Kwani Chato siyo Tanzania?
Akijenga uwanja wa ndege huko anatumia peke yake? Hakuna uchumi huko? Hii ni sera ya chuki.
Nilisema tangu zamani. Rais Magufuli amefanya mambo mengi sana. Mtu asiyeyatambua sisi tutamtambua kama myopic ambaye atayadharau, hatayasimamia na atayaacha yapotee likiwemo suala la nidhamu kazini na uwajibikaji. Usipoona namna anaitoa nchi kwa kasi ya ajbau kutoka uchumi tegemezi kwenda kujitegemea, utakuwa mbumbumbu usiyestahili kugombea nafasi hata ya ubunge. Kama utafumbia macho namna amefumua mikataba ya wizi na kulinda raslimali zetu tutakuona wewe unalengo la kuendeleza ufsadi uliokuwa umeota ndevu na kulindwa kwa mtutu katika awamu ya nne. Kama hutaona vile amejnga hadhi ya nchi kimataifa pasipo show face, wewe utakuwa juha usiyetakiwa hata kuingia kwenye kamati ya mipango na maendeleo ya taifa. Kama huwezi kuona namna anavyokakatika kuweka uchumi imara na ajira endelevu kwa kuanza na uijenzi wa miundo mbinu sahihi, hatutaki kukusikiliza.
Siasa za chuki na visasi, havitajenga taifa wala kutaboresha maendeleo zaidi ya kuleta migawanyiko ambayo haitadumaza maisha tu bali italeta mateso makubwa kwa vizazi vyetu.
Tunataka mtu anayetambua umuhimu wa msuala aliyoyafanya Rais Magufuli ili ayalinde na kuyaendeleza.
Tunataka mtu anayeweza kujenga hoja namna atatumia misigi aliyoiweka Magufuli katika kufanya maendeleo ya taifa.
Tunataka mtu anayeweza kubainisha makamilisho ya juhudi za rais Magufuli na kuelewa namna gani atayakamilisha.
Tunataka mtu anayeelewa mapungufu ya Rais Magufuli na ajue na kueleza jnisi gani atafanya ili kufanya mapinduzi katia eneo zile.
Tunataka mtu mwenye vision inayotekelezeka na siyo matusi na kutuvuta kuturudisha nyuma.
Tunahitaji maendeleo ya taifa na si propaganda za kutaka vyeo ki ujanga ujanja kwa kutumia uelewa duni wa wananchi wa chini.
Tunahitaji nia na uwezo wa kiongozi kulindoa taifa katika hali alipolifikisha raisi wetukulipeleka mbele zaidi na si kujifanya kwamba hajafanya kitu wakati kila mtu anajua Kikwkt aliliporomosha taifa na kuliingiza katika shimo la urefu gani kwenda chini.
Ninaomba tujali utaifa na maisha ya Vizazi vyetu na siyo ubinafsi, udanganyifu na hadaa. Watu kama Membe kugombea urais wa nchi ni tusi kubwa sana kwa Watanzania. Watanzania tuwe makini na Membe.