Uchaguzi 2020 CCM tutafanya makosa makubwa kama tutajaribu kuzibeza hoja za Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 CCM tutafanya makosa makubwa kama tutajaribu kuzibeza hoja za Tundu Lissu

Tundu Lissu tayari ameshaonyesha wazi kuwa ni mwiba mchungu kwa CCM kuelekea kwenye kampeni, kwa muda mfupi aliopanda kwenye majukwaa yasio rasmi kwa ajili ya kampeni ameoneka kuwa Ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja zitakazo wabadilisha wengi mawazo hata kwa WanaCCM wenyewe.

Huyu Tundu ana uwezo mkubwa sana wa kujieleza, kujenga , na kutetea hoja kuliko watu wanavyo fikiria.

Na kwa vile Watanzania wa leo wengi hawana tena ushabiki wa vyama kama zamani, ni rahisi sana kuoambanua kile anacho kusema Lissu na yale yaliyotokea miaka mitano iliyo pita Kisha wakachukua hatua ambazo zitaweza kuishangaza hata CCM ambao wanadhani wanaweza kuhodhi utawala milele.

Ni ukweli ulio wazi tu kwamba kwa vyama vyote vya siasa watu wao watakaopanda kwenye majukwaa ya kampeni wasipojipanga vizuri Tundu atawagaragaza vibaya sana kwa hoja.

Kuna hoja dhaifu inayotolewa na makada wengi wa CCM kwamba urais hauwezi kutolewa kwa mtu kama huruma kwa sababu tu eti alipata shambulio la kupigwa risasi; huo ni udhaifu wa kujenga hoja na hilo litweza kuamsha hisia na kuwakumbusha wengi juu ya kipindi kigumu walichopitia Watanzania hapo nyuma.

La msingi kwa CCM msimbeze Lissu na kujaribu kupambana naye, bali mjipange kupambana na hoja zake ambazo kwa hakika zitakuwa kama msumari wa moto kwenye kidonda kibichi.
Wakati ule wa Lowassa silaha za kimkakati ilikuwa ni Msukuma na Kibajaji na "story" za mtu kujinyea. Sasa hapa ni hoja kwa hoja, bandika bandua. Hakuna tena ubabaishaji wala siasa rahisi, bali ni "facts" zenye kuthibitika na kuonekana kwa uwazi kabisa.
 
Kwa hakika Kuna mambo ni surprise aisee,nimeshangaa Sana kwamba eti kwa miaka 5 tu, tumekopa zaidi ya Trilioni 40!(Kama hii ni kweli) hii nchi tutakuwa tumerogwa haki ya Mungu, hivi kweli tunakopa pesa nyingi kiasi hicho zinakwenda wapi? Ndiyo haya madaraja, barabara, ndege na vivuko?

Kama ndiyo ina maana kila kitu tunafanya kwa kukopa? Makusanyo yetu yaliyoongezeka yanakwenda wapi?

Kama kweli haya yametokea, (kukopa zaidi ya trilioni 40 kwa miaka 5 tu) itakuwa ni UHUJUMU UCHUMI WA KIWANGO CHA JUU ZAIDI HAPA NCHINI!
Ndiyo maana watu wenye akili,wanaoipenda nchi yao na watoto wao wanaona kumpa Magu miaka mingine mitano ni uasi kwa nchi hii.Huyu anapaswa kuondoshwa either kwa kura au nguvu.Ya Malawi yanatakiwa kutokea hapa kwetu pia
 
Umesahau msemo kuwa, raisi wa nchi hii hapatikani kwa makaratasi ya kuwekwa kwenye box?. Wewe endelea kubwabwaja tu. Utanishawishi endapo utanambia kuwa chadamu mna katiba mpya na tume yenu ya uchaguzi siyo ile ya Dodoma. Fomu ya kugombea upewe Dodoma makao makuu ya CCM alafu ukabidhiwe Ikulu Dodoma makao makuu ya CCM? Ikulu yenyewe ndiyo imeanza kujengwa hata mjui inajengwaje ... Endeleeni kuota mchana.


Huo ndiyo ukweli japo siyo mzururi
 
Ndani ya CCM sijaona mtu wa kuzijibu hoja za Lissu!!
Kazi mnayo!!
 
Ukijibishana na chizi ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu!
Yule asiyejulikana ni mzee au kijana kweli ana uwezo wa kujibu hoja za Lissu.. wakati uwezo wa kumaliza tatizo la kura za maoni na rushwa Lumumba kashachemka.
 
Ukweli Lissu atashinda urais. Magufuli atatangazwa kuwa ndiye rais.

Watu Wana hasira za mwezi wa 11 mwaka jana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa watakomesha Kama si kulipiza.
 
Ukweli lisu atashinda uraisi. Magufuli atatangazwa kuwa ndiye raisi.

Watu Wana hasira za mwezi wa 11 mwaka jana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa watakomesha Kama si kulipiza.
Mwamko umeongezeka
 
Lissu mwepesi sana bora Lowassa alikuwa tishio...

Kwa upinzani huu wa mwaka huu USHINDI mapemaaa mnoooo...
 
Jibu hoja iliyopo mezani, acha viroja mkuu.
Hakuna hoja hapo ni uhuni wa kupotosha watz kishetani! Unapita juu ya barabara zilizojengwa kwa usimamizi thabiti wa Magu, unafika nyumba I salama kwa Kuwa nchi ni salama unaanza kupotosha ukweli unaonekana kwa macho kabisa...ni juha na mpumba-fu tu ndio anaweza fanya hayo!
 
