Pre GE2025 CCM wapinga kauli ya Nape Nnauye kuhusu imani yake kwenye ushindi wa chaguzi nchini, wasema CCM haihitaji mbeleko

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Nilionya kwamba Kauli ya Nape hata kama ametoa kimasihara ila inaweza kuondoa Imani Kwa mfumo wa Demokrasia na taasisi zake hivyo haifai na inatakiwa kupingwa na kukemewa.

Baada ya Kauli hiyo CCM Kupitia Mwenezi wake na Itikadi imeoinga Kauli hiyo na kusema Chama hicho hakihitaji Mbeleko kushinda uchaguzi kwani kina rekodi za utendaji wa kuwaletea maendeleo Wananchi na Kila mmja anaona.👇👇


My Take
Nape aombe radhi au Rais ampige chini,huku ni kulewa madaraka.
 
Alichosema Nape ni ukweli, na ameusema makusudi akijua wazi hatuwezi kuwafanya chochote, ndio maana amesema kwa kebehi na jeuri.

Anachokisema Makalla ndio uongo, na atapata dhambi kwa Mungu, CCM ni wezi najua hivyo, wao wanajua, Makalla anatudanganya.
 
Nape ni mwizi wa hela za wananchi. Na amekiri kabisa kwamba ana makampuni ya simu yanayoweza kukata hela za wateja ili kujenga soko. Kumbe ndio maana tunajikutaga tu tumekatwa hela bila makubaliano. Ipo siku ukweli wote utawekwa wazi.
 
Kinywa cha mtu hutoa yaujazao moyo wake,Nape yuko sahihi alichosema ndicho CCM inafanya miaka yote. Ni Nape huyu huyu aliyesema 2015 kuwa CCM inashinda hata kwa goli la mkono.
 
Amosi Makala anajikosha tu. Sio mara ya kwanza kwa Nape kusema hivyo, alishawahi kutamka kwamba CCM wanashinda hata kwa bao la mkono, so ni kawaida yao kupata ushindi haramu.

Ikumbukwe Nape amewahi kuhudumu nafasi aliyonayo komredi Makala kwa sasa, so anaongea kutokana na uzoefu.

Hata saa mbovu kuna wakati inakuwa sahihi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…