CCM: Wananchi hawajawahi kudai Katiba mpya bali hilo ni takwa la wanasiasa kwa maslahi yao binafsi

CCM: Wananchi hawajawahi kudai Katiba mpya bali hilo ni takwa la wanasiasa kwa maslahi yao binafsi

Amesema raia wa kawaida...Kuna raia wa makundi mbalimbali, wanasiasa,wafanyakazi, wasomi etc...Kama kudai mishahara huwa raia wanadai? Acheni upotoshaji...Fanyeni siasa raia wawaamini kwanza, wakishawaamini hamuhitaji katiba wao wenyewe watawapa nchi na mtaandika hiyo katiba kama ndiyo objective ya chama chenu
Hakuna cha kinachoitwa wananchi wa kawaida.wananchi ni binadamu wote wenye uraia wa nchi.hizo zingine ulizotaja ni majukumu tu ya kawaida ya kila siku.ata rais wa nchi ni mwananchi.Ata katiba ya sasa inamaboresho kadhaa na nia ya marekebisho hayo ilitolewa na makundi mbalimbali ndani ya jamii.na hayo makundi kwapamoja ndio wananchi wenyewe.msitake kuwapa jina wale mnaowaita wanyonge kua ndio wananchi kwa vile tu wana umaskini
 
Wananchi B kadhaa waogope bunduki zisizozidi m5 za jeshi lote?

Au ni kakikundi fulani hivi unakazungumzia?

Mm naongelea wananchi kama wale wa mikutano ya TL na EL.

Kama wale waloenda mpokea TL airport pamoja na mitutu iliyokuwepo.
Sielewi unakwenda wapi na maelezo yako haya hapa.

Kama unaridhika nayo kwamba ndio ushahidi unaowapa matumaini ya kuendelea kuwakandamiza waTanzania, sina sababu ya kukushawishi vinginevyo. Kaa nayo hivyo hivyo yakufaidishe mwenyewe.
 
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo amehoji kama kuna siku wananchi wamewahi kubeba mabango wakidai katiba mpya?!

Kadhalika Chongollo amehoji Tume huru ya uchaguzi inamsaidia nini mwananchi wa kawaida hadi aidai?

Kimsingi katiba mpya ni dai la wanasiasa kwa maslahi yao na siyo hitaji la wananchi kwa sasa a esisitiza Chongollo

Source: Channel ten

My take; Nakubaliana na Katibu u
Hivi wanachama wa CCM ndio wanaoitwa wananchi pekee wa nchi hii?
 
Katibu mkuu wa CCM ndugu Chongollo amehoji kama kuna siku wananchi wamewahi kubeba mabango wakidai katiba mpya?!

Kadhalika Chongollo amehoji Tume huru ya uchaguzi inamsaidia nini mwananchi wa kawaida hadi aidai?

Kimsingi katiba mpya ni dai la wanasiasa kwa maslahi yao na siyo hitaji la wananchi kwa sasa a esisitiza Chongollo

Source: Channel ten

My take; Nakubaliana na Katibu u
utopolo
 
Sielewi unakwenda wapi na maelezo yako haya hapa.

Kama unaridhika nayo kwamba ndio ushahidi unaowapa matumaini ya kuendelea kuwakandamiza waTanzania, sina sababu ya kukushawishi vinginevyo. Kaa nayo hivyo hivyo yakufaidishe mwenyewe.
Huwezi kunielewa.

Ila ujumbe ulitolewa leo ni kuwa humu nchini hakuna mwanasiasa atakayetoa kafara maslahi yake ya kiutawala ili ampatie maslahi mwanasiasa mwingine, katiba mpya ni fursa ya maslahi kwa baadhi ya wanasiasa na hatari ya kupoteza kwa baadhi ya wanasiasa hivyo kama kweli katiba unaihitaji sana, simama na wenzio ipiganie bila kutumia mwanasiasa.
 
Akumbuke mwenyekiti wake kwa sasa, alikuwa mwenyekiti wa Bunge la Katiba.
 
Sheria ya bunge ya mwaka 2012 inatambua uwepo wa mchato wa kupatikana kwa katiba mpya. Tume iliundwa na mabilioni yalitumika katika mchakato na wananchi tulitoa maoni yetu. Bunge la watu zaidi ya 500 lilikutana na wakala posho za kutosha. Waliokuwa wajumbe wa bunge lile ni viongo wote wa sasa kuanzia Rais, waziri mkuu, Kabudi, Polepole n.k. Why leo waseme wananchi hatuhitaji katiba?
Ata sasa hivi viongozi wote na wafuasi wa ccm wanaojifanya hawataki katiba mpya nikwasababu rais kaonyesha haina haja kwa sasa,siku rais atakayosema kuwe na mchakato wa katiba mpya utawaona nawao wanabadilika.
 
