CCM tunahitaji kufanya reforms kwenye chama. Siasa zimebadilika sio za miaka hiyo

CCM tunahitaji kufanya reforms kwenye chama. Siasa zimebadilika sio za miaka hiyo

Magufuli alipora uchaguzi wa nani wewe kwa akili yako kwamba Lowassa alimshinda Mgufuri au Lissu alimshinda Magufuli ?Kiufupi pamoja na mapungufu yake Magufuli aliuza kwa utendaji kazi wake Mkuu acheni propaganda Kama Lissu anavyojiuza kwa Kupenda HAKI na Ufisadi basi Magufuli alijuza kwa utendaji kazi wake na pia Sio fisadi ndo maana zilikuja propaganda nyingi mara kwa Magufuli kulikutwa na Dora laki Tisa kitu ambacho ni Uongo kwa namna alivyochukiwa Magufuli ingekua balaah mara pesa China miradi yake yote ilipigwa vita but ilikua miradi ya kimkakati Achana na Magufuli Man
Tazama nimesema uchaguzi wa kuanzia lini. Na kwa taarifa yako kupora uchaguzi sio lazima uwe huwezi kushindwa, bali kupata kura zisizo na uhalisia. Ni hivi, toka Magufuli alipoingia madarakani, ndio uporaji wa chaguzi nyingi na uhuni wa kipuuzi kuharibu chaguzi, na lengo lilikuwa ionekane ccm imekubalika sana wakati wake. Uchaguzi wa 2020 mimi nilikuwa wakala kituo fulani, kura zilizopigwa hazikufika 120, ila Magufuli alipewa kura 432, huku Lisu aliyekuwa amepata kura 76 akaandikiwa kura 3. Huo ni mfano halisi, na huu uchafu ulifanyika nchi nzima. Huyu mama kichwa Nazi naye akapora kwa kuiga upuuzi ule ule wa Magufuli. Ameiga tembo kunya akapasuka msamba.

Kulikuwa na uchaguzi wa marudio hapa Dar Jimbo la Said Mtolea wakati wa Magufuli. Kwa macho yangu niliona box la kura likiletwa kituoni kwa uratibu wa jeshi la polisi, kituo cha ITV kilikuwa mubashara mtangazaji akiwa Sam Mahela. Mtangazaji alipomuhoji msimamizi wa kituo mbona box la kura linaingizwa kituoni kinyume na sheria, msimamizi kwa fedheha akawa anasema ana shughuli nyingi aulizwe polisi. Na polisi alipoulizwa akasema aulizwe msimamizi wa kituo. Baadae matangazo mubashara yakakatwa. Cha ajabu eti kituo cha ITV kwenye taarifa ya habari ya saa 2 usiku ikaomba msamaha kwa kurusha taarifa isiyo na maadili ambayo ingeweza kuharibu amani ya nchi. Tokea wakati huo hakukuwa na matangazo mubashara tena kwa vyombo vyote vya habari wakati wa chaguzi, bali vilivyoteuliwa na kutangaza yanayotakiwa tu na Magufuli. Upuuzi ule ndio ilitumika chaguzi za SM 2019 na 2020. Kipindi hicho ndio mgombea wa uhitimu wa chuo kikuu wa upinzani ilisemekana hajui kusoma na kuandika! Unaweza usikukubali, lakini kwa taarifa yako Magufuli alikuwa shetani katika umbile la binadamu. Na kwa kukusaidia Magufuli kupora chaguzi hakuanza akiwa rais tu, bali hata alipokuwa waziri. Pitia historia yake ni mara ngapi alishinda kwa chaguzi halali. Jenga tabia ya kuheshimu ukweli hata kama unauma.
 
Bila kufanya reform ndani ya CCM, chama kinaenda kupotea kabisa. Ukiangalia hata propaganda zinazotumika sasa zimepitwa na wakati. Hii ishu ya Heche imeonyesha kwamba CCM imefika mwisho kimawazo na kifikra, kwa sababu wananchi wanawahi kutambua kuwa hizi ni propaganda.

Siasa zimebadilika. CCM lazima itengeneze kizazi chenye ujasiri wa kuhoji. Kama alivyosema Mwalimu Nyerere, hata mwenyekiti wa chama anapokosea lazima kuwe na vijana wa kumhoji. Dunia inaelekea huko.

Dunia haiwezi kusimama kwa sababu wewe umekataa kutembea nayo. Wananchi wa Tanzania si wa kipindi cha uhuru. Wengi wanajua kinachoendelea, isipokuwa wamebanwa na wanaogopa kutekwa. Ndio maana hata propaganda za udini kipindi kile waliweza kuzikwepa. Sasa limekuja suala la Heche, wananchi wanajua hizi ni propaganda na wanazikwepa.

Ni muda wa CCM kufanya reform na kuja na CCM mpya itakayojikita kutatua kero za wananchi badala ya kuwekeza kwenye propaganda, wizi na ufisadi. Tunahitaji wana CCM wanaoweza kutoka kupinga utekaji, mauaji na ufisadi wakiwa na macho makavu bila woga wa kufikiria kesho yao.

Sio vijana tulionao sasa ambao wamegeuka kuwa misukule ya watawala. Wanasifia kila kitu, hata mwenyekiti wa chama akifanya kosa wao ni kusifia tu. Hatuwezi kuwa na nchi iliyojaa makasuku halafu tukategemea maendeleo. CCM ni muda wa kubadilisha siasa zetu. Nyekundu isemwe ni nyekundu, nyeupe isemwe ni nyeupe. Hata chadema walifanya reforms ndo kimefanya vizuri Chadema ya Mbowe ilikua imekaribia kukata roho Ila baada ya kufanya reform tumeona chama kimekua na nguvu za kutisha Siasa za kujificha kwenye vyombo vya dola haiwezi kutusandia
CCM sio chama bali ni cartel ya washenzi na wauaji ,wezi ,mafisadi
 
Hata mwenyekiti wao akijamba wao wanapiga makofi, Taifa la ku clap clap tu, uwa nashangaa kila kitu kupiga makofi tu.
 
Back
Top Bottom