CCM waliomba kanisa Katoliki kuwaleta CHADEMA katika meza ya maridhiano!

This is very ridiculous..

Kumbe wanajua fika kuwa bila CHADEMA, hakuna kitu kinachoitwa maridhiano haijalishi watazuga na kujifanya hamnazo kwa kiwango gani..!

Hata hivyo, Ts & Cs za kuifanya CHADEMA ikubali kukaa meza Moja na wauaji hawa ziko very clear lakini hawataki kusema kinawashinda nini kutekeleza au ingalau waseme, hili tunaweza lakini hili ni gumu kwa sbb 1, 2, 3 nk...?

Mfano; Kuna ugumu gani;

1. Kuendelea kum - detain kiongozi (Tundu Lissu) wa hawa mnaowaomba mkae nao meza mmoja mtatue mgogoro kwa kesi ya bure na ya uongo kabisa? Hivi ktk hili hawa wapuuzi wanaanzia wapi hasa kuwalaumu CHADEMA kwa kukataa kushiriki mazungumzo ktk mazingira ya namna hii..?

2. Na ni kwanini wanaendelea kuwakamata na kuwafungulia viongozi na wafuasi wa CHADEMA kesi za uongo za makosa ya ugaidi ambao haupo halafu wakati huohuo mkitoa wito wa maridhiano? Does it make any sense..?

3. Vipi msuluhishi au mtu wa kati wa kuongoza hayo mazungumzo? Nalo Lina ugumu nyie CCM? Mleteni hata Yoeli Museven awe kati pale🤪

4. Na vipi kuwawajibisha walioua ndugu zetu ingalau wakae pembeni tu katika kipindi hiki.?
===
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya yake ya Wazazi kimeomba viongozi na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuingilia kati na kutumia nafasi yao ya kidini kuwaombea na kuwashawishi viongozi wa CHADEMA ili waweze kuweka pembeni kile walichokiita ukaidi na kuitikia wito wa kurejea kwenye meza ya maridhiano ya kisiasa.

Wito huo umetolewa Agosti 11, 2026 na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wakazi wa Kilosa Mjini, mkoani Morogoro, kufuatia mkutano uliofanyika Agosti 10, 2026, Ikulu ya Chamwino Dodoma, kati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Maaskofu wa TEC.

Akipongeza hatua ya Rais Samia na Maaskofu wa Katoliki kukutana na kujadili masuala ya kitaifa, Hapi alisisitiza kuwa TEC imeonyesha mfano wa kuigwa wa ukomavu wa kidemokrasia unaopaswa kufuatwa na vyama vya upinzani:

“Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA. Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi.

Pamoja na ombi hilo la CCM, msimamo wa sasa wa CHADEMA kupitia viongozi wake wakuu umekuwa ukisisitiza kuwa hawatashiriki katika mchakato wowote wa maridhiano na Serikali au CCM bila kuwepo kwa mpatanishi huru wa kimataifa asiyefungamana na upande wowote, kuachiliwa Mwenyekiti wa chama hicho taifa Tundu Lissu na kuwepo kwa ukweli na uwajibikaji kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2026.

Hata hivyo hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika alisema kuwa viongozi wa dini nchini wanaweza kuongoza mchakato huo kama wapatanishi rasmi wa ndani endapo pande zote zitakubaliana.

Kauli ya Hapi imesukumwa na kikao cha Agosti 10, 2026, ambapo Rais Samia alikutana na Maaskofu wa TEC Ikulu ya Chamwino. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa Katoliki, kujadili amani, mshikamano, na masuala yanayogusa siasa, imani, na maendeleo ya jamii na kukumbusha nafasi ya madhehebu ya dini katika kulea jamii yenye maadili na uwajibikaji.

Source Jambo TV
Huyu chawa anaongea pumba tu
 
CCM waache kanisa lifanya kazi ya kanisa.

Mana kila siku kulishambulia kanisa lina changanya dini na siasa.
 
Bila kupunguza chochote kwa nafasi/hadhi iliyonayo CHADEMA; mimi nitakwambia bla ya shaka yoyote kwamba hao ni waTanzania wanaotafutwa kuingia kwenye maridhiano.

Maana yake ni kwamba, sasa hivi ni CHADEMA ndiyo inayowakilisha matakwa ya waTanzania.

Bila CHADEMA kuhusika kwenye hayo yanayoitwa maridhiano, maana yake ni kuwa waTanzania hawajaridhia upuuzi huo.
I strongly agree with you...

Na ndio mantiki ya Uzi huu..

Maswali ya Kujibiwa:

1. Unafikiri hawa CCM na serikali yao haramu ni kwanini hawasemi chochote juu ya vigezo na masharti yaliyowekwa na CHADEMA ili kuwafanya wakae katika meza hiyo ya mazungumzo badala yake wao wanailaumu tu CHADEMA kuwa haitaki mazungumzo ya kutatua mgogoro huu wa kisiasa...?

