LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametoa wito kwa TAMISEMI kuhakikisha haki na nafasi za kugombea zinalindwa kwa kuzingatia demokrasia, licha ya kuwepo kwa mapingamizi mbalimbali ya awali.

Akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika Jumanne, Novemba 12, 2024, katika ofisi ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam, Dkt. Nchimbi amebainisha kuwa, kufuatia mazungumzo yake na Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Tanzania, waliamua kwamba hatua za rufaa zichukuliwe kwa umakini zaidi ili wagombea wengi zaidi wa vyama vyote wapate nafasi ya kushiriki uchaguzi. Amesema kuwa, licha ya baadhi ya makosa ya msingi, kama vile mgombea wa nafasi maalum ya wanawake kujaza mwanaume, makosa madogo yanapaswa kupuuzwa katika hatua za mwisho za rufaa ili kuimarisha demokrasia changa ya nchi.

Dkt. Nchimbi pia aliwataka viongozi wa serikali, hasa waziri anayehusika na serikali za mitaa, kufuata sheria kwa uangalifu lakini pia kuzingatia umuhimu wa kukuza demokrasia na ushiriki wa Watanzania wengi zaidi kwenye uchaguzi.
Your browser is not able to display this video.
 
Khaaaaa!!! Ccm matapeli kweli, yaani Chama kinamuagiza TAMISEMI


Hizi wizara za mfukoni hizi.
 
Hii ni habari mbaya kwa wafuasi wa jiwe na baadhi ya wagalatia,

Samia ni Rais wa mfano
 

Yaani maagizo ya uchaguzi yanatoka kwenye Chama halafu tunasema tuna nchi hapa na mfumo wa demokrasia !!!! Tanzania inakatisha tamaa sana watu
 
Rubbish..🚮🚮🚮💩💩
 
Naona wamekubali kwamba demokrasia ni changa kwa miaka zaidi ya 60! wenzetu Kenya , Botswana, South Africa wamekuwa zaidi yetu au. Ubinafsi ndiyo tatizo letu. Tuwe wazalendo wa kweli na kuweka nchi mbele sio CCM ! na makada bali nchi
Na baadhi ya hizo nchi tumezisaidia kupata Uhuru ila soon tutaenda kujifunza kwao.
---
Nafuatilia hapo Msumbiji kinachotokea kwamba ni product ya elimu waliyo jifunza kutoka Tanzania!.
 
Tunakutengenezea kosa alafu tunakutatulia. Siku zote utatuona wema alafu tunakupiga kwenye sanduku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…