Wakati CCM inabebwa na wajumbe wa nyumba10 na kaya zao CHADEMA wanabebwa na mbowe

Halafu ikifika kwenye kura anatafutwa mchawi

Na ikifika kwenye maandamano kina Tundu wanakimbia halafu wanasema andamaneni[emoji849][emoji849]
Ccm ingekua inabebwa na wajumbe wa nyumba 10 kamwe tusingeona kile kituko cha uchaguzi uliopita.mkavuruga hadi mitandao.Hicho chama ni sawa na mbwa mzee aliyeng'oka meno,kinajitutumua kikiwaona polisi na vyombo vya dola na serikali.ukiondoa hivyo hakuna kitu ata kubweka hawezi.
 
Ila ndiyo kinakuongoza wewe mwerevu, sasa jitathmini unakaaje nchi ya wajinga? Kama mjanja si ungekuwa wewe mtawala basi?
Ccm wamerithi nchi wala hakuna jipya.na muda wakulilia mali yakurithi ndio unaishilia hivyo na hawawezi tena kupambana kutafuta zao kwa nguvu zao ndo maana tunaona wakitumia polisi kujibu hoja.ila hilo haliwezi kuwasaidia milele.
 
Serikal ndio wenye wajbu na uwezo wa kufanya ayo yote katiba mpya na mengine haiitajik mabango wala mvutano kama suhala lina umuhimu lifanyike kama uku kusema et wananchi hawajatoa mabango sio kigezo ilo suhala la katiba lipo na watu wakitenga bajet posho zikaliwa na pia kuna sehem limeishia je unataka kusema hao waliotenga bajet kipind iko hawakua viongoz wa serikal hii au katiba ya nchi haitungw au kufanyiwa marekebisho mpaka watu waingie barabaran na mabango ,na nan atakaekubal ilo jambo lifanyike ,na je iyo katiba ya mwaka 77 kwan wananchi ndio wote waliingia mitaan na mabango ad ikatungwa ,na lin serikal kupitia vyombo vyake ilitangaza kwamba wanasubr watu waingie mitaan na mabango alaf ndo waruhusu mchakato wa katiba uendelee ,nimekutolea mfano wa tozo kwa sababu sio kila jambo serikal inafanya kisa wananch wametaka au wameandamana serikal mara nying inafanya vtu pale tu inapoona ili jambo lina manufaa na linafaa sio kwa mabango wala maandamo
Naona unajitahidi sana kuelimisha huyo poyoyo.Wanafanya makusudi tu kuunga kila kauli inayotolewa na viongozi wao bila ata kutumia zao kufikiri.sio makosa yao ni ujinga tu unawasumbua.
 
Swali langu,

1. Mwananchi ni yupi?

2. Mwanasiasa ni yupi?

3. Kudai katiba kunahalalisha vipi kuwa huyu ni mwanasiasa?
Hapa ndipo unapoweza kuelewa kuwa zaidi ya 99% ya Journalists wa Tanzania ni maamuma na makanjanja kwa 100%....

Yaani wanaitwa na kiongozi wa umma, anamwaga ujinga wake mbele yao, wanamuuliza maswali magumu yenye maslahi kwa umma, anawajibu kunya, kirahisi na kipropaganda wanamwacha aende free bila kumtoa jasho...

Yaani waandishi wa habari wa Bongoland au Bongolala wanalishwa pumba na matango pori nao kama wajinga na wasioenda shule wanakubali tu...

Tafsiri ya hii, maana yake ni kuwa, kiongozi huyu anawatazama na kuwaona waandishi wote aliowaita kuripoti habari yake kuwa ni wajinga, wapumbavu na mabongolala tu....!!

Ndiyo. Likely ndivyo walivyo...

Mfano; sijui ni kwanini tu waandishi wetu hawa walishindwa kumuuliza maswali muhimu na magumu kama haya na wahakikishe anatoa majibu sahihi na ya kuridhisha...

Waandishi wa habari hakikisheni mna uelewa wa kutosha wa mambo ya katiba na kisheria, elimu, biashara, afya, michezo, current trending affairs globally nk nk mnapokwenda kuhojiana na viongozi ili kuepuka kuripoti ujinga na upumbavu wa viingozi hao kwa kuwa wanakuwa wameshawatambua kuwa nyie ni maamuma, hamjui lolote....!!

