PreGE2025 CCM tambueni ya kuwa CHADEMA ni joka kubwa lenye vichwa vingi.. Ukikata kimoja vinachipua vingine

PreGE2025 CCM tambueni ya kuwa CHADEMA ni joka kubwa lenye vichwa vingi.. Ukikata kimoja vinachipua vingine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mkuu ukituliza kichwa utajua kuwa shida haipo kwa hao kijani na njano, ila shida ipo kwa hao blue na nyekundu wanaohama na waliobaki. Kama wanahama kwa mapenzi yao, jua kuwa ndani ya chama kuna jambo halipo sawa, na kuendelea kumlaumu adui bila kutafuta ufumbuzi wa kwanini wanahama ni sawa kumpa mseto mgonjwa wa UTI.
Kama wanahama kwa kushawishiwa na pengine kwa kuhongwa kwa kodi zetu, basi jua kuwa watu wa blue na nyekundu wanahongeka hata waliobaki ni either haijaingia ofa nzuri au nafasi walizo nazo bado wana maslahi nazo.
Amini kwamba kila mtu ananunulika ila wanatofautiana dau tu. Kama blue na nyekundu wanataka kusimama imara ni lazima kwanza kuhakikisha umoja ndani ya chama, hao wanaotoka wanaenda kuuza ramani ya vita kwa adui.

Binafsi sijawahi kumwamini mwanasiasa, eti apige makelele kutetea umma, sijawahi amini hilo, wanafanya hivyo kwa sababu hio ni kazi waliyoichagu na ndio inayoleta ugali mezani, ila si kwamba wanahuo msimamo. Ipo mifano miingi ya watu waliokua shupavu kabisa ndani ya blue na nyekundu, ila ugali ulipotaka kumwagika, loyalty ya chama yote iliisha wakachagua ugali, wengine walipewa ubalozi nk.
100%
 
Naunga mkono hoja ila chama hakiwezi kuwa ni mpango wa Mungu,bali mtu ndie mpango wa Mungu,hivyo kwa Chadema Tundu Lissu ni mpango wa Mungu kupitia Chadema,ila sio mara moja wala mbili,shetani huweza kuingilia mpango ili kuutibua!,tuliona kwa Mama yetu Eva kule Bustanini Adeni!
Shetani alimjaribu hata Masiah,hivyo japo Tundu Lissu ni mpango wa Mungu, na fighting for reforms ni mapambano for a good cause, hivyo NR ni vita ya Mungu,ila NE ni shetani ameipenyeza!,hakuna mtu anaweza kuzuia uchaguzi!The Voices From Within: Tundu Lissu ni Mpango wa Mungu, NRNE ni Mpango wa Shetani, ni li Pepo! Limemkumba Lissu!, Akiachana Nalo, Anatinga Ikulu 2025! Uthibitisho Tundu Lissu ni mpango wa Mungu ni huu Unabii:Tundu Lissu aliponywa Kifo kutimiza kusudi fulani la Mungu kwa Tanzania,2025,Akiisha Timiza Tu Anatwaliwa - Huu ni Unabii wa Kweli au wa Uongo?
Uthibitisho NE ni mpango wa shetani ni huu Pre GE2025 - Lissu na kauli mbiu ya “No Reforms, No Election” ni mipango ya Mungu au ya Shetani kutusambaratisha?

Swali muhimu sana,ni kama kweli Lissu ni mpango wa Mingu,kwanini atumike na shetani bila kujijua?,sababu ni moja tuu,pepo la NE limemkumba Lissu ili kumzuia asigombee urais 2025 kwasababu Lissu ni bonge la fursa,angegombea angetusua mapema tuu asubuhi!
Lissu ni fursa Pre GE2025 - Hata Kusipofanyika Reforms, 2025 CHADEMA Ina Fursa!, Ila They Are Just Too Blind to See!, Hawajitambui! No Election ni Utopia!. Wake Up!
Tundu Lissu ni mtu wa thamani sana Chadema Thamani Kuu ya Tundu Lissu ndani ya CHADEMA ni Ipi Kati ya Uwezo wa Uenyekiti wa chama au Uwezo wa kukipeleka chama Ikulu 2025 ?

Udhaifu mmoja pekee wa Tundu Lissu Chadema,he is not a good team player hivyo is a liability Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Ila pamoja na kuwa ni a liability,some liabilities zinakuwa turned into assets zenye thamani kubwa sana!,vivyo hivyo asset iki depreciate sana inageuka liability na kuwa disposed off Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ?

P
well said, "he is not a good team player hivyo is a liability", nadhani ni ngumu sana kumbadilisha awe ni asset, kwa sababu tabia zake ni genetically inherited, je kuna uwezekana wa kufanyia genetic modification kwa maslahi ya umma??
 
"CCM wanataka tuingie kwenye uchaguzi ambao refa ni wa kwao, sisi tumekataa na CCM wametafuta watu vibaraka wakaunda chama cha kuwasaidia, wengine tulikuwa nao eti wanasema sisi ndoto zetu zinakatishwa kwa 'no reforms', chama hiki hakikuanzishwa kwa ndoto ya Heche kuwa mbunge, kimeanzishwa kwa ndoto ya wewe kuishi maisha mazuri kipiganieni chama hiki, chama hiki kina ndoto cha kukufanya uendeshe gari," - @hechejohn

#CHADEMAShinyanga
#EastAfric
FB_IMG_1747469745381.jpg
aTV
 
Upo sahihi kiongozi. Hoja yangu ipo kwenye kukosekana kwa loyalty ya kweli kwa wanachama. Hata wewe unaonekana loyal kwa sababu hujawekewa dau la size yako kuondoa hio loyalty yako kwa chama. Jambo la pili ni pengine viongozi wa juu kuna mahala wanakosea approach ya namna wanavyo tekeleza azima yao. Mkuu uongozi ni kuunganisha watu, sio kuwatawanya, ni kuwafanya waamini kuwa nikisema maji risasi itageuka maji. Wakikuamini watakua obedient, obedience inatengeza loyaty. Akili inapaswa kutulia kwanza, kuona namna sahihi ya kufanya. Kuendelea kutumia nguvu huku kondoo wakitawanyika, na kujiaminisha eti bahari inajisafisha ni kuendelea kujikaanga wenyewe tu.

kwa umri wake naamini anajua siasa ni nini, ila anaweka ukweli mfukoni na kuandika ushabiki
Akili itatuliaje wakati mtu hayuko katika mazingira ya utulivu!!??,, We unaona wapi viongozi wa chama wanakosea ili watu wasiondoke!!,??
 
Akili itatuliaje wakati mtu hayuko katika mazingira ya utulivu!!??,, We unaona wapi viongozi wa chama wanakosea ili watu wasiondoke!!,??
Baassi, nimekuelewa mkuu, kama viongozi hawajui tatizo na ninyi wanachama hamjui, basi safari bado mbichi hii. Siku mkujua ndio mtajua namna ya kuziba
 
Kuna ujinga mkubwa sana unafanywa na ccm kwa kutumia kodi zetu kutaka kukidhoofidha na kukiua kabisa CHADEMA
Hawa waliobuni hii project sijui ni akina nani huko ccm

Hivi kweli mpaka Leo ccm inashindwa kujua kwamba
CHADEMA sio TLP?
CHADEMA sio CUF?
CHADEMA sio NCCR- MAGEUZI?

Wanadhani na wanajiongopea kwamba kwakuwa walifanikiwa kuvi difuse hivyo vyama hapo juu basi wataweza kwa CHADEMA

CHADEMA ni chama kibeba maono ya Taifa la Tanganyika.. CHADEMA NI MPANGO KAMILI WA MUNGU kuliokoa taifa la Tanganyika..!

Huku wakikiyumbisha chama kwa kuwashawishi viongozi wa mikoa mbalimbali kuondoka CHADEMA.. huko mikoani mikutano ya NO REFORMS NO ELECTION chini ya Heche na timu yake inazidi kupata uungwaji mkono na wananchi wa kawaida

Hatuoni wananchi wakisusia mikutano ya no reforms no election kwakuwa tu viongozi wao wa ngazi za chini na za kati wanakihama chama..kinachoendelea na kinachotokea ccm hawaamini kabisa macho yao.. Wanebaki na press conference za kupangq huku wakichekwq na kudharauliwa na hata wana ccm wenzao wenye akili
Hivi wanashindwa kutambua kabisa kwamba CHADEMA imeshavuka level za kuwa chama cha viongozi na wanachama wachache?

Hivi wanashindwa kabisa kujua kwamba CHADEMA ina mashina lukuki kwa maelfu kiasi kwamba ukikata mmea kwenye shina moja inachipua mingine kumi?
CHADEMA kwa sasa ni imani

CHADEMA kwa sasa ni tumaini
CHADEMA kwa sasa ni furaha, ni faraja na ni mwanga wa taa kwenye giza totoro liitwalo ccm!

Wananchi wanaihitaji CHADEMA iwe mvua liwe jua kuliko viongozi wenye bei wanaonunulika.. Ndio maana kuhama kwao sio mjadala na wala wananchi hawastuki

CHADEMA ni joka kubwa lenye vichwa vingi.. Ukikata kimoja vinachipua vingine... com ni mti wa mkafiri ukiushika tu unaishia kukunukia na kukutia nuksi😂
Mwenye Chama ni Mbowe lazima akipate Chama chake
 
okay, CHADEMA itashiriki uchaguzi mkuu?
 
Wale wanaohitaji CCM Idumu milele huku Upinzani Umekufa, kuna muda utafika wataanza kufa bila kuuona Mwisho wa CCM Ikiwa kufa kwao ndio Mwisho wa CCM..
Upinzani ni imani na sio Chama.
FB_IMG_1766661064267.jpg
 
Back
Top Bottom