CCM: Wananchi hawajawahi kudai Katiba mpya bali hilo ni takwa la wanasiasa kwa maslahi yao binafsi

CCM: Wananchi hawajawahi kudai Katiba mpya bali hilo ni takwa la wanasiasa kwa maslahi yao binafsi

"Wapi uliona wananchi wamedai katiba mpya, dai la katiba mpya ni letu sisi wanasiasa, hivi kupitia kupatikana kwa katiba mpya itawaletea wananchi unga? Katiba mpya inayodaiwa na wanasiasa ni kwa ajili ya kutengeneza nafasi za uongozi na madaraka"

Daniel Chongolo,Katibu Mkuu wa CCM
Tukusanye maoni ya wananchi tutapata ukweli..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo ile Tume ya Jaji Warioba ilizunguka kipindi kile kukusanya maoni kwa sababu ya takwa la Wanasiasa, na siyo wananchi!!

Ok!!!
Ukiona watu hawataki maboresho yoyote jua wanatambua yatawaumiza wao. Kila kitu kinahitaji kuboreshwa tatzo viongozi wetu hawaifikirii Tanzania ya kesho zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hiyo yale maoni ya rasim ya jaji warioba yalitolewa na watu wa india?
Hiyo ya jaji warioba si nyinyi UKAWA baada ya kuvimbiwa maposho mkakimbia? Unalaumu nini sasa hapa? Walaumu Mbowe, Lipumba, Mbatia na Slaa waliofanya kampeni ya kujitoa (baada ya kuhongwa na JK)
 
E8geW3GWUAE0F0I.jpg

Pale maccm wanapo jaribu kuzima moto kwa majani.
 
Watanzania wengi ni pumbavu, wajinga na wasiojitambua

Mwananchi =mtanzania yeyote

Na mtanzania yeyote anahaki kimsingi kutoa maoni yake, kiuchumi, kisiasa na kijamii

Hoja ya katiba mpya ni takwa la watanzania ndio maana

1. Kikwete alibariki - ccm
2. Bunge lilipitisha -ccm
3. Bunge likatenga bajeti -ccm
4. Tume ya katiba mpya chini ya jaji
warioba iliundwa- ccm
5. Tume ikazungunguuka Nchi nzima na akina Kabudi, polepole, hayati Dr. Mbungi kupata maoni- ccm
6. Rasim ya jaji warioba (ccm) ikaandaliwa
7. Bunge la katiba mpya likaundwa chini ya Marehem Samweli Sita na Samia Suluhu - ccm

Wajingawajinga ndio wanazuka na hoja za kijingajinga kupinga hoja zenye mashiko.

Katiba mpya nilazima kwa faida ya watanzania wote.
 
Hiyo ya jaji warioba si nyinyi UKAWA baada ya kuvimbiwa maposho mkakimbia? Unalaumu nini sasa hapa? Walaumu Mbowe, Lipumba, Mbatia na Slaa waliofanya kampeni ya kujitoa (baada ya kuhongwa na JK)
Kwa hiyo unathibitisha JK alikuwa mtoa rushwa?
 
Huo utafiti uliomuwezesha kuhitimisha kwamba Watanzania hatutaki Katiba Mpya aliufanya lini na katika mikoa ipi? Na ukubwa wa sample yake ulikuwa upi?

Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo amehoji kama kuna siku wananchi wamewahi kubeba mabango wakidai katiba mpya?!

Kadhalika Chongollo amehoji Tume huru ya uchaguzi inamsaidia nini mwananchi wa kawaida hadi aidai?...
 
... Tume ya Warioba ilikuwa inatekeleza matakwa ya wanasiasa na sio ya wananchi? Hili lichama lina ndimi elfu na moja! Hakika CCM ni baba wa uongo!
 
