"Utulivu" wa mitutu ya bunduki na mabomu ya machozi, huo ndio unauita utulivu?
Wananchi wanahitaji uongozi wa kuwaongoza kudai Katiba Mpya. Viongozi hao mnawatia hofu na kuwabambikizia kesi za ugaidi, leo bado na akili mbovu kama hiyo unakuja hapa kudai kwamba wananchi hawahitaji katiba mpya?
Ondoa hiyo mitutu ya bunduki na mabomu, halafu uone kitakachotokea kuhusu wananchi na uhitaji wao wa katiba mpya.
Vinginevyo, endelea kukandamiza na hiyo mitutut na vitisho vyote ulivyo navyo, huku ukijidai hakuna hitaji la katiba mpya, itakapofika mahali ambapo vitisho na mitutu haitakuwa na aana yoyote kwa wananchi, hapo ndipo utakapotambua uhitaji mkubwa walionao wananchi juu ya katiba mpya.
Najuwa bado huko ndani ya CCM kutakuwa na watu wenye akili za kutosha kujuwa linakoelekea taifa letu.