Mkiwa na ufahamu huu, watawaheshimu na hawatakuwa wanakutana nanyi kuzungumza na vyombo vyenu vya habari huku wakiwa wamelewa mvinyo wa madaraka yao...

Poor Tanzanians journalists....!!
 
Hapa ndipo unapoweza kuelewa kuwa zaidi ya 99% ya Journalists wa Tanzania ni maamuma na makanjanja kwa 100%....

Yaani wanaitwa na kiongozi wa umma, anamwaga ujinga wake mbele yao, wanamuuliza maswali magumu yenye maslahi kwa umma, anawajibu kunya, kirahisi na kipropaganda wanamwacha aende free bila kumtoa jasho...

Yaani waandishi wa habari wa Bongoland au Bongolala wanalishwa pumba na matango pole wanakubali tu...

Tafsiri ya hii, maana yake ni kuwa, amewaona waandishi wote aliowaita na wajinga, wapumbavu na mabongolala tu....!!

Mfano; sijui ni kwanini tu waandishi wetu hawa walishindwa kumuuliza maswali muhimu kama haya na wahakikishe anatoa majibu sahihi na ya kuridhisha...

Poor Tanzanians journalists....!!
20210811_214253.jpg
 
Does it relate in anyway with what I just commented? If you can, try to explain how... Thanx
Waandishi wa habari wameshughulikiwa vilivyo kwa kipindi kirefu, wapo crippled not only financially lakini pia mentally ndio maana wanashindwa kuuliza chochote cha maana, wanaitwa kama formality na yoyote atakayeamua kutekeleza majukumu yake ataitwa "radical" na "atafundishwa" namna anatakiwa afanye kazi yake...akiamua kuwa independent pia ataonyeshwa "ugumu" wa kile anachojaribu kufanya.
 
Huwezi kunielewa.

Ila ujumbe ulitolewa leo ni kuwa humu nchini hakuna mwanasiasa atakayetoa kafara maslahi yake ya kiutawala ili ampatie maslahi mwanasiasa mwingine, katiba mpya ni fursa ya maslahi kwa baadhi ya wanasiasa na hatari ya kupoteza kwa baadhi ya wanasiasa hivyo kama kweli katiba unaihitaji sana, simama na wenzio ipiganie bila kutumia mwanasiasa.
Usinifanye kuwa kilaza kama wewe usiyeelewa kitu.

Lakini ngoja nikusifu kwa kutambua hili uliloandika hapa mwenyewe, kama kweli unaelewa ulichoandika:

"Ila ujumbe ulitolewa leo ni kuwa humu nchini hakuna mwanasiasa atakayetoa kafara maslahi yake, ya kiutawala ili ampatie maslahi mwanasiasa mwingine"
Kama unaelewa maana ya maneno hayo uliyoandika hapa, sina sababu kabisa ya kuhangaika na wewe, ila kwa jambo moja tu usilolielewa vizuri kama inavyoonyesha kukomalia kwako kwa jambo hili.
Maslahi ya Tanzania (waTanzania), kamwe usiyachanganye na maslahi ya wanasiasa, iwe CCM, CHADEMA au chama kingine chochote cha siasa.

Wananchi wataungana na chama chochote/ kundi lolote litakalosimamia matakwa yao kuondoa dhulma za wazi amabazo sasa CCM wanaonyesha kwa wananchi wa nchi hii.

Wewe utaendelea kuimba hapa ukidharau juhudi hizo zinazofanywa kwa njia mbalimbali, ikiwemo na kujifanya kwamba wananchi hawana mahitaji ya Katiba Mpya, kwa vile tu kundi lako la utawala linafaidika na hali hiyo. Kuwa kipofu kwa maksudi hiyo ni hiari yenu, lakini haitazuia mabadiliko yanayokuja kuwafyekea mbali kama hamtazinduka toka kwenye ndoto hizi mbaya zinazowasumbua wakati huu.

Unadai hapo juu, kwamba hakuna wananchi wanaoweza kukabili bunduki milioni tano. Nikuhakikishie kwamba haihitajiki wananchi milioni tano; laki tano hadi milioni moja inatosha kabisa kuwatupilia mbali wavunja haki za waTanzania nyinyi mliolewa madaraka.

Safari hii hamponi.
 
Back
Top Bottom