CCM watatoka madarakani kwa njia ya kura ni muhimu kujiandikisha na kupiga kura

CCM watatoka madarakani kwa njia ya kura ni muhimu kujiandikisha na kupiga kura

Kauli za wapinzani kuimba CCM wanaiba kura au hawezi toka kupitia boksi la kura hazina Afya kabisa .Muitikio wa kujiandikisha umekuwa mdogo sana kwa baadhi ya maeneo .

CCM wanatumia nguvu kubwa kuhakikisha kila mwanaCCM anajiandikisha kupiga kura , Upinzani unatumia nguvu kubwa kuaminisha wanachama wao kuwa CCM wanaiba kura na hawezi kutoka madarakani kwa uchaguzi.

Kauli hizi zinaipa ushindi CCM maana wanaCCM wakipiga kura wanashinda , Upinzani tunakimbilia kusema wanaiba hatupigi kura .

Hapa JF tu sidhani kama kuna hata 5 % ya watu washawahi piga kura uchaguzi wa Serikali za mitaa huko .lakini bado CCM akishinda utasikia kaiba .

Ukiachana na 2020 ambapo hayati Magufuli aliamua kutimiza ahadi yake ya kutorudisha upinzani bungeni baada kumdharau , Upinzani ulikuwa unaingia bungeni , unapata madiwani japo kwa kulinda kura .

Mi nadhani tuendelee kuamini katika boksi la kura sio kila siku CCM itakuwa imara na dola itakuwa upande mmoja , kuna siku yaja CCM itaanguka kama vilivyoanguka vyama vingine.

Kutojiandikisha na kutopiga kura kunaipa Mwanya ccm kupita kihalali lakini pia inakuwa rahisi kufanya udanganyifu .
Una kichaa
 
Back
Top Bottom