Uchaguzi 2020 CCM tutafanya makosa makubwa kama tutajaribu kuzibeza hoja za Tundu Lissu

Wananchi wakiamua mzee hamna wa kuwazuia
 
wacha nkuulize swali moja jepesi, unajua kwanini lazima ukope hata kama sio kwa ajili ya matumizi? ukishindwa hili swali basi we ni mbumbumbu
Usilete maskhara kwenye Mambo ya msingi, hili ni taifa kubwa linalopaswa kujengwa kwenye misingi ya haki, usawa,utu na uadilifu mkubwa!

Usifaninishe na familia yako wala ya bibi na babu yako, kwani lini tuliambiwa kuwa pesa tumekopa na tunafanya mambo haya, zaidi zaidi tunaambiwa makusanyo yameongezeka na tunatekeleza miradi mikubwa kwa pesa zetu cash,(mfano kununua ndege)

Sasa Kama huwezi kushtuka deni la taifa kupaa kwa 40 Trilioni ndani ya miaka 5 pekee, wewe utakuwa mfu kifikra!

Kasome mkopo wa Trilioni 2.7 za ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar-es-salaam, ITAKUSAIDIA!
 

Umemaliza mkuu, labda niongezee hapo, kwa kauelewa kangu kadogo najaribu kuwaza izo Trilioni 40 ni fedha nyingi sana, basi hata nusu yake ingeelekezwa kwenye kuboresha huduma za kijamii zinazomgusa mwananchi moja kwa moja, ingekuwa jambo la mbolea sana kwa upande wa Mh' Pombe.
Mfano:

>Upatikanaji wa maji safi vijijini,

>Elimu bora kwenye shule za serikali (Maabara kwenye kila shule+Waalimu wenye weledi),

>Huduma bora ya afya (madawa+Huduma bora za vipimo"vifaa vya kisasa"-Hapa nazungumzia hospitali zetu za rufaa mikoani sio lazima mgonjwa kutoka Arusha Mt' Meru Hospital kupelekwa kcmc au muhimbili), bila kusahau vituo vidogo vya afya.

Ni dhahiri wame"MISUSE" hayo mapesa na wajanja wamepiga za kwao huku walipa kodi wanapiga mihayo na kuvuja jasho juani huku wao kwenye ma-V8 yao wanakula ac na kujilipa mamilioni na hawalipi kodi. Inaumiza sana hii kitu, na huu unafiki hautaisha Tanzania bila kuwatoa hawa jamaa wamejisahau sana kwa kuishi kimazoea.

Angalau wapinzani asilimia kubwa wapo majimbo ya mijini hata wanachangamoto ndogo ndogo, sasa hawa wa ccm ukiangalia majimbo yao (Maisha ya Mbunge na Mwananchi anayemwongoza ni sawa na MBINGU NA ARDHI) kichekesho akiwa bungeni kazi yake ni kusifu na kuabudu, anajisahaulisha makusudi matatizo ya waliomtuma pale bungeni. TUAMKE WATANZANIA, HATUJALOGWA ILA TUNA HURUMA ZA KIJINGA.

#NIYEYE
 
Miundombinu unayoiona tunajenga kwa pesa zetu za ndani, alisikika Magufuli kwenye mikutano yake akiongea.
 
Viongozi wako Ile siku ya Uhuru walivyoenda jijini mwanza kwaajili ya kuomba maridhiano walikodi maji ya bahari ya Hindi kwenda Mwanza?

Halafu watu tukisema Upinzani wa Tz umejaa wanafiki wa Taifa hili mnatunanga.
Walianza hivi hivi kwenye kuchukua form, nyuzi kibao dodoma kuzizima, lissu kufunika kwa wasindikizaji.
Ilipofika siku yenyewe aibu, wakaanza kulalamikia media, sijui media ndio zilizuia watu wasijitokeze.
 
Viongozi wako Ile siku ya Uhuru walivyoenda jijini mwanza kwaajili ya kuomba maridhiano walikodi maji ya bahari ya Hindi kwenda Mwanza?

Halafu watu tukisema Upinzani wa Tz umejaa wanafiki wa Taifa hili mnatunanga.

Kwani walikodi ya ATCL?
 
Kwani walikodi ya ATCL?
Hujaelewa swali Mkuu mimi sijauliza walienda na kampuni gani Bali nimeuliza walienda na usafiri gani?

Je walienda na usafiri wa maji mnayoyataka au walienda na usafiri wa ndege msioutaka?
 
Walianza hivi hivi kwenye kuchukua form, nyuzi kibao dodoma kuzizima, lissu kufunika kwa wasindikizaji.
Ilipofika siku yenyewe aibu, wakaanza kulalamikia media, sijui media ndio zilizuia watu wasijitokeze.
Hawa CDM wakati mwingine wanahitaji Akili kidogo ili uwaelewe ukiwa na Akili timamu Huwezi kuwaelewa wanataka Nini, msimamo wao Ni upi na Sera zao za kudumu Ni zipi.
 
Msinge wafanyia roho mbaya fastjet unadhani nani angepanda humo
Inshu hapa nikwanini walipanda kitu ambacho hawataki kinunuliwe nchini si Kama siyo wanafiki kweli wangepanda Basi au wakaenda kwa usafiri wa maji wanaoyataka.

Upuuzi na ujinga wa kupinga pinga Kila kitu ndo unaufanya upinzani wa Afrika kuonekana wa hovyo kabisa.
 

Mbona mwaka 2015 alikuwa majukwaani lakini hamkuchua nchi pamoja na kuwapo lowasa?
 
Ana uwezo kujieleza kisheria, kwa kisiasa hamna kitu
 
Umeanza Vizuri kabisa Ila umemaliza kipuuzi Sana Baada ya kumaliza hoja zako kwa kuhusisha Mambo ya uchumia chama.

To be honestly Mimi Sina chama hivyo Basi siwezi kukujibu Maana Mimi siyo mwanachama na wewe unataka kujibiwa na mwanachama.

Mimi Ni raia mpiga kura tu Namkubuli Sana Mbowe, namkubali Sana Magufuli na simukubali kabisa Tundu lissu.
 
Hujaelewa swali Mkuu mimi sijauliza walienda na kampuni gani Bali nimeuliza walienda na usafiri gani?

Je walienda na usafiri wa maji mnayoyataka au walienda na usafiri wa ndege msioutaka?

Kwahiyo ulitaka waende na meli Dar-mwanza.
 
Alisema enough is enough!
Waendelee na propaganda yeye anajenga na kutetea hoja.
 
CCM hawana ubavu wa kujibu hoja za Lissu, Wamefumbwa na mazoea ya kubebwa na tume pamoja na vyombo vya dola! Mwaka huu watashangaa! Yale mambo ya kuanza kuambiana mtaisoma namba au mtapata tabu sana wakati sote tuna haki ya kufaidi rasimali za taifa letu, ule uhuni uliopitiliza! Tena safi waendelee kuimba kiwimbo chao hichoicho cha kura za huruma ili siku atakaposhinda asubuhi wapate aibu ya mwaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…