Umesahau msemo kuwa, raisi wa nchi hii hapatikani kwa makaratasi ya kuwekwa kwenye box?. Wewe endelea kubwabwaja tu.

Utanishawishi endapo utanambia kuwa chadamu mna katiba mpya na tume yenu ya uchaguzi siyo ile ya Dodoma. Fomu ya kugombea upewe Dodoma makao makuu ya CCM alafu ukabidhiwe Ikulu Dodoma makao makuu ya CCM? Ikulu yenyewe ndiyo imeanza kujengwa hata mjui inajengwaje ... Endeleeni kuota mchana.

Vilevile mugabe aliwai kuongea hayo maneno na ni kweli zanu pf bado ipo madarakani,lakini Zimbabwe inasikisha.umeme masaa manne kwa siku.doctor wa zim analipwa laki ya tz.

Hivi unajua kwanini tra wameacha kutangaza mapato? Makusanyo yanazidi kushuka. Zimbabwe uchumi umekufa,washabiki wa zanu pf na wale walioipinga wote wamekutana Afrika kusini wakitafuta vibarua vya kufyeka nyasi huku kila mtu akimlaumu mwenzake
 
Vilevile mugabe aliwai kuongea hayo maneno na ni kweli zanu pf bado ipo madarakani,lakini Zimbabwe inasikisha.umeme masaa manne kwa siku.doctor wa zim analipwa laki ya tz. Hivi unajua kwanini tra wameacha kutangaza mapato? Makusanyo yanazidi kushuka. Zimbabwe uchumi umekufa,washabiki wa zanu pf na wale walioipinga wote wamekutana afrika kusini wakitafuta vibarua vya kufyeka nyasi huku kila mtu akimlaumu mwenzake

Hizi kauli za tra mapato yameshuka, sijui bandarini Malori hakuna yamehamia Msumbiji na blabla nyengine nyingi tulizisikia tangu 2016 hadi leo. Fisi anayesubiria mkono wa mwanadamu kudondoka
 
Sasa walivyo waajabu watamtuma Musiba kuja kujibu hii hoja bila fact. Kumbuka na CCM wakumbuke, kina Lissu, Mnyika na Zitto wapo wamejaa tela na data zoooote ambazo hata BOT wanajaribu kuficha. CCM wawe wapole na watulie waone namna ya kupambana na hoja za Lissu. Pia suala la kupambana na Rushwa ndani ya Chama litaitesa sana CCM maana hakuna aliyemsafi hata Katibu Mkuu
Na Mwenyekiti wao....
 
Umesahau msemo kuwa, raisi wa nchi hii hapatikani kwa makaratasi ya kuwekwa kwenye box?. Wewe endelea kubwabwaja tu.

Utanishawishi endapo utanambia kuwa chadamu mna katiba mpya na tume yenu ya uchaguzi siyo ile ya Dodoma. Fomu ya kugombea upewe Dodoma makao makuu ya CCM alafu ukabidhiwe Ikulu Dodoma makao makuu ya CCM? Ikulu yenyewe ndiyo imeanza kujengwa hata mjui inajengwaje ... Endeleeni kuota mchana.

Mnatumia kila vioja na vitisho kumkatisha nani tamaa?

Kwani mkisema Rais wa Tanzania hapatikani kwa kupiga kura mtamtisha nani?

Kama damu tulishamwaga. Kama risasi tulishapigwa. Kama mauti tulishaonja tukarudi kuishi tena!

Hatuna cha kuogopa tena. Nyie ndio mnaogopa. Maana hamjawahi kuonja risasi...wala mauti...wala kumwaga damu yenu kwa ajili ya nchi hii.

Ni wakati myaonje haya safari hii ili mjifunze kuheshimu haki na kuthamini uhai wa binadamu wenzenu.

Uovu haulipi siku zote. Una mwisho. Chezeeni uchaguzi huu mwaka huu muone. Maana kama ni kumwaga damu ni zamu yenu..kama ni kuonja risasi ni zamu yenu, kama ni lazima kufa ni zamu yenu pia (japo sina hakika kama na ninyi mtarudi toka wafu kama TL). Mkiiba haki ya wengi safari hii si vibaya tuchapane ili tuheshimiane. Tuanze upya na tujenge nchi kama watanzania wenye haki miliki sawa ya nchi.

Be warned!
 
Kwa hakika Kuna mambo ni surprise aisee,nimeshangaa Sana kwamba eti kwa miaka 5 tu, tumekopa zaidi ya Trilioni 40!(Kama hii ni kweli) hii nchi tutakuwa tumerogwa haki ya Mungu, hivi kweli tunakopa pesa nyingi kiasi hicho zinakwenda wapi? Ndiyo haya madaraja, barabara, ndege na vivuko?

Kama ndiyo ina maana kila kitu tunafanya kwa kukopa? Makusanyo yetu yaliyoongezeka yanakwenda wapi?

Kama kweli haya yametokea, (kukopa zaidi ya trilioni 40 kwa miaka 5 tu) itakuwa ni UHUJUMU UCHUMI WA KIWANGO CHA JUU ZAIDI HAPA NCHINI!
Mpaka April 2020, jumla ya deni la Tanzania lillikuwa trilioni 55.43. Kati ya hilo deni la ndani ni trilioni 14.85 na deni la nje ni trilioni 40.57 (chanzo ni hotuba ya waziri Mpango bungeni Dodoma mwezi june 2020)
 
in simple terms hujui , na ndo cdm walivo akili za bangi tu na ndo maaana mgombea wenu alibaki kupungia miti tu alivoenda dodoma
Hauna tofauti na waliokuwa Wana support ukoloni enzi TANU inatafuta uhuru
 
Back
Top Bottom