CCM: Wananchi hawajawahi kudai Katiba mpya bali hilo ni takwa la wanasiasa kwa maslahi yao binafsi

Serikal ndio wenye wajbu na uwezo wa kufanya ayo yote.
Viongozi wa chama tawala yaani serikali unayoipa huo wajibu wameshakwambia wananchi hawataki katiba mpya, wanasiasa wachache ndo wanaitaka. Sasa maneno mengi mengi ya nn?
 
"Katiba Mpya Si Hitaji la CCM kwa Manufaa yao Kuendelea Kubaki madarakani."

Katiba iliyopo ina manufaa kwa CCM na sio manufaa kwa nchi (Tanzania).

Wananchi kutoshika mabango haina maana kwamba wananchi hawaihitaji katiba mpya; bali ni ulaghai unaotumiwa na CCM kuendelea kutetea katiba mbovu inayowalinda wao na siyo kulinda maslahi ya Tanzania.
 
Wanaosema wananchi hawataki Katiba mpya tuwapatie maoni na takwimu za walioshiriki katika maandalizi na maoni ya katiba mpya yaliyozikwa na wanakijani.
 
Sasa kama inahitajika kwann mabango yasishikwe? Kwann isipiganiwe na wanaoitaka? Utulivu wa nn iwapo viongozi hawawapi wananchi wanachohitaji?
 
Codes za kuisambaratisha ccm ni mbili.
Katiba mpya na uraia pacha hivi vitu Katu ccm haitoviruhusu,ikiviruhusu tu itakufa.
Ccm na umasikini ni kiatu na mguu.
 
Reactions: BAK
Naunga mkono hoja ya KATIBU WETU MKUU kamarada Chongolo👊

Katiba mpya ni TAKWA LA WANASIASA NA UROHO WAO WA MADARAKA......

Sisi wananchi wala hatuihitaji katiba mpya......

#SiempreSerikaliMbiliZaJMT
 
Acha kuandika ujinga wewe!!! Maccm kama wanapendwa kiasi hicho kwanini wanapora uchaguzi badala ya kushinda kihalali? Kwanini wanahofia uchaguzi HURU na wa HAKI hao wanaopendwa? Kwanini Mkapa alipotaka uchaguzi wa 2020 usimamiwe na Tume huru ya uchaguzi maccm yakaingia mitini? Acha kuonyesha ujuha wako hadharani.
 
Sisi wananchi dai letu ni tozo za miamala ya simu kuondolewa na siyo Katiba mpya kama chadema wa avyoongopa na siyo kukubali tozo za miamala ya simu kama Rais Samia anavyoongopa
 
Sasa kama inahitajika kwann mabango yasishikwe? Kwann isipiganiwe na wanaoitaka? Utulivu wa nn iwapo viongozi hawawapi wananchi wanachohitaji?
"Utulivu" wa mitutu ya bunduki na mabomu ya machozi, huo ndio unauita utulivu?

Wananchi wanahitaji uongozi wa kuwaongoza kudai Katiba Mpya. Viongozi hao mnawatia hofu na kuwabambikizia kesi za ugaidi, leo bado na akili mbovu kama hiyo unakuja hapa kudai kwamba wananchi hawahitaji katiba mpya?

Ondoa hiyo mitutu ya bunduki na mabomu, halafu uone kitakachotokea kuhusu wananchi na uhitaji wao wa katiba mpya.

Vinginevyo, endelea kukandamiza na hiyo mitutut na vitisho vyote ulivyo navyo, huku ukijidai hakuna hitaji la katiba mpya, itakapofika mahali ambapo vitisho na mitutu haitakuwa na aana yoyote kwa wananchi, hapo ndipo utakapotambua uhitaji mkubwa walionao wananchi juu ya katiba mpya.

Najuwa bado huko ndani ya CCM kutakuwa na watu wenye akili za kutosha kujuwa linakoelekea taifa letu.
 
Wananchi B kadhaa waogope bunduki zisizozidi m5 za jeshi lote?

Au ni kakikundi fulani hivi unakazungumzia?

Mm naongelea wananchi kama wale wa mikutano ya TL na EL.

Kama wale waloenda mpokea TL airport pamoja na mitutu iliyokuwepo.
 
Mbona mama yenu naye kasema wananchi ndio wameomba tozo ni lini tulihojiwa tukaomba tozo?
 
Uko ndiko kufilisika kwa chama tunakosema kila mara.chama kikongwe kilichokaa madarakani takribani miaka 60,viongozi wake wanatoa majibu mepesi kwenye swala la katiba.Uku nikuishiwa hoja kwa kiwango kikubwa.Nasio kwamba hawajui bali wanafanya makusudi kutapatapa kukinusuru chama kilichoishiwa hoja.
 
Swali ni kuwa ushawahi waona wananchi wakitoka na mabango kudai katiba? Kama wanaitaka watoke waidai hakuna haja ya kutumia mwanasiasa wa upinzani.
Hao wananchi utatumia njia gani kupata mawazo yao bila kupitia makundi maalum.Uku nikutapatapa tu kusiko na msingi wowote.
 
Huyu kaanzisha fukuto la mjadala, unaweza kula kwake
 
Hao wananchi utatumia njia gani kupata mawazo yao bila kupitia makundi maalum.Uku nikutapatapa tu kusiko na msingi wowote.
Wenye mamlaka wamekwambia, wananchi hawataki katiba. Ulimsikia? Njia pekee ya kuonyesha hawapo sahihi ni kuwaambia TUNATAKA KATIBA sio sijui mawazo kupitia makundi maalum sijui sanduku la maoni.
 
Huna unachojua wewe.hakuna dudumizi mwenye akili ata mmoja.tulia wenye akili wakusaidie kufikiri kwa ajili ya wajukuu zako.
 
Kwani CCM ilipoliweka suala la katiba mpya kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ilikuwa haijui inachokifanya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…