheri tuseme kuliko kukaa kimya.

Mwisho, hata kama jamaa baada ya kukataliwa na binti then akaanza kutangaza sura ya binti kuwa ni mbaya, bado wewe unayetangaziwa usipuuze mwangalie binti sura yake km kweli inamakovu??? Ukibaini haina basi sema kuwa jamaa anamtangaza binti kwakuwa katoswa.

Nenda ukasome habari ya kuzama kwa meli kubwa ya titanic hata ktk mtandao!. Uone namna ilivyozama na namna watu walivyoangamia.

Kifupi nikwamba wengi wao nahata nahodha wao, walizarau maonyo.
 
Labda kama hujui kwanini hili tunalisemea, nikwamba, linaweza kuathiri watu wengi sana nahata sisi wananchi wanyonge.

Usizani wafanyakazi wte watalipokea sawa sawa! Ndio maana kukawa na utaratibu wa kumshughulikia mkosaji kisheria, tena ndani ya mahakama. Ili kulinda utu wake.
Kunawatu wamepoteza maisha kaka kwa hii stail.
Utu wa mtu ndilo jambo muhimu ktk maisha ya binadam.
Utu wa mtu hauthaminishwi kwa cheo, pesa, au madaraka.

Km wewe ni mkristo, nijibu hili swali dogo, kwamba kwanini yule mwanamke aliyekamatwa amezini ,nakisha kupelekwa kwa yesu ili yesu atoe hukumu, unadhani kwa nini yesu aliwaambia wale washtaki wake kuwa ambaye hana dhambi aanze kumponda huyu mwanamke jiwe? Je! Kwa nini hakutokea hata mmoja?
KWANINI YESU
ALIFANYA HIVYO?... Alijua hakuna ambae hana makovu ya makosa , na alitaka tuonyane kwa staha na kuheshimiana siyo kama mafarisayo yalivyomburuta mama wa watu.

NIJIBU SWALI HILI.
............................................
Kicheree alivyotolewa TRA kwenda kuwa RAS nae alitangazwa kupunguziwa mshahara? Nae sialiharibu TRA?
Diwani alipopelekwa kuwa RAS nae alipunguziwa mshahara?
Aijipi aliyepewa ubarozi, nae alitangazwa kupunguziwa mshahara?
Andegenyee wa fire nae alipunguziwa mshahara???
Nawengine wengi.

Tuweni wakweli , maana msema kweli ni mpenzi wa mungu.
Enzi na Enzi
 
Kwa majibu haya, tunakuomba mheshimiwa endelea kupunguza mshahara wa hawa watu ikibidi walipwe mia tano, hadi siku akili ziwakae sawa!

Kwamba Lissu ni adui yako???? Alikufanya nini? Hebu eleza huku ukiambatanisha ithibati thabiti hapa.
 
Huu ni utawala ambao unajitahidi kila raia wake awe masikini na kwakweli unafanikiwa sana,jiwe anajigamba kupokea mshahara 9m na anaiona ndogo sana,Ingekuwa vema tungejua na allowance zake kwa mwezi hapa ndio kwenye kipimo sio mshahara.
Mara nyingi tawala zakibabe huwa zinaongoza sana kwa ufisadi,muda ni hakimu mzuri wacha tusubiri.
 
Suala la kupunguza salary siungi mkono but rather Government wangeongeza mshahara kwa hao Maboss wa Time ya Madini
 
Mtoa mada nikuambie tu kwamba mliishi kwa mazoea huyu Rais ndio anafaa kwa Tanzania hii.
 
Magufuli anapanga mpaka mishahara ya Watu na kila kitu ndani ya Nchi.
Kwani nini maana ya kuwa Rais, hujui kwamba tuko kwenye matengenezo baada ya mifumo ya nchi kuoza kwa rushwa, ufisadi na vyeti fake. Ili kujenga lazima uvunje, uharibu na kuangamiza. Usiishi kwa mazoea
 
Endeleeni na matusi lakini kumbuka mtaendelea kutawala humu JF lakini si kuingia Ikulu ya Chamwino.
Ukiona mtu anajiita Jiwe, mara Jembe, unadhani utamshauri nini?
Mtu anayemgawa mama yake kwa malipo ya jogoo
 
Hafai ? Wakati tumemchagua wenyewe. Wewe unayefaa uko wapi sasa tukuone.
Rais mwenye majina mengi ujue hafai na dikteta. Hivyo Idi Amin, Kamuzu Banda, et al walikuwa na majina mangapi kila mmoja? Tena majina ya hovyooo. Wengine waliitwa Dada (Idd Amin), kuku (Kamuzu) na sasa nasi tuna Jiwe!!!.
 
Huo ni wimbo tulishauchoka. Tafuteni mwalimu mpya wa kwaya yenu atunge nyimbo zingine. CCM hii kwa upinzani wa nchi hii itatawala mpaka ichoke yenyewe.
 
Kituko mbele ya watu gani ? Wewe na wapinzani wenzio uchwara ndio kituko katika nchi hii
Nyie ndiyo mnamponza jiwe mpaka anaonekana kituko mbele ya watu(wanaojielewa lakini wewe haumo).
 
Naam. Waambie ndugu yangu
 
Huyo ni mkuu wa nchi. Hujui kuwa Rais ndiye mkuu wa Utumishi wa umms ?
 
Tukikosa mtu mbadala ataendelea aendelee kuinyoosha nchi
Wanachotakiwa kumshauri ni kujiandaa kutoka madarakani baada ya 2025 maana kashajipanga kuchezea katiba yetu na kuwa kama best yake mseven
 
Mbona wenye vyeti fake waliendelea kuongezeka nchii hii, Rais aliyekuwepo hakujua ? Mwacheni RAIS wetu achape kazi na kuondoa uozo wote. Mlizoea vya kunyonga vya kuchinja hamuviwezi.
 
Hiyo CHADEMA ya wajanja iko wapi ? Usituletee ugali uliochacha hapa siye tuko busy kuijenga nchi.
 
Ujue ili iweje ? Huo mshahara tu wa Mbowe huko CHADEMA huujui sembuse wa mkuu wa nchi ili uufanyie nini ?
 
Watu walipwe kulingana na uzalishaji wao, kwa vile waliboronga kazi basi ni busara wapunguziwe mshahara kufidia hasara waliolisababishia taifa na tena walipaswa kustaafishwa kabisa, rais ana huruma.
Kiwango chao cha kuboronga wakijua au?
Waliboronga vipi na kwa nini?
Mambo mengine utakuta yalikuwa nje ya uwezo wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…