Huo utafiti uliomuwezesha kuhitimisha kwamba Watanzania hatutaki Katiba Mpya aliufanya lini na katika mikoa ipi? Na ukibwa wa sample yake ulikuwa upi?
Swali ni kuwa ushawahi waona wananchi wakitoka na mabango kudai katiba? Kama wanaitaka watoke waidai hakuna haja ya kutumia mwanasiasa wa upinzani.
 
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo amehoji kama kuna siku wananchi wamewahi kubeba mabango wakidai katiba mpya?!

Kadhalika Chongollo amehoji Tume huru ya uchaguzi inamsaidia nini mwananchi wa kawaida hadi aidai....
Wanasiasa siyo Katika kundi ndani ya wananchi, au ni wanasiasa Raia wa Kenya?

Yeye siyo Mwanasiasa?, mbona haihitaji

Maoni ya katiba ya Warioba yalitolewa na wanasiasa au Wananchi?

Ni nani alivuruga na kuedit Maoni ya wananchi katika katiba ya warioba?. Si ni wanasiasa
 
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo amehoji kama kuna siku wananchi wamewahi kubeba mabango wakidai katiba mpya?!

Kadhalika Chongollo amehoji Tume huru ya uchaguzi inamsaidia nini mwananchi wa kawaida hadi aidai...
Hivi Wanasiasa sio Wananchi?
 
Kwaiyo ule mchakato wa katiba ya warioba ulikua mchakato wa malaika walioshuka kuanzisha mchakato wa katiba mpya alafu wakaondoka.

Dah hii style tunasema mtoto kakuomba hela alafu huna badala ya kumweleza kwa utaratibu unachukia unamfukuza yaani atakuja tena mpaka utampatia hiyo hela.

CCM wanaoogopa katiba mpya kwa sababu hawataki mwenyekiti wao apokonywe mamlaka kwenye tume ya katiba inayowasaidia kushinda uchaguzi.

CCM wanaogopa kuondolewa mfumo wa chama dola ambapo unawasaidia wao kutumia vyombo vya dola kufanikisha maslahi yao
Lakini tujiulize toka 1977 mpaka Sasa kuna mabadiliko mbalimbali yametokea kiuchumi,kijamii,kisiasa ambapo kwa katiba hii imepigwa Sana viraka lakini tunaona kuna haja ya kutengeneza mpya ambayo itakishi mahitaji ya Sasa na badae
 
Akiongea na waandishi wa habari Leo 11/8/2021 ametoa maelekezo mwenye halmashauri na kisha kukaribisha maswali.
Moja ya swali ilikuwa Katiba mpya...
Jamaa linatumia maqalio kufikir, kwa hyo wanasiasa sio wananchi?

Na Kama wanasiasa sio wananchi, wamepewaje dhamana ya uongozi??

Kwamba daktar sio mwanachi? Kwamba mwalimu sio Mwananchi?

Halijui tofauti na uhusiano Kati ya cheo na uananchi?!!!!

Tatizo la CCM viongozi wao %kubwa wanatumia akil za kuazima maqalion na sio kichwa!

Taifa limekula hasara kabisaaah kuongozwa na CCM
 
Wananchi au watanzania kwa ujumla vipaumbele vyetu ni maendeleo, amani, upendo na umoja. Hili swala la katiba mpya linataka kutumiwa kama uchochoro na wanasiasa uchwara ili kupiga hela katika vikao vya katiba.

Inajulikana kwamb wanaodai katiba ni wale walioshindwa vibaya ktk uchaguzi mkuu, kwa maana hiyo hawana ruzuku wala mshahara wowote wanaoupata kupitia bunge kama walivyozoea miaka ya nyuma.

Sasa wanataka kupiga hela kupitia bunge la katiba ili wajaze matumbo yao. Nasema tena watanzania katiba sio kipaumbele chetu. Sisi tunachotaka ni maji safi, shule na hospital zijengwe kwa wingi hasa vijijini, barabara nzuri, mazingira mazuri ya kufanyia biashara na ajira.
 
Back
Top Bottom