2. Je, unafikiri kuwa mpango wa Samia na CCM yake ni kutaka uwepo wa mazungumzo na maridhiano kwa kuihusisha CHADEMA pasipo uwepo wa Tundu Lissu ambaye ndiye kiongozi mkuu wa chama hicho? Unadhani hili linaweza kuwezekanaje aisee...?

NOTE:
✓ Bila shaka mgogoro upo hapa ktk hoja #2 hapo juu. CCM, serikali ya Samia na yeye mwenyewe Samia Suluhu Hassan wanamuogopa Tundu Lissu vibaya kwa sababu ya misimamo yake na wepesi wake wa kung'amua hila na uongo wa upande wa pili.

✓ Wanatoka uwepo wa mazungumzo na maridhiano pasipo uwepo wa Tundu Lissu kwa sababu wanataka mambo yawe vilevile kama ilivyo miaka yote. Wanajua pasipo uwepo wake, wengine ni nyanya tu na watakubaliana na kila takwa la CCM kama ilivyokuwa enzi za mwamba, Mzee wa kulamba asali Freeman Mbowe..

✓ Bahati mbaya sana kwa Samia Suluhu Hassan na CCM ktk harakati zao kujaribu kulifanikisha hili, wamekumbana na kikwazo kingine ambaye kiuhalisia ni Tundu Lissu mwingine kwa tabia na misimamo na mtu asiyehongeka kirahisi yaani John Heche

✓ Na upande mwingine pressure ya Jumuiya ya Kimataifa UN, EU, Commonwealth, nchi washirika wa maendeleo nk

Watabaki na msimamo wao?
 
CCM NDIO CHAMA HATARI SANA HIV HAWA VIONGOZI WANAJIFUNGIA NA KUNYWA DAMU ZA WATU KMA ISHARA YA KUJITOLEA KUMTETEA KIONGOZ
 
This is very ridiculous..

Kumbe wanajua fika kuwa bila CHADEMA, hakuna kitu kinachoitwa maridhiano haijalishi watazuga na kujifanya hamnazo kwa kiwango gani..!

Hata hivyo, Ts & Cs za kuifanya CHADEMA ikubali kukaa meza Moja na wauaji hawa ziko very clear lakini hawataki kusema kinawashinda nini kutekeleza au ingalau waseme, hili tunaweza lakini hili ni gumu kwa sbb 1, 2, 3 nk...?

Mfano; Kuna ugumu gani;

1. Kuendelea kum - detain kiongozi (Tundu Lissu) wa hawa mnaowaomba mkae nao meza mmoja mtatue mgogoro kwa kesi ya bure na ya uongo kabisa? Hivi ktk hili hawa wapuuzi wanaanzia wapi hasa kuwalaumu CHADEMA kwa kukataa kushiriki mazungumzo ktk mazingira ya namna hii..?

2. Na ni kwanini wanaendelea kuwakamata na kuwafungulia viongozi na wafuasi wa CHADEMA kesi za uongo za makosa ya ugaidi ambao haupo halafu wakati huohuo mkitoa wito wa maridhiano? Does it make any sense..?

3. Vipi msuluhishi au mtu wa kati wa kuongoza hayo mazungumzo? Nalo Lina ugumu nyie CCM? Mleteni hata Yoeli Museven awe kati pale🤪

4. Na vipi kuwawajibisha walioua ndugu zetu ingalau wakae pembeni tu katika kipindi hiki.?
===
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya yake ya Wazazi kimeomba viongozi na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuingilia kati na kutumia nafasi yao ya kidini kuwaombea na kuwashawishi viongozi wa CHADEMA ili waweze kuweka pembeni kile walichokiita ukaidi na kuitikia wito wa kurejea kwenye meza ya maridhiano ya kisiasa.

Wito huo umetolewa Agosti 11, 2026 na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wakazi wa Kilosa Mjini, mkoani Morogoro, kufuatia mkutano uliofanyika Agosti 10, 2026, Ikulu ya Chamwino Dodoma, kati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Maaskofu wa TEC.

Akipongeza hatua ya Rais Samia na Maaskofu wa Katoliki kukutana na kujadili masuala ya kitaifa, Hapi alisisitiza kuwa TEC imeonyesha mfano wa kuigwa wa ukomavu wa kidemokrasia unaopaswa kufuatwa na vyama vya upinzani:

“Maaskofu TEC, waombeeni CHADEMA. Mungu awasaidie pepo ya ukaidi iwatoke, waende kwenye meza ya maridhiano,” amesema Hapi.

