Ni hizo tu ulizozisikia kutoka kwa Tundu Lissu? Ngoja nikukumbushe...
1. Kwa miaka 5 tu serikali ya awamu ya tano imekopa zaidi ya Trilioni 40, (kama Ni kweli zimekwenda wapi?) Hoja hii inapaswa kujibiwa kwa sababu tumeambiwa mara zote kuwa makusanyo yameongezeka na miradi yetu inatumia fedha za ndani
2. Ujenzi wa Hydroelectric power kule rufiji sio jambo jipya, (japo ni zuri) kwani kuna wengine walishajenga mabwawa kama hayo na yanafanya kazi mfano, Kidatu, Mtera n.k
3. Ujenzi wa reli si Jambo jipya (japo ni zuri), kwani reli zilijengwa na watangulizi wengine, mf.TAZARA NA RELI YA KATI na waliondoka baada ya muda wao kuisha, kwa hiyo hoja kwamba yeye aongezewe muda kwa sababu hizo ni dhaifu sana
4. Kukanyagwa kwa sheria mbali mbali, ikiwemo kuwadhulumu wafanyakazi haki zao za kimsingi kama kuwaongezea mishahara, kuwapandisha madaraja (vyeo) uhamisho, kusinyaa kwa ajira n.k haya yote ameyakanyaga bila huruma,kinyume Cha sheria!
Hayo ni baadhi tu ya mengine mengi ambayo Tundu Lissu ameyazungumzia na yanapaswa kujibiwa kwa hoja, unaweza kutusaidia kujibu kwa niaba ya chama chako?