Kuna ujinga mkubwa sana unafanywa na ccm kwa kutumia kodi zetu kutaka kukidhoofidha na kukiua kabisa CHADEMA
Hawa waliobuni hii project sijui ni akina nani huko ccm
Hivi kweli mpaka Leo ccm inashindwa kujua kwamba
CHADEMA sio TLP?
CHADEMA sio CUF?
CHADEMA sio NCCR- MAGEUZI?
Wanadhani na wanajiongopea kwamba kwakuwa walifanikiwa kuvi difuse hivyo vyama hapo juu basi wataweza kwa CHADEMA
CHADEMA ni chama kibeba maono ya Taifa la Tanganyika.. CHADEMA NI MPANGO KAMILI WA MUNGU kuliokoa taifa la Tanganyika..!
Huku wakikiyumbisha chama kwa kuwashawishi viongozi wa mikoa mbalimbali kuondoka CHADEMA.. huko mikoani mikutano ya NO REFORMS NO ELECTION chini ya Heche na timu yake inazidi kupata uungwaji mkono na wananchi wa kawaida
Hatuoni wananchi wakisusia mikutano ya no reforms no election kwakuwa tu viongozi wao wa ngazi za chini na za kati wanakihama chama..kinachoendelea na kinachotokea ccm hawaamini kabisa macho yao.. Wanebaki na press conference za kupangq huku wakichekwq na kudharauliwa na hata wana ccm wenzao wenye akili
Hivi wanashindwa kutambua kabisa kwamba CHADEMA imeshavuka level za kuwa chama cha viongozi na wanachama wachache?
Hivi wanashindwa kabisa kujua kwamba CHADEMA ina mashina lukuki kwa maelfu kiasi kwamba ukikata mmea kwenye shina moja inachipua mingine kumi?
CHADEMA kwa sasa ni imani
CHADEMA kwa sasa ni tumaini
CHADEMA kwa sasa ni furaha, ni faraja na ni mwanga wa taa kwenye giza totoro liitwalo ccm!
Wananchi wanaihitaji CHADEMA iwe mvua liwe jua kuliko viongozi wenye bei wanaonunulika.. Ndio maana kuhama kwao sio mjadala na wala wananchi hawastuki
CHADEMA ni joka kubwa lenye vichwa vingi.. Ukikata kimoja vinachipua vingine... com ni mti wa mkafiri ukiushika tu unaishia kukunukia na kukutia nuksi😂