mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
"Wapo Wanaccm waliowekewa mapingamizi, wapo wa ACT, wapo wa CHADEMA, na majibu ya mapingamizi yalitoka, lakini kwa hatua za rufaa kwa maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Rais wa Tanzania nilipofanya naye mazungumzo, ambacho tumekiona wapo wagombea wengi sana wa vyama mbalimbali ambao waliwekewa mapingamizi katika hatua za awali.
Katika maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM, tumeelezana kuwa ni vizuri watu wapate nafasi, hivyo nitumie nafasi hii kutoa wito kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa, tunatambua umefuata sheria lakini ni muhimu kukumbuka kwamba demokrasia yetu bado ni changa, ni muhimu tuzidi kukua.
Soma Pia:
Tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI, katika hatua ya mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogomadogo ili Watanzania wengi zaidi wapate nafasi ya kugombea. Yapo makosa makubwa, kwa mfano nafasi ni maalumu kwa wanawake lakini amejaza mwanaume"