LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametoa wito kwa TAMISEMI kuhakikisha haki na nafasi za kugombea zinalindwa kwa kuzingatia demokrasia, licha ya kuwepo kwa mapingamizi mbalimbali ya awali.

Akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika Jumanne, Novemba 12, 2024, katika ofisi ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi amebainisha kuwa, kufuatia mazungumzo yake na Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Tanzania, waliamua kwamba hatua za rufaa zichukuliwe kwa umakini zaidi ili wagombea wengi zaidi wa vyama vyote wapate nafasi ya kushiriki uchaguzi. Amesema kuwa, licha ya baadhi ya makosa ya msingi, kama vile mgombea wa nafasi maalum ya wanawake kujaza mwanaume, makosa madogo yanapaswa kupuuzwa katika hatua za mwisho za rufaa ili kuimarisha demokrasia changa ya nchi.

Dkt. Nchimbi pia aliwataka viongozi wa serikali, hasa waziri anayehusika na serikali za mitaa, kufuata sheria kwa uangalifu lakini pia kuzingatia umuhimu wa kukuza demokrasia na ushiriki wa Watanzania wengi zaidi kwenye uchaguzi.
 
Maagizo ya Mwenyekiti wa CCM tumeona yapo makosa ambayo mtu amekosea mwaka wake wa kuzaliwa na mengineyo na kwa mujibu wa kisheria makosa haya hayampi mtu nafasi ya kugombea lakini tunatambua Demokrasia yetu ni changa.

Tumetambua watendaji wamefuata sheria lakini inabidi tutambue demokrasia yetu ni changa na hivyo tunaomba mamlaka kupuuza makosa madogo madogo.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi mapema leo.
Khaaaaa!!! Ccm matapeli kweli, yaani Chama kinamuagiza TAMISEMI

Hizi wizara za mfukoni hizi.
 
Maagizo ya Mwenyekiti wa CCM tumeona yapo makosa ambayo mtu amekosea mwaka wake wa kuzaliwa na mengineyo na kwa mujibu wa kisheria makosa haya hayampi mtu nafasi ya kugombea lakini tunatambua Demokrasia yetu ni changa.

Tumetambua watendaji wamefuata sheria lakini inabidi tutambue demokrasia yetu ni changa na hivyo tunaomba mamlaka kupuuza makosa madogo madogo.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi mapema leo.
Hii ni habari mbaya kwa wafuasi wa jiwe na baadhi ya wagalatia,

Samia ni Rais wa mfano
 
Jf Tuhifadhieni hii - Enzi za Mwalimu kumwambia mwenzako hana KAZI ilikuwa laana kubwa sana
Screenshot_2024-11-09-12-12-11-90.png
 
View attachment 3150391
Chama cha Mapinduzi kimetoa wito kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambayo inaratibu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutanguliza mbele haki ya Kidemokrasia na kupuuza Makosa madogo yaliyojitokeza kwa Wagombea wakati wa Ujazaji Fomu za Uteuzi

Yaani maagizo ya uchaguzi yanatoka kwenye Chama halafu tunasema tuna nchi hapa na mfumo wa demokrasia !!!! Tanzania inakatisha tamaa sana watu
 
Naona wamekubali kwamba demokrasia ni changa kwa miaka zaidi ya 60! wenzetu Kenya , Botswana, South Africa wamekuwa zaidi yetu au. Ubinafsi ndiyo tatizo letu. Tuwe wazalendo wa kweli na kuweka nchi mbele sio CCM ! na makada bali nchi
Na baadhi ya hizo nchi tumezisaidia kupata Uhuru ila soon tutaenda kujifunza kwao.
---
Nafuatilia hapo Msumbiji kinachotokea kwamba ni product ya elimu waliyo jifunza kutoka Tanzania!.
 
Maagizo ya Mwenyekiti wa CCM tumeona yapo makosa ambayo mtu amekosea mwaka wake wa kuzaliwa na mengineyo na kwa mujibu wa kisheria makosa haya hayampi mtu nafasi ya kugombea lakini tunatambua Demokrasia yetu ni changa.

Tumetambua watendaji wamefuata sheria lakini inabidi tutambue demokrasia yetu ni changa na hivyo tunaomba mamlaka kupuuza makosa madogo madogo.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi mapema leo, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Tunakutengenezea kosa alafu tunakutatulia. Siku zote utatuona wema alafu tunakupiga kwenye sanduku
 
Back
Top Bottom