CCM tunahitaji kufanya reforms kwenye chama. Siasa zimebadilika sio za miaka hiyo

Tazama nimesema uchaguzi wa kuanzia lini. Na kwa taarifa yako kupora uchaguzi sio lazima uwe huwezi kushindwa, bali kupata kura zisizo na uhalisia. Ni hivi, toka Magufuli alipoingia madarakani, ndio uporaji wa chaguzi nyingi na uhuni wa kipuuzi kuharibu chaguzi, na lengo lilikuwa ionekane ccm imekubalika sana wakati wake. Uchaguzi wa 2020 mimi nilikuwa wakala kituo fulani, kura zilizopigwa hazikufika 120, ila Magufuli alipewa kura 432, huku Lisu aliyekuwa amepata kura 76 akaandikiwa kura 3. Huo ni mfano halisi, na huu uchafu ulifanyika nchi nzima. Huyu mama kichwa Nazi naye akapora kwa kuiga upuuzi ule ule wa Magufuli. Ameiga tembo kunya akapasuka msamba.

Kulikuwa na uchaguzi wa marudio hapa Dar Jimbo la Said Mtolea wakati wa Magufuli. Kwa macho yangu niliona box la kura likiletwa kituoni kwa uratibu wa jeshi la polisi, kituo cha ITV kilikuwa mubashara mtangazaji akiwa Sam Mahela. Mtangazaji alipomuhoji msimamizi wa kituo mbona box la kura linaingizwa kituoni kinyume na sheria, msimamizi kwa fedheha akawa anasema ana shughuli nyingi aulizwe polisi. Na polisi alipoulizwa akasema aulizwe msimamizi wa kituo. Baadae matangazo mubashara yakakatwa. Cha ajabu eti kituo cha ITV kwenye taarifa ya habari ya saa 2 usiku ikaomba msamaha kwa kurusha taarifa isiyo na maadili ambayo ingeweza kuharibu amani ya nchi. Tokea wakati huo hakukuwa na matangazo mubashara tena kwa vyombo vyote vya habari wakati wa chaguzi, bali vilivyoteuliwa na kutangaza yanayotakiwa tu na Magufuli. Upuuzi ule ndio ilitumika chaguzi za SM 2019 na 2020. Kipindi hicho ndio mgombea wa uhitimu wa chuo kikuu wa upinzani ilisemekana hajui kusoma na kuandika! Unaweza usikukubali, lakini kwa taarifa yako Magufuli alikuwa shetani katika umbile la binadamu. Na kwa kukusaidia Magufuli kupora chaguzi hakuanza akiwa rais tu, bali hata alipokuwa waziri. Pitia historia yake ni mara ngapi alishinda kwa chaguzi halali. Jenga tabia ya kuheshimu ukweli hata kama unauma.
 
CCM sio chama bali ni cartel ya washenzi na wauaji ,wezi ,mafisadi
 
Hata mwenyekiti wao akijamba wao wanapiga makofi, Taifa la ku clap clap tu, uwa nashangaa kila kitu kupiga makofi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…