Pamoja na ombi hilo la CCM, msimamo wa sasa wa CHADEMA kupitia viongozi wake wakuu umekuwa ukisisitiza kuwa hawatashiriki katika mchakato wowote wa maridhiano na Serikali au CCM bila kuwepo kwa mpatanishi huru wa kimataifa asiyefungamana na upande wowote, kuachiliwa Mwenyekiti wa chama hicho taifa Tundu Lissu na kuwepo kwa ukweli na uwajibikaji kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2026.

Hata hivyo hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika alisema kuwa viongozi wa dini nchini wanaweza kuongoza mchakato huo kama wapatanishi rasmi wa ndani endapo pande zote zitakubaliana.

Kauli ya Hapi imesukumwa na kikao cha Agosti 10, 2026, ambapo Rais Samia alikutana na Maaskofu wa TEC Ikulu ya Chamwino. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa Katoliki, kujadili amani, mshikamano, na masuala yanayogusa siasa, imani, na maendeleo ya jamii na kukumbusha nafasi ya madhehebu ya dini katika kulea jamii yenye maadili na uwajibikaji.

Source Jambo TV
CCM wangemtumia sheikh Saidi Mwaipopo
 
Hivi mboga mboga si mara zotee wanatamba kua hata bila Chadema maridhiano yatafanyika.hii milio ni ya nini sasa?.

Wasira amesisitiza mara kadhaa kua vyama vipo vingiii mnoo mnooo.
 
Huwezi kuitenganisha CHADEMA na Kanisa Katoliki. Analotaka TEC lazima CDM waunge mkono. Hawawezi kutofautiana
Ndio sera za mazezeta wa sisiemu kuwatambua wa Tz Kwa dini zao na sehemu wanazotoka ili waendele kushukilia madaraka kwa nguvu
 
Si alisema CHADEMA ni Magaidi...watakaaje na Anti- Ugaidi-CCM..!!?
Usanii tu huo na kutaka kuhadaa UMMA kwamba CHADEMA ni Chama Cha Wakatoliki...

CHADEMA Komaeni tu Ts&Cs zenu..
 
Huwezi kuitenganisha CHADEMA na Kanisa Katoliki. Analotaka TEC lazima CDM waunge mkono. Hawawezi kutofautiana
Kwa hiyo kama chadema hawataki extra judicial killings kuna ubaya gani TEC nao wakilaani watu kutekwa na kuuawa?
 
Hakuna maridhiano bila Katoliki kwa upande wa madhehebu, na chadema kwa upande wa vyama vya siasa. Mengine ni kudanganyana.

..ukiisikiliza hotuba ya Ally Hapi utasikia KEJELI ndani yake.

..Hapi anawaomba Maaskofu wafanye maombi ili " pepo mchafu " atoke Chadema!!

..Kauli ya namna hiyo haipaswi kutolewa na kiongozi mkubwa ktk chama kikongwe kama CCM.

..Pia kwanini Hapi anawalenga Maaskofu wa Kanisa Katoliki wakati kuna madhehebu mengi nchini yanayoweza kuombea maridhiano?

..Je, ni sahihi kwa kiongozi wa CCM kuwakejeli Maaskofu wa TEC muda mfupi baada ya mkutano wao na Raisi?
 
Huwezi kuitenganisha CHADEMA na Kanisa Katoliki. Analotaka TEC lazima CDM waunge mkono. Hawawezi kutofautiana
Safi sana, na kanisa Catholic ni moja ya taasisi zinazojitambua sana hapa. Ni sifa kuwa na mtazamo mmoja na TEC.
 
Ndo huwa nawashangaa waislamu wanaodhani wanaweza kupata nafasi za juu huko CHADEMA
 
Kwa hiyo kama chadema hawataki extra judicial killings kuna ubaya gani TEC nao wakilaani watu kutekwa na kuuawa?
Hapana. Sio kama TEC hawataki jambo lazima CDM waungane nao. Sio eti wanalotaka CDM TEC walifate
 
Ndio sera za mazezeta wa sisiemu kuwatambua wa Tz Kwa dini zao na sehemu wanazotoka ili waendele kushukilia madaraka kwa nguvu
Kwani uongo?
Lini umewahi kusikia CDM wakitofautiana na TEC au Katoliki?
 
Ndo huwa nawashangaa waislamu wanaodhani wanaweza kupata nafasi za juu huko CHADEMA
Huko cdm waisilimu wanafuata vyeo au itikadi? Au waisilamu sifa ya kuwa mahali kwao ni kuwa na vyeo? Mbona kwenye mpira hamusemi wachezaji wa team ya taifa wapangwe kwa vigezo vya dini?
 
Ni kweli ni kwasababu wote wanazungumzia haki, hata rais marehemu ally Hasani Mwinyi alisomeshwa na wakatholiki , Papa kiongozi wawakatholiki amejenga uhusiano mzuri na viongozi wa kiislamu duniani
Afadhali wewe umekubaliana nami
 
Back
